JK ashiriki mkutano wa uandishi Katiba ya Libya | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, March 21, 2016

JK ashiriki mkutano wa uandishi Katiba ya Libya

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Afrika (AU) katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalumu la Uandishi wa Katiba ya Libya unaoendelea mjini Salalah, Oman.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Martin Kobler. Katika mkutano huo, Kikwete alielezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu.
Aliwakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya, hususan hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Aliwakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kuwapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto zinazoikabili Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us