Mamelodi Sundowns yajiweka pazuri kutwaa klabu bingwa Afrika | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, October 16, 2016

Mamelodi Sundowns yajiweka pazuri kutwaa klabu bingwa Afrika

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imejiweka kwenye nafasi nzuri kuelekea mchezo mchezo wa marudiano wa fainali ya klabu bingwa Afrika Jumamosi ijayo baada ya kuifunga Zamalek 3-0 kwenye mechi ya kwanza mjini Pretoria.

Licha ya ushindi huo mnono ilioupata Sundowns, tangu mwaka 2010 ambapo TP Mazembe iliifunga Esperance ya Tunisia 5-0, bado hakuna klabu ambayo imeweza kufanya hivyo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya fainali.

Anthony Laffor na Tebogo Langerman walifunga magoli mawili ya kuongoza kipindi cha kwanza huku bao la tatu likifungwa kipindi cha pili.

Ushindi huo unaifanya Sundowns kupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano mjini Alexandria ambako watakuwa wakisaka taji lao la kwanza barani Afrika na kuwa timu ya pili kutoka Afrika Kusini kushinda taji hilo kubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Wakitazamwa na watazamaji 40,000 Sundowns walikuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwa kuichezesha Zamalek katika mchana wa jua kali.

Endapo Sundowns watatwaa taji mwishoni mwa juma lijalo, wataandika historia mpya kwenye ardhi ya Afrika Kusini kwa ngazi ya vilabu. Walitupwa nje mapema wakati wa hatua za kufuzu dhidi ya AS Vita Club lakini walirejeshwa tena mashindanoni baada ya Vita Club kupokwa nafasi hiyo kufatia kumchezesha mchezaji asiye na vigezo.

Mchezo wa marudiano utapigwa Alexandria Jumapili October 23.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us