Azam FC ipo tayari kwa mapambano Caf | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, March 13, 2016

Azam FC ipo tayari kwa mapambano Caf


azam fc 
Kikosi cha timu ya Azam Sc.
 Johannesburg
AZAM FC leo Jumamosi inacheza na Bidvest Wits katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika huku Kocha Stewart Hall akitamba timu yake kupata ushindi kutokana na maandalizi waliyofanya.

Akizungumza jijini Johannesburg, Hall, raia wa Uingereza, alisema wataingia uwanjani wakiwa tayari wanawajua wapinzani wao kwani awali walipata vielelezo mbalimbali vya Bidvest.

Hall alisema jana Ijumaa asubuhi walifanya kikao cha mwisho na wachezaji wote na benchi la ufundi kutazama baadhi za video za wapinzani ili kuwajua wachezaji wenye madhara kabla ya kucheza nao.
Aliongeza kuwa, tangu wamefika huko, wanakabiliana na changamoto ya baridi na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, hivyo wamechukua tahadhari za kutosha kukabiliana na hali hiyo ili kupata ushindi huo.
“Mechi siyo nyepesi kwetu dhidi ya Bidvest tutakayoicheza kesho (leo), kama unavyojua mechi za ugenini zinakuwa na mambo mengi, pia wenzetu watakuwa na sapoti ya mashabiki.
“Lakini kwa upande wa ufundi, maandalizi tuliyofanya ya kikosi chetu yanatosha kupata ushindi katika mechi hii,” alisema Hall.
Kwa upande wake nahodha wa Azam, John Bocco, alisema: “Tuna morali kubwa kuelekea mechi hii na Bidvest Wits, naamini tutafanya vizuri licha ya changamoto ya baridi.”
Mchezo huo wa raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho utachezwa kwenye Uwanja wa Bidvest unaomilikiwa na timu hiyo, uliopo Johannesburg. Timu hizo zitarudiana Machi 20, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us