Ofisa Mifugo chupu chupu atumbuliwe jipu Misenyi | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 15, 2016

Ofisa Mifugo chupu chupu atumbuliwe jipu Misenyi


OFISA Mifugo wa Kata ya Kakunyu wilayani Misenyi mkoani Kagera, Eric Kagoro amenusurika kutumbuliwa jipu kwenye mkutano wa hadhara baada ya kuhusishwa na sakata la kuruhusu ng’ombe 291 kulisha kwenye Ranchi ya Mifugo ya Misenyi.

Tukio hilo ni la jana wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mamia ya wananchi waishio jirani na ranchi hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye makao makuu ya ranchi hiyo.
Waziri Mkuu alimuibua Kagoro katikati ya mkutano kwa kumtaja jina na tuhuma zinazomhusu kuhusu mifugo iliyokamatwa. “Ofisa Mifugo wa kata yupo hapa?,” alihoji Waziri Mkuu na kuendelea kumhoji, “Wewe ndiyo Eric?”
Alipojibu Ndiyo, Majaliwa alimuuliza tena, “Nimekujuaje?” “Nimeambiwa wale ng’ombe waliokamatwa ni wa rafiki yako na wewe ndiye ulitoa kibali waje kulishwa kwenye ranchi hii. Siyo kazi yako kuruhusu mifugo ya nje ije kulishwa hapa kwenye ranchi.
Kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza mifugo kwenye ranchi ili ipate malisho, “ alisema. “Leo nimekusamehe. Kazi yako ni kuhakikisha mifugo ya kwenye kata hiiiko salama. Kazi yako ni kuwasaidia wafugaji wa kata hii wafuge vizuri na uhakikishe mifugo yao inakuwa na tija,” alisema Waziri Mkuu hukuakishangiliwa na wananchi.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaasa watendaji wa kata na vijiji kutotumia nafasi zao kuleta migogoro baina ya watu wa nje na wananchi wanaowaongoza. “Mwenyekiti wa kijiji huna ruhusa ya kugawa kitalu cha ranchi au kuruhusu mtu yeyote akalime ndani ya ranchi”, alisema.
Aliwataka pia maofisa uhamiaji wawe makini na vyeti vya kuandikisha uraia wanavyovitoa kwa wananchi wanaoishi mipakani kwa kile alichosema, imekuwa ni mianya ya kuleta migogoro ya ardhi. “Watu wa uhamiaji kuweni makini na CN mnazotoa (CN=Certificate of Naturalisation). Wote wanaoomba CN wanataka blocks (vitalu) tu.”
Alitoa agizo kuwa watafutwe watu wote walioingia nchini kwa mgongo wa CN, wakamatwe na kurejeshwa makwao. “Kuna watu wamekuja hapa nchini wakaomba CN lakini wakikaa wanaleta wenzao waje kununua ardhi kwa kutumia mgongo wa CN zao.”
Alisema watu wametoka Wilaya ya Karagwe ambako pia kuna tatizo kama la Misenyi na kuwataka wahusika wajiandae kuchujwa na kuchukuliwa ardhi zao kama watakuwa hawajaziendeleza ili wapewe Watanzania wenye uhitaji wa kulima na kufuga.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us