CAF: Chad yajiondoa Taifa stars mashakani. | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, March 27, 2016

CAF: Chad yajiondoa Taifa stars mashakani.

: Chad yajiondoa mashindanoni na kuicha Tanzania Taifa Stars mashakani
Chad imejiondoa kutoka kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani huko Gabon.
Shirikisho la soka la Chad limefikia kauli hiyo kutokana na ukosefu wa fedha.

Katika barua iliyotumwa kwa shirikisho la soka la Tanzania,mwenyekiti wa shirikisho la soka la Chad Moctar Mahamoud, alisema kuwa hawana fedha za kutosha kufadhili safari ya kwenda Dar Salaam kwa mechi ya marudiano dhidi ya Taifa Stars hapo kesho.
CAF imewapiga marufuku Chad kutoka kwenye mashindano ya mwaka wa 2019 mbali na kuitoza faini ya dola $20,000 pesa za Marekani.
 
Tanzania iliyokuwa imeratibiwa kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Chad kesho sasa imesalia napointi 1.
Kufuati kujiondoa kwa Chad sasa matokeo ya mechi zote dhidi ya Chad zimefutiliwa mbali na shirikisho la soka la Afrika CAF.
Chad ilikuwa inaburuta mkia katika kundi G.
Tanzania iliyokuwa imeratibiwa kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Chad kesho sasa imesalia na pointi 1.
Misri iliyokuwa imeizaba Chad 5-1 sasa ndio wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 4.
 
Mwenyekiti wa shirikisho la soka la Chad Moctar Mahamoud, alisema kuwa hawana fedha za kutosha kufadhili safari ya kwenda Dar Salaam
Super Eagles ya Nigeria ambao wameratibiwa kuchuana dhidi ya Misri mjini Alexandria siku ya Jumanne sasa sharti washinde alama zote ilikumaliza katika nafasi ya kwanza.
Sheria za CAF zinasema kuwa endapo kundi litakuwa na timu 3 basi timu inayoongoza pekee ndiyo inayosonga mbele.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us