Rais MAGUFULI awataka watanzania kufanya kazi | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, March 27, 2016

Rais MAGUFULI awataka watanzania kufanya kazi



Rais JOHN MAGUFULI amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo ya nchi na kukuza uchumi wa taifa ikiwa ni sehemu ya kuondokana na umasikini nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini huku akisikilizwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
Rais MAGUFULI amesema hayo Jijini DSM katika  Ibada ya PASAKA alipopata fursa  ya kuwasalimu waumini  wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri AZANIA FRONT alipokwenda kusali pamoja na mkewe mama JANET MAGUFULI.
 Pamoja na mambo mengine Rais MAGUFULI amesema kipindi hiki cha sikukuu watanzania wanapaswa kudumisha upendo na kujenga umoja kwa taifa zima ili kufikia malengo mbalimbali ya maendeleo.
Awali akitoa mahubiri katika ibada ya  pasaka Askofu wa Kanisa la Kiinjili la kiluteri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dokta ALEX MALASUSA alisema wananchi wote wanapaswa kuwa na  hofu ya Mungu ili kuweza kushinda changamoto mbalimbali katika jamii  ikiwemo rushwa.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us