Chadema wajipanga kuandamana nyumbani kwa JPM | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, August 01, 2016

Chadema wajipanga kuandamana nyumbani kwa JPM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake.

“Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.

“Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwaonya Chadema kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila kufuata utaratibu kwani hatawavumilia.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us