Nassari aongoza maziko ya diwani pekee wa CCM | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, March 27, 2016

Nassari aongoza maziko ya diwani pekee wa CCM

ALIYEKUWA Diwani pekee wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika halmashauri ya Meru, mkoani Arusha, Naftali Mbise jana amezikwa na umati wa watu, viongozi wa dini pamoja na vyama mbalimbali vya siasa akiwemo Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Akiongoza misa ya maziko hayo jana katika Kata ya Ngarenanyuki ambayo alikuwa akiiongoza diwani huyo, Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Tengeru, aliwasihi waumini wa dini ya Kikristo kujiweka tayari kwa maana hakuna mtu anayejua kesho itakuwaje.
Naye Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alisema anakosa neno la kuzungumza sababu diwani Mbise amekufa kifo cha ghafla mno kwani Desemba 11, 2015 waliingia kwenye mchakato wa kuweka uongozi ndani ya halmashauri ya Meru pamoja na kamati za kudumu ndani ya halmashauri.
Alisema wakati wa mchakato alimwita faragha na kumuuliza anataka awekwe kamati gani na kumjibu kuwa awekwe Kamati ya Elimu, Afya na Maji na kabla kamati haijaanza kazi diwani Naftali amefariki dunia.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Michael Lekule Laizer akitoa salamu za Chama alisema Chama kimepoteza diwani mahiri lakini hawatakata tamaa kwani maendeleo ya wananchi ni wananchi wenyewe, hivyo Chama kimepoteza mtu shujaa ambaye alikuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi wa kata yake.
Diwani huyo alifariki dunia juzi baada ya kuanguka juu ya mti, alipokuwa anapunguza matawi nyumbani kwake. Halmashauri ya Meru ina jumla ya Kata 18 ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015, CCM ilishinda kata moja tu ya Ngarenanyuki.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us