Anna kilango Malechela: Rais Magufuli Anaujua Utendaji Wangu ndio Maana Amenipa Nafasi ya Ukuu wa Mkoa | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, March 14, 2016

Anna kilango Malechela: Rais Magufuli Anaujua Utendaji Wangu ndio Maana Amenipa Nafasi ya Ukuu wa Mkoa

Image result for ANNE KILANGO
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Same Mashariki ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mteule wa Shinyanga, Anna Kilango Malechela, amesema jitihada zake na utendaji katika kuihudumia jamii ndio sababu kuu iliyomfanya Rais Magufuli  kumpa nafasi ya kuuongoza mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Sun Rise cha Times Fm, Malechela amedai hata ‘anguko’ lake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, aliangushwa na watu wenye sababu binafsi na si kukataliwa na Wananchi.

“Mungu ni mwema, sikuwa na hili wala lile, nimekaa Bungeni miaka 15 na Mh Rais akiwa kama Mbunge, kwahiyo alikuwa anaona utendaji wangu, kupambana na kero za wananchi na jinsi nilivyo na jitihada.

“Unajua wanaosema tunabebwa tulianguka kwenye uchaguzi, watazame kwa  upana zaidi, wengine tuliangushwa, naahidi kutumia kauli mbiu ya kazi tu kuitumikia Shinyanga” Alisema Mama Anna Kilango.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us