MSANII DIAMOND PLATNUMZ ATOA MSAADA WA TSH. MIL 20 KWA TAASISI YA UPASUAJI/MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, August 11, 2016

MSANII DIAMOND PLATNUMZ ATOA MSAADA WA TSH. MIL 20 KWA TAASISI YA UPASUAJI/MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA.

Msanii wa muziki Diamond Platnumz ametoa msaada wa tsh 20 Milioni kwa ‘GSM Foundation’ kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo ya kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na GSM Foundation imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.

Raisi huyo wa label ya ‘WCB’ ameonyesha kughuswa na jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangili kiasi hicho.

“Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa na watu basi nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na ndio maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,” aliandika Diamond Istagram. “Leo Mapema nilitembelea ofisi za GSM foundation kuwasilisha kidogo tulichobarikiwa kwa niaba ya WCB. kwajili ya kusaidia watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa (Bobble Head Syndrome) na Mgongo wazi,”

Kwa upande wa GSM Foundation, ameandika:Leo tumepokea hundi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz kama mchango wake kwa #GSMFoundation. Tunamshukuru kwa kuja kututembelea ofisini kwetu na kwa msaada aliotupatia. Mwenyezi Mungu amuongezee pale alipopunguza.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us