Daktari aliyetuhumiwa kuchangia kifo ajifungua | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

Daktari aliyetuhumiwa kuchangia kifo ajifungua


DAKTARI wa zahanati ya Kapalamsenga mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda mkoa wa Katavi, Rehema Munga anayetuhumiwa na wakazi wa kijiji hicho kusababisha kifo cha Bibiana Kilangi (49) kwa kugoma kumhudumia, amejifungua salama.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpanda , Dk Jovin Mlinda alikiri kuwa Munga alijifungua mtoto mwenye uzito wa kilo tatu hospitalini hapo Jumapili iliyopita. Siku moja kabla ya Munga kujifungua mtoto huyo hospitalini hapo, askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka kambi ya Ikola mwambao mwa Ziwa Tanganyika walilazimika kuzingira nyumba yake ili kulinda usalama wa maisha yake na familia yake baada ya wananchi wenye hasira kutishia kuichoma moto.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda , Hamad Mapengo alidai kuwa mgonjwa huyo alifikishwa na ndugu zake katika zahanati ya Kapalamsenga saa 7:00 usiku kwa matibabu lakini daktari alikuwa tayari amelala nyumbani kwake.
Akifafanua Mapengo alieleza kuwa ndugu wa mgonjwa huyo walilazimika kumfuata daktari wa zahanati hiyo nyumbani kwake ikiwa ni umbali wa mita 20 kutoka katika zahanati hiyo lakini aligoma kuamka akidai kuwa ameshalala.
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo, aliamua kuwashauri ndugu wa mgonjwa huyo, wampeleke mgonjwa wao katika Kituo cha Afya cha Karema kilichopo umbali wa kilomita 15 kutoka kijijini hapo.
“Tulimsihi sana lakini aligoma kabisa kutoka nyumbani kwake akatutaka tumpeleke mgonjwa wetu katika Kituo cha Afya cha Karema. Tulipomfikisha katika kituo hicho cha afya alibainika kuwa na upungufu wa damu mwilini, mgonjwa wetu alikata roho saa 10:00 alfajiri. Mbaya zaidi kituoni hapo hakukuwa na akiba yoyote ya damu hivyo wakati tukipanga kumsafirisha kwenda Hospitali ya Wilaya mjini Mpanda alikata roho,” alisisitiza mtoa taarifa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mapengo, wanakijiji hao walifikia uamuzi wa kuuchukua mwili wa marehemu huyo ili wakautelekeze nyumbani kwa mganga huyo ili aufanyie maziko. “Hata hivyo viongozi wa kijiji hicho waliweza kuwataarifu askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kambi Ikola ambapo walifika nyumbani kwa daktari huyo na kuizingira. Wanakijiji hao walilazimika kutawanyika na kurejea makwao,” alisisitiza Mapengo .
Inaelezwa kuwa kutokana na sakata hilo, uongozi wa hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda walituma gari kwenda kijijini Kapalamsenga umbali wa kilomita 120 kutoka Mpanda mjini kumchukua mganga huyo.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us