OLE SENDEKA Msemaji mpya wa CCM | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, March 20, 2016

OLE SENDEKA Msemaji mpya wa CCM



Chama cha mapinduzi CCM kimemteua Mbunge wa Zamani wa SIMANJIRO mkoani Manyara, CHRISTOPHER OLE SENDEKA kuwa msemaji wa chama hicho
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Akitangaza hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jijini DSM katibu mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA amesema uteuzi wa OLE SENDEKA kwa msemaji wa chama hicho, ni hatua ya kupunguza majukumu ya kiutendaji kwa aliyekuwa msemaji wa chama hicho NAPE NNAUYE aliyeteuliwa kuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Kanana amesema hatua hiyo itatoa fursa kwa watendaji hao kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi  katika kuwatumikia wananchi.
Akizungumza mara baada ya uteuzi huo,msemaji huyo wa CCM CHRISTOPHER OLE SENDEKA ametoa wito kwa wanasiasa nchini kuacha siasa za  kuponda jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kutimiza majukumu yake, ambapo amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us