HUU HAPA MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA DR.JOHN POMBE MAGUFULI. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, April 02, 2016

HUU HAPA MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA DR.JOHN POMBE MAGUFULI.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli jana alimpigia simu mtangazaji wa kipindi cha ‪Clouds360‬ cha ‪‎CloudsTv‬, Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa Rais.

Rais alisema mshahara alioukuta na ambao analipwa  ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000)   na  wala  sio milioni 30  kama  wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360.

Aliahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.

Gazeti  la  Nipashe toleo  la jana  lilikuwa na habari  iliyowanukuu Tundu Lissu  na  Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .
 
Hivi karibuni, Dk. Magufuli ameahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa zaidi usizidi kiasi hicho.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us