MAREKANI yaiwekea vikwazo KOREA KASKAZINI | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

MAREKANI yaiwekea vikwazo KOREA KASKAZINI



Wakati KOREA KASKAZINI, ikiwa imemfunga, miaka kumi na mitano jela pamoja na kazi ngumu, mwanafunzi mmoja raia wa MAREKANI
Wakati KOREA KASKAZINI, ikiwa imemfunga, miaka kumi na mitano jela pamoja na kazi ngumu, mwanafunzi mmoja raia wa MAREKANI, baada ya kupatikana na hatia ya kuiba bango lenye propaganda, huko KOREA KASKAZINI, MAREKANI nayo imelipiza kisasi.

MAREKANI imeiwekea vikwazo vipya KOREA YA KASKAZINI, ikiwa ni hatua ya kupinga kitendo cha nchi hiyo kumfunga raia wake huyo, ambaye alikwenda KOREA YA KASKAZINI, na kundi la wanafunzi wenzake kwa ajili ya masomo ya kujifunza kwa kutalii.

Mwanafunzi huyo alilazimishwa kuomba radhi hadharani, mbele ya waandishi wa habari. MAREKANI imesema, kitendo kilichofanywa na KOREA KASKAZINI hakiwezu kukubalika na nchi yoyote, kwani kosa alilofanya mwanafunzi huyo, halistahili adhabu kali aliyopewa.

Vikwazo vya sasa vya MAREKANI dhidi ya KOREA KASKAZINI vinawahusu viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us