Muda kuzima simu feki hautaongezwa | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, April 01, 2016

Muda kuzima simu feki hautaongezwa




SERIKALI imesema haitaongeza muda wa kuzima simu feki, baada ya
Juni 17 iliyotangaza awali. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alitoa msimamo huo wakati akijibu risala ya Mkuu wa Wilaya Kibondo, Ruth Msafiri aliyetaka Serikali isimamishe mpango huo kwa kuwa utaathiri Watanzania wengi masikini.
Waziri Mbarawa alisema, ni muhimu kuzima simu feki zote ili kupunguza tatizo la wizi kwa kutumia mitandao ya simu inayofanywa zaidi za simu za aina hiyo.
Alisema, matukio mengi ya kihalifu yamekuwa yakitokea kwa kutumia simu hizo akitolea mfano wa tukio la West gate lililofanyika nchini Kenya, sambamba na utapeli unaofanywa kwa viongozi na watu wenye fedha nchini na kwamba mawasiliano kupitia simu hizo yanapotafutwa kwenye mitandao huwa hayapatikani.
“Faida ya kuzima simu feki ni kubwa kuliko kuacha matumizi ya simu hizo yakiendelea na tafiti zinaonesha kuwa watu milioni 1.2 ndio watakaoathiriwa na hatua hiyo,” alisema Profesa Mbarawa.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us