Bunge Laahirishwa Baada ya Wabunge wa Upinzani Kumgomea Naibu Spika Kwa Kukataa Hoja ya Wanafunzi 7000 Waliofukuzwa UDOM | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, May 30, 2016

Bunge Laahirishwa Baada ya Wabunge wa Upinzani Kumgomea Naibu Spika Kwa Kukataa Hoja ya Wanafunzi 7000 Waliofukuzwa UDOM


Naibu Spika wa Bunge ameahirisha Bunge kabla ya muda wake baada ya wabunge kutaka kujadiliwa suala la wanafunzi wa Udom kufukuzwa chuoni wakati hawana kosa.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliomba mwongozo na kutaka sakata la wanafunzi hao lijadiliwe lakini Naibu Spika, Tulia Ackson alisema jambo hilo haliwezi kusitisha shughuli za Bunge hivyo haliwezi kujadiliwa kwa wakati huo.

Kauli hiyo iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa Bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us