Ferguson aipa nafasi Leicester City | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, April 01, 2016

Ferguson aipa nafasi Leicester City

Getty
Meneja wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson anaamini Leicester City wanastahili
kutawazwa mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Leicester wamekuwa na msimu mzuri 2015-2016 wakiwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano huku wakiwa wamebaki na mechi saba.
Msimu uliopita wote ulikuwa wa wasiwasi kwa Leicester kwani walikuwa wakipigania kutoshuka daraja lakini hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu.
Hata hivyo, kutokana na hali na moyo wa kujituma walio onyesha chini ya Claudio Ranieri msimu huu, Ferguson anadhani hakuna timu inayostahili kushinda taji la ligi zaidi ya Leicester.
Ferguson ambaye alinyakuwa mataji 13 ya ligi akiwa na United amesema kwa uwezo mkubwa walioonyesha Leicester hana shaka kuwa wanastahili kushinda taji hilo.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us