Jason, Daphne wajiachia ufukweni | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, March 13, 2016

Jason, Daphne wajiachia ufukweni



3209B77600000578-3484448-image-a-20_1457548505194Staa wa muziki wa R&B, Jason Derulo na mpenzi wake, Daphne Joy wakiwa ufukweni.
CASA ARAMARA, Mexico
ANAPIGA kote kote! Staa wa muziki wa R&B, Jason Derulo na mpenzi wake, Daphne Joy wameonyesha kuwa wanapendana sana baada ya kuonekana wakijiachia vya kutosha huko Punta Mita, Mexico, Jumanne ya wiki hii.

Jason Derulo ambaye amewahi kutoka na msanii mwenzake, Jordin Spark aliyedumu naye kwa miaka mitatu, sasa ameangukia kwenye penzi la mrembo Daphne Joy ambaye ni ‘ex’ wa staa wa hip hop, 50 Cent aliyezaa naye mtoto mmoja, Sire Jackson, 3.




jason


Wakifurahia jambo.
Staa huyo mwenye miaka 26 ambaye kwa sasa anatisha na Ngoma ya Hello Friday na mpenzi wake huyo aliyenaye kwa miezi minne sasa walipata nafasi ya kujiachia vilivyo kwenye Fukwe za Casa Aramara huku wakionyesha mapenzi ya hadharani na watu kuwashangaa.
Wakiwa huko walicheza michezo mbalimbali kama kukimbizana, kumwagiana maji, kuendesha pikipiki zinazojulikana kama ATV pamoja na mingine mingi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us