Bella, Wema, Idris Walivyofunika Katika Black Tie | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, July 11, 2016

Bella, Wema, Idris Walivyofunika Katika Black Tie









































Usiku wa kuamkia leo, staa wa Bongo Muvi, Wema Abraham Sepetu pamoja na mwandani wake, Idris Sultan waliiongoza shoo ya Black Tie iliyokuwa maalum kwa King Of The Best Melodies, Christian Bella iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa King Solomoni, Kinondoni jijini Dar.

Katika shoo iliyohudhuriwa na mashabiki kibao, Bella alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 10 tangu aingie kwenye muziki nchini ambapo aliungwa mkono na mashabiki na mastaa kibao wa muziki wa Dansi, Bongo Fleva pamoja na Bongo Muvi wakiongozwa na Irene Uwoya, JB, Steve Nyerere, Shilole, Jacqueline Wolper, Linah, Barnaba, Faiza Ally, Odama na wengine kibao.

Shoo hiyo iliyoandaliwa na rafiki wa karibu na Wema aitwaye Muna (Muna Logistic), ilianza mida ya saa nne za usiku kwa burudani kutoka kwa msanii Nandy na baada ya hapo alifuatiwa Linex kisha Linah na kumalizia kwa Barnaba ambaye aliwakumbusha mashabiki Wimbo wa Barua aliouimba zamani na Linah.

Ulipofika muda wa saa nane kasoro, Bella aliingia jukwaani na kufunika ambapo alipiga nyimbo zake zote kali kuanzia yapo wapi mapenzi, Nagharamia na nyingine kibao.

Baada ya Bella kufanya shoo ya kwanza, alimpisha Wema na Idris ambao kwa mara ya kwanza walipanda na kutambulisha waandaaji wa shoo hiyo.

“Tunawapongeza Muna Logistic lakini pia nimpongeze Bella kwani ndiye msanii pekee aliyeweza kutamba kwa muda mrefu bila kuchuja.

“Bella ameaandaliwa CD, DVD za muziki wake tangu alipoanza na kufikisha hiyo miaka 10,” alisema Wema Sepetu akiitikiwa na Idris.

Kilichofuta baada ya hapo, Walifungua shampeni spesho (za makaratasi ya kung’ara) ambazo zilipendezesha ukumbi wote na kulipukwa kwa furaha.

Baada ya kushuka kwa Wema na Idris, MC mwingine aliyekuwa akiongoza shoo hiyo, Gardner G. Habash aliruhusu shoo kuendelea kwa Bella ambapo kivutio kikubwa kilikuwa pale alipopanda na kuanza kuimba Wimbo wa Nani Kama Mama huku akitaja jina la msanii mmojammoja ambaye ameguswa na wimbo huo kuja kutoa chochote na baada ya hapo kilichofuatiwa ni mvua ya hela kutoka kwa mastaa kibao wakiongozwa na Alawi Junior.

Mbali na shoo hiyo, kivutio kingine kilikuwa ‘red carpet’ ambayo ilikuwa kitofauti na iliyoongozwa na baadhi ya mastaa wakiwemo Miss Tanzania, Lilian Kamazima.

Imeandaliwa na Andrew Carlos na Musa Mateja/GPL

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us