Wanufaika mishahara hewa waanza kubanwa | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, April 16, 2016

Wanufaika mishahara hewa waanza kubanwa

http://habarileo.co.tz/images/resized/images/frequent/angela-kairuki_210_120.jpgWaziri wa nchi ofisi ya Rais (utawala bora) Bi.Angela Kairuki

SAKATA la mishahara hewa iliyokuwa ikiigharimu Serikali zaidi ya Sh bilioni 1.8 kila mwaka, limechukua sura mpya baada ya mishahara hiyo kubainika kuwepo karibu katika kila kona ya nchi.



Mbali na kusababisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango kusimamishwa kazi kabla hata ya kumaliza mwezi tangu aanze kutumikia cheo hicho, sasa watumishi walionufaika na mishahara hiyo wameanza kushikwa na kufikishwa mahakamani.

Jana, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Abdul, maarufu kwa jina la Nyamangaro (44), alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, akikabiliwa na makosa ya wizi wa mishahara ya watumishi hewa inayofikia Sh milioni 29.4.
Mishahara ya 2013

Wakili wa Serikali, Michael Ng’hoboko alidai mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya Aprili 29, 2013 na Machi 27, 2014, mshitakiwa aliiba Sh milioni 29.4 huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa mshitakiwa alikuwa akijipatia mishahara hiyo ambayo wahusika walishastaafu kazi muda mrefu kupitia akaunti yake namba 50802503513, iliyoko Benki ya NMB, tawi la mjini Singida.

Hata hivyo, mshitakiwa alikana kutenda makosa hayo na kesi yake imeahirishwa hadi Aprili 27 mwaka huu itakapotajwa tena. Mshitakiwa alitakiwa kutoa Sh milioni 14.7 taslimu ya dhamana mahakamani au awe na mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha fedha. Taarifa zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni zinaonesha kwamba mshitakiwa hakufanikiwa kupata fedha hizo na kurudishwa rumande.

Idadi yao
Uhakiki uliofanywa na serikali kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa nchini, mpaka sasa umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa mabilioni hayo ya fedha. Uhakiki unaendelea na wafanyakazi hewa zaidi wanaendelea kugunduliwa.

Kutokana na changamoto hiyo, Machi 15 mwaka huu wakati Rais John Magufuli akiwaapisha wakuu wa mikoa, alitoa siku 15 kwa viongozi hao kuhakikisha wanajumuisha wafanyakazi wote na kuwaondoa watumishi hewa.

Alipokwenda Chato mkoani Geita, Rais Magufuli alitolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17 na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.

Rais Magufuli pia alisema Serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us