Rais Magufuli athibitisha watendaji TRA, Takukuru | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, March 14, 2016

Rais Magufuli athibitisha watendaji TRA, Takukuru


RAIS John Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali; ambazo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Waliothibitishwa ni Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA ambaye anakuwa Kamishna Mkuu wa taasisi hiyo.
Pia Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, amethibitishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini. Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema watendaji hao walioteuliwa hivi karibuni wamethibitishwa kuanzia jana.
Watendaji hao waliteuliwa kukaimu nafasi hizo Desemba mwaka jana baada ya Rais kutengua uteuzi wa waliokuwa wakishika nafasi hizo. Kidata alikaimu nafasi hiyo baada ya uteuzi wa Harry Kitilya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, kutenguliwa. Naye Mlowola aliteuliwa kukaimu, baada ya rais kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru aliyekuwapo Dk Edward Hosea.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us