LULU MICHAEL ASEMA HANA BIFU LOLOTE NA HAMISA MOBETO | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, July 20, 2016

LULU MICHAEL ASEMA HANA BIFU LOLOTE NA HAMISA MOBETO

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha tetesi za kwamba ana bifu na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Dj Majay, Hamisa Mobeto.

Muigizaji huyo ambaye kwa saa anadaiwa kutoka kimapenzi na Majay, aliingia kwenye malumbano na baadhi ya mashabiki wa Mobeto katika mitandao ya kijamii wakimtuhudi kuiba bwana.

Akiongea katika kipindi cha Weekend Chart Show cha Clouds TV Ijumaa iliyopita, Lulu amesema hata tatizo na Mobeto ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Majay.

“Sipendi sana kuongelea issue ambayo nitakuwa kama nachochea, mimi ni mtu fulani very peace, very very peace, sina tatizo naye,” alisema Lulu.

Akiongelea kama ni kweli kuna watu walikuwa wanatumwa na Mobeto ili wamtukane alisema “Siwezi kujua kwa sababu sijafuatwa direct, lakini sina tatizo naye, mtu akinipa kijembe namchukulia kama mtu kanipa kijembe”

Hata hivyo, Lulu na CEO wa EFM, Dj Majay kwa sasa wapo karibu zaidi, kwani wawili hao wamekuwa wakipost picha zao katika mitandao ya kijamii wakiwa pamoja.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us