MREMBO JOKATE MWEGELO ADAIWA KUSHURIKI PATI YA MASHOGA | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, August 01, 2016

MREMBO JOKATE MWEGELO ADAIWA KUSHURIKI PATI YA MASHOGA


Tuhuma nzito! Ubuyu ulionyooka mjini unadai kwamba, mwanamitindo the big name Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ anadaiwa kushiriki kwenye pati ya wanaume wanaojihusisha na ngono ya jinsi moja almaarufu mashoga ambayo imeelezwa kuwa hufanyika kwa siri kila Jumamosi moja ya mwezi.

Habari hizo zilidai kwamba, shughuli hiyo hufanyika kwa siri kubwa kwenye jumba moja la kifahari lililopo Masaki jijini Dar. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kuna shirika moja lina mpango wa kuendeleza ushoga hapa nchini hivyo limekuwa likikutana na mashoga mbalimbali kwa kuwaandalia pati na kuwawezesha ambapo ndani ya pati hiyo kuna mambo yasiyo ya kawaida yanayofanyika. 



KISIKIE CHANZO    “Ninyi waandishi wa habari hivi mnajua kuna maovu mengi ambayo yanaendelea hapa nchini? Hivi mnajua kuwa kuna ufuska unaendelea kwenye pati zinazofanywa kila Jumamosi moja ya kila mwezi? Huko huwa wanaalikwa wanawake na wanaume lakini walengwa

wakubwa ni mashoga,” alinyetisha mtoa ubuyu wetu na kuongeza: “Wamo pia mastaa na watu maarufu kama Jokate.” Baada ya chanzo chetu kutoa ubuyu huo, Wikienda lilituma kachero wake wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambaye alijipenyeza na kuingia ndani ya pati hiyo ambapo alishuhudia mambo kibao ya aibu kwani anakuambia kuna kipindi kinaitwa kujichanganya (mixing time) ambapo inabidi wanaume wajichanganye na wanawake wakati huo ndiyo watu huutumia kufanya mambo ya kifuska ambayo hayaandikiki gazetini. MSIKIE OFM: “Dah! Ingekuwa inaruhusiwa kupiga picha, ningefanya hivyo kwani ni mambo ya kushangaza ambayo yanaendelea kule ndani kwenye jengo (jina linahifadhiwa) ambalo liko jirani na Ufukwe wa Coco (Dar) na linalindwa saa zote. “Cha kushangaza ambacho sikukitarajia ni pale nilipomuona mwanamitindo Jokate Mwegelo naye amekuja kwenye sherehe. Yeye hakuniona na wala asingenijua huenda alipoalikwa hakujua kinachoendelea lakini alikuja na alisherehekea kama kawaida na mwingine yupo ana jina

ya kuulizwa swali hilo, Jokate alikaa kimya kwa zaidi ya dakika ishirini ambapo mwandishi wetu alimtupia swali lingine akimuuliza sababu ya ukimya ni nini? Ukimya huo ulikoma baada ya saa moja ambapo alijibu akisema kuwa kuwa hapajui sehemu hiyo na wala hakwenda huko. Mwandishi aliendelea kumbana kwa maswali na kumkumbusha watu aliotajwa kuwa nao ambapo alisema kuwa, hakumbuki ni lini kisha akaongeza kuwa hayupo Dar huku akisisitiza kuwa amekuwa akinyamaza kwa sababu anasingiziwa vitu vingi. “Mimi sipo Dar, hiyo pati ilifanyika lini? Mimi sijui lolote, kwani unaongelea nini? Hata hivyo, naomba msiniandike kwa mambo hayo machafu, mimi sielewi,” alisema Jokate. TUJIKUMBUSHE Hivi karibuni kuliibuka tafrani kati ya mashoga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo baadhi walikamatwa baada ya kukutwa kwenye pati yao maeneo ya Kinondoni ndipo kukaibuka maneno kuwa kuna watu wanaotaka kumkwamisha Makonda kwa kuwafadhili watu hao kwa ajili ya kuendeleza uchafu huo ambao unapigwa vita kote nchini. NENO LA MHARIRI Gazeti hili bado linaendelea kufuatilia sherehe hizo zinazotajwa kufanyika kila Jumamosi moja ya mwezi na  kama litajiridhisha litafikisha sehemu husika lengo ikiwa ni kukemea mambo ya kishoga ambayo hayakubaliki nchini kwetu.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA


google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us