SNURA AFUNGUKA MAJANGA ILIVYOMSABABISHIA KUTAPELIWA | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, June 08, 2016

SNURA AFUNGUKA MAJANGA ILIVYOMSABABISHIA KUTAPELIWA


Stori: Gladness Mallya

STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi ambaye alipata kiki ya aina yake kwa kibao chake cha Majanga, amefunguka kuwa licha ya kupata shoo nyingi kupitia ngoma hiyo, lakini pia alipata majanga kwa kutapeliwa mara kadhaa.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Snura alisema promota mmoja alimpeleka kufanya shoo mkoani Kilimanjaro na Mererani Arusha, lakini baada ya kuwa ameshafanya kazi, mtu huyo alimkimbia bila kumpa chake, kiasi kwamba alilazimika kurejea Dar kwa lifti.

“Sitasahau, nilisaidiwa lifti mimi na wacheza shoo wangu kutuleta Dar, lakini baadaye nilikuja kumpata huyo promota, nikamnyang’anya pete ya ndoa na uchumba, ninazo mpaka leo maana hakunilipa,” alisema Snura.
Source GPL

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us