Rais Magufuli: Shinyanga Ina Watumishi Hewa 226. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 20, 2016

Rais Magufuli: Shinyanga Ina Watumishi Hewa 226.

BOFYA  KUPATA APP YA TANZANIAMPYASASA..BOFYA HAPA

Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.
 
"Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge” ,amesema Rais Magufuli.

Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja ,jambo lililosababisha rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi hewa 45 katika awamu ya kwanza.

Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Rais alitangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake. 

Je, una tangazo,habari,picha,makala,Maoni na ushauri wasiliana nasi kupitia,Simu namba 0716528779/0755542721
na Email.titoemmanuel93@gmail.com 

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us