Q-Chillah kufanya bonge la kolabo na Diamond platnumz hivi karibuni | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 13, 2016

Q-Chillah kufanya bonge la kolabo na Diamond platnumz hivi karibuni



Q-Chief amedai kuwa anataka kufanya wimbo mkubwa na Diamond.

Ameiambia blog hii kuwa mazungumzo kwaajili ya kufanyika wimbo huo yapo sehemu nzuri.

“Diamond ana management yake, na he is big to his own way that huwezi tu kukurupuka ukasema tunafanya kazi,” anasema.
“Licha ya kwamba mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao anawaadmire sana na mimi ni mmoja kati ya mashabiki wake, napenda kazi zake hasa this latest ambayo amefanya na AKA naona improvement na changes, mimi napenda mtu ambaye anabadilika ambaye habaki pale pale, napenda mtu ambaye anafunguka zaidi,” ameongeza.
“Nikimtumia message anarespond vizuri sana, kitu ambacho ananipa moyo zaidi. Lakini mimi na Diamond hatutakiwi kufanya kazi nyepesi, tunatakiwa kufanya kazi kubwa, kazi yenye uzito, kazi yenye ubora, kazi yenye kumbukumbu, kazi ambayo itaishi, itaingiza pesa na itamtoa Q-Chief kutoka hatua moja kumpeleka hatua nyingine. Kwahiyo tusubirie kwasababu nataka kuandika kitu kizuri.”

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us