Tukio la Ujambazi lililofanikiwa zaidi, kusisimua na kuushangaza Ulimwengu | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, July 24, 2016

Tukio la Ujambazi lililofanikiwa zaidi, kusisimua na kuushangaza Ulimwengu

Mwaka 2003 lilitokea tukio kubwa zaidi la ujambazi ambalo labda ndio lililotumia akili na maarifa zaidi pengine kushinda tukio lolote la ujambazi kwa miaka 50 iliyopita.. Tukio hili lilishuhudia wahusika wakitokomea na vitu vyenye thamani ya zaidi ya Bilioni 200 (100 mln USD)!
Uthubutu, ubunifu, akili na maarifa yaliyotumika kutekeleza tukio hili limefanya mpaka kampuni ya utengenezaji filamu ya Paramount Pictures kununua haki za hadithi ya tukio hili ili watengeneze filamu itakayo husu mkasa mzima wa tukio hili..

TUKIO LENYEWE

Mwanzoni mwa mwaka 2000 mfanyabiashara wa madini (almasi) Leonardo Natarbartolo alifungua ofisi mjini Antwerp nchini ubelgiji, mji ambao ndio kituo cha biashara ya madini ya almasi ulimwenguni.. Ofisi yake ilikuwa katikati kabisa ya kitovu cha mitaa ambayo ndio hasa biashara ya almasi hufanyika. Natarbartolo alijihusisha hasa katika manunuzi ya kiwangi cha kawaida cha almasi (small deals) lakini jambo ambalo watu hawakulifahamu ni kwamba walikuwa wamemkaribisha moja kati ya manguli wa wizi wa almasi ulimwenguni!
Kutokana na kujitambulisha kama mfanya biashara mwenzao, Natarbartolo alipata fursa ya kuingia katika Kuba (vault) za wafanyabiashara wengine ili aweze kukagua mali kabla ya kuinunua na aliutumia fursa hii kuyasoma mazingira ya Ofisi hizo zilizo hifadhi madini na kuja kufanya uhalifu kesho yake..
Natarbatolo aliishi hivi mjini Antwerp kwa miezi kadhaa kabla hajakutana na mfanyabiashara ya almasi Myahudi ambaye kukutana kwao kulipelekea kufanikisha tukio ambalo liliushangaza ulimwengu na limeendelea kuushangaza ulimwengu mpaka leo hii..



MAANDALIZI

Mwaka mmoja baada ya Natarbatolo kuingia Antwerp, siku hiyo akiwa kwenye mgahawa akinywa kahawa alifuatwa na Mfanyabiashara wa Kiyahudi ambaye alimuomba wazungumze faragha kuhusu biashara muhimu. Baada ya kukaa nae chemba Myahudi akamueleza amza yake kuwa anataka amshirikishe katika tukio la ujambazi na alimuuliza kama anahisi Vault ya Antwerp Diamond Center inaweza kuibiwa... Natarbartolo akamjibu kwa kifupi kuwa atamjibu swali hilo kama yuko tayari kumlipa dola laki moja! Na Myahudi huyo akakubali

Siku mbili baadae Natarbatolo alielekea ilipo Main Vault ya Antwerp Diamond Center (kumbuka kutokana na yeye kujitanabaisha kama mfanyabiashara ya almasi kwa mwaka mmoja aliokaa Antwerp hivyo alifanikiwa kujisajili ili aweze kuhifadhi almasi zake katika Main Vault ya Antwerp)..
Kitu ambacho watu wote wakiwepo walinzi hawakikugundua ni kwamba katika mfuko wa pembeni wa suti yake aliweka peni ambayo inaonekana kama peni ya kawaida lakini ilikuwa ni peni maalumu iliyokuwa na kamera ndogo ya siri.. Kamera hii ilimsaidia Notarbartolo kurekodi mandhali yote ya ndani ya vault na jinsi ulinzi ulivyo...
Kesho akajutana na yule myahudi na kumpa jibu lake kuwa ni immposible kuvunja na kuiba main vault ya Antwerp inayohifadhi almasi zote zilizopo katika mji huo.. Akampa ile peni ambayo imerekodi mandhali ya Vault pia akampa na maelezo ya mdomo kwanini haiwezekani kuiba katika ile vault na akamsisitiza zaidi juu ya matabaka ya ulinzi (security levels) ambayo yana protect vault hiyo. Matabaka hayo yapo kama ifuatavyo..

1) Combination dial ambayo unatakiwa uingize tarakimu nne za siri

2) Sehemu ya kuingiza funguo maalum

3) Sensor ya mitetemo (seismic sensor)

4) geti la Chuma lililo sambamba na mlangi

5) sensor ya sumaku (magnetic sensor)

6) Kamera ya nje ya mlango

7) Keypad ya kuzima alarm

8) sensor ya mwanga (light sensor)

9) Kamera ya ndani ya vault

10) sensor ya joto na mjongeo (heat & motion sensor)

Jumlisha; walinzi na ulinzi unaozunguka jengo hilo.. Natarbartlo akmsisitizia yule myahudi "..it is immposible to rob the Antwerp diamond center vault"..

TUKIO LILIVYOTEKELEZWA

Miezi kama mitano ikapita ndipo Notarbartolo akapokea simu kutoka kwa yule myahudi na safari hii alimuomba wakutane nje kidogo ya mji wa Antwerp... Baada ya kuonana yule myahudi alimchukua Notarbatolo mpaka kwenye nyumba moja inayofanana na ghala kubwa.. Ndani yake Notarbatolo alikuta kitu ambacho hakutegemea kabisa... Yule myahudi alikuwa ametengeneza replica inayofanana kabisa na main vault halisi ya kuhifadhia almasi ya hapo mjini Antwerp.. Pia akamtambulisha kwa watu watatu ambao pia aliwakuta hapo! Natarbartolo amekataa kabisa mpaka leo hii kutoa majina halisi ya watu hawa lakini anawasimulia kwa nicknames walizokuwa wanatumia, kulikuwa na The genius (huyu ni mtaalamu wa mambo ya kidigitali na eletroniki), kulikuwa na The monster ( huyu alikuwa ni mekanika na mtaalamu wa umeme) na kulikuwa na mzee wa makamo ambaye walimuita The King of Keys (huyu ni mtaalamu wa kufungua vitasa na makufuli ya aina zote pamoja na kufoji funguo)..
Yule myahudi aliwaambia kazi ya ile replica ni wao wafanye mazoezi na kuitafiti na hatimae wajue namna gani wataweza kuingia ndani ya vault ya Antwerp pasipo kugundulika..

Iliwachukua miezi mitano Natarbartolo na wenzake kufanya mazoezi na kutengeneza perfect plan itakayowawezesha kuingia katika vault na kuiba pasipo kugundulika..


SIKU YA TUKIO..

Siku moja kabla ya tukio, yaani February 14 2003 Notarbartolo alienda mchana kwenye vault kana kwamba kuna almasi ameenda kuhifadhi lakini akajitahidi akae karibu na kifaa cha kuhisi joto na mjongeo (heat/motion sensor) na kwa kutumia hair spray aliyoificha ndani ya jaketi lake akapulizia juu ya kifaa hicho hivyo kukifanya kisiwe na uwezo wa kuhisi mabadiliko yoyote ya joto au movement ndani ya vault...

Ilipowadia siku ya tukio lenyewe.. February 15
Notarbartolo na wenzake waliendesha gari mpaka karibu kabisa na jengo lenye vault! Jengo lilikuwa na ulinzi mkali kwa mbele lakini nyuma ya jengo hakukuwa na ulinzi mkubwa kwani watu wa ulinzi walikuwa na imani kubwa sana na teknolojia yao inayosaidia kulinda jengo lao..
Wote wakashuka kwenye gari isipokuwa Notarbatolo alibaki kwenye gari! Baada ya kushuka wote wakazunguka nyuma ya jengo ambako walitumia ngazi ambayo The genius alikuwa ameificha hapo mchana wake wakapanda mpaka ghorofa ya pili.. Baada ya wote kupanda katika balcony ya ghorofa ya pili ilibidi wakae mbali na madirisha kwani yote yalifungwa vifaa vya kuhisi joto na movement na vikigundua tu kuwa kuna mabadiliko ya joto au movement basi alarm inalia..
Alichokifanya The genius alichukua kitambaa kirefu kilichotengenezwa kwa polyester kujifunika na kusogolea kifaa kile cha heat and motion sensor.. Kutokana na yeye kujifunika kwa nguo yenye material ya polyester hii ilipelekea kifaa kile kushindwa kudetect kilichokuwa kinatokea na alipokifikia karibu kifaa kile akakifunika kabisa na nguo ile kwahiyo korido ikawa iko salama kwa wao wote kupita.. Wakafungua madirisha wakaingia ndani na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini kwenye vault..

Baada ya kufika chini nje ya mlango wa vault ambako kulikuwa na giza kutokana na kuzimwa taa.. Wakatumia fursa hiyo kuzifunga kamera kwa mifuko meusi na kisha wakawasha taa.. Baada ya kuwasha taa ilikuwa sasa ni jaribio la kufungua mlango na hapa ndio wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani wakikosea kitu kimoja tu maana yake alarm italia na mchezo utaishia hapo..

Itaendelea wakuu..

CREDIT TO JAMII FORUM

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us