Naibu Spika apewa ulinzi mkali wa polisi | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, June 13, 2016

Naibu Spika apewa ulinzi mkali wa polisi

Naibu Spika wa bunge, Dk Tulia Ackson ameongezewa ulinzi hasa kipindi hiki ambacho wabunge wanajadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17. Tangu Serikali ilipowasilisha bajeti, idadi ya walinzi kwa ajili ya Dk. Tulia iliongezeka hadi watano idadi ambayo ni kubwa kuliko awali.

Jambo hilo limesababisha hata wabunge wa CCM na wa upinzani kushangaa huku wengine wakihoji sababu. Wapo baadhi ya wabunge waliodhani huenda ulinzi wa Dk. Tulia umeongezwa baada ya kutoa mwongozo mwishoni mwa wiki wa wabunge wa upinzani kutolipwa posho za vikao vyote walivyotoka nje.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us