Majeshi ya KENYA yaua Al shabab 19 | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

Majeshi ya KENYA yaua Al shabab 19

Majeshi ya ulinzi ya KENYA yamewaua wapiganaji 19 wa kikundi cha kigaidi cha AL SHABAAB baada ya mapigano makali katika eneo la AFMADHOW nchini SOMALIA
Majeshi ya KENYA yaua Al shabab 19
Msemaji wa jeshi la KENYA, Kanali David Obonyo amesema vikosi vya Kenya vilibaini njama za wapiganaji wa AL SHAABAB ambao walikuwa na njama za kufanya shambulio kwa vikosi vya AMISOM na kambi ya taifa ya jeshi la Somalia iliyopo AFMADHOW.

Kanali Obonyo ameongeza kuwa majeshi ya KENYA pia yameteketeza gari la magaidi hao na kukamata bunduki 10 aina ya  AK-47, silaha za masafa marefu tatu na mabomu ya kutega ardhini.

Jaribio la Al-shabaab kuvamia vikosi vya jeshi la Somalia na Kenya katika kambi ya  AFMADHOW linakuwa miezi miwili  baada ya wanamgambo hao wenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda kuvamia kambi ya jeshi la Kenya eneo la El Adde na kuwauwa takribani wanajeshi mia moja.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us