Friday, December 09, 2016
Thursday, October 27, 2016
BREAKING NEWS: HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA(7) 2016
Kutokana na ukweli kwamba si kila mtu mwenye acces na mtandao na itambidi kwenda internet cafe kuangalia,KINGAZITZ BLOG tumekurahisishia mambo.
Endapo utahitaji huduma ya kuangaliziwa jina la mwanao au ndugu yako fanya yafuatayo;
1.Tuma jina la mwanao,mkoa,wilaya na shule aliyosoma
(mfano:juma paul-PWANI,KIBAHA,UHURU PRIMARY)
kwenda namba 0716528779
2.Huduma hii uatozwa tshs 1000 tu.(kwa ajili ya kuisuport kingazitz blog)
3.Tuma pesa kwenda namba 0755542721-MPESA
0716528779-TIGO PESA
5.Utajibiwa ndani ya dk.moja tu,tuma pesa kwanza ndio ujibiwe
BREAKING NEWS:HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA(7)2016
Kutokana na ukweli kwamba si kila mtu mwenye acces na mtandao na itambidi kwenda internet cafe kuangalia,KINGAZITZ BLOG tumekurahisishia mambo.
Endapo utahitaji huduma ya kuangaliziwa jina la mwanao au ndugu yako fanya yafuatayo;
1.Tuma jina la mwanao,mkoa,wilaya na shule aliyosoma
(mfano:juma paul-PWANI,KIBAHA,UHURU PRIMARY)
kwenda namba 0716528779
2.Huduma hii uatozwa tshs 1000 tu.(kwa ajili ya kuisuport kingazitz blog)
3.Tuma pesa kwenda namba 0755542721-MPESA
0716528779-TIGO PESA
5.Utajibiwa ndani ya dk.moja tu,tuma pesa kwanza ndio ujibiwe
Tuesday, October 18, 2016
PICHA 8: Wasichana 21 waliokuwa wametekwa na Boko Haram walivyokutana na familia zao.
Aprili 2014 zaidi ya wasichana 270 walitekwa wakiwa shuleni katika mji wa Chibok na wapiganaji wa Boko Haram, mpaka leo ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana hao, Alhamisi ya October 13, 2016 ziliripotiwa taarifa za kuachiwa kwa baadhi ya wasichana hao na kurejeshwa baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa serikali ya Nigeria na viongozi wa Boko Haram.
Leo October 17 2016 Wasichana 21 wa Chibok hatimaye wamekutana na familia zao
Jambazi Awajeruhi Kwa Bomu Askari na Raia Wanne Kigoma
Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji hicho. Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.
Alisema askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza Madukani alikokwenda kununua mahitaji.
Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa asiuawe kwa kipigo.
Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera, ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa ardhini.
Pia, walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne (risasi 30 kila moja) na mbili (risasi 20 kila moja) na risasi 75 zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa.
Mtui alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia juzi akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni). Alisema majeruhi wote watano walipata matibabu hospitalini hapo na waliruhusiwa kurudi nyumbani.
Monday, October 17, 2016
Watumishi TBS na TRA Waliohusika n a Upotevu wa Makontena 100 Bandarini Watakiwa Kujisalimisha Haraka kabla Hawatumbuliwa
Serikali imewataka baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) walioshirikiana na wenzao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitisha makontena zaidi ya 100 bila kukaguliwa na shirika hilo katika Bandari ya Dar es Salaam kujisalimisha haraka.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alitoa agizo hilo jana wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa TBS.
“Nimeanza kukusanya orodha ya majina ya watu waliosaidia kupitisha makontena haya na nikija nayo hawatapona,”alisema.
Aliwataka wote wanaojijua kuhusika kujisalimisha mapema na kutubu ili wasamehewe kabla ya hatua hiyo.
Makontena hayo yalipitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni bila ya kuthibitishwa na TBS.
Pia, aliitaka TRA kuacha kutoa makontena bila ya shirika hilo kuthibitisha au kukagua ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa sababu ndilo lenye mamlaka hayo.
Alisema watakaotubu watapaswa kusema walishiriki vipi na lini, walishirikiana na nani na kutaja sehemu yalikopelekwa ili Serikali iweze kusaidia kukomesha hali hiyo.
Mwijage alisema anaamini waliofanya hivyo katika mamlaka hiyo walifanya kwa utashi wao bila ya ushiriki wa viongozi wao na kwamba sasa wakati umefika wa kukomesha tabia hiyo.
Alilitaka baraza hilo jipya la wafanyakazi kushirikiana na menejimenti kuhakikisha matatizo yanayojitokeza yanapatiwa ufumbuzi kwa masilahi ya nchi na kwamba Serikali itahakikisha inaongeza vitendea kazi na watumishi ili kufikia malengo ya shirika.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Egid Mubofu alisema baraza hilo lina wajumbe 48 wanaotoka katika vitengo mbalimbali na litakaa kwa muda wa miaka mitano.
“Baraza hili linaundwa kutokana na mkataba wa menejimenti na Chama cha Wafanyakazi (Raawu),” alisema Dk Mubofu.
Alisema wafanyakazi wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu katika majukumu yao ya kila siku.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TBS, Profesa Mekanya Maboko alilitaka baraza hilo kufanya kazi kwa kushirikiana na menejimenti na bodi kuhakikisha shughuli za udhibiti wa ubora zinafanyika kwa ufanisi.
“Bodi itaendelea kuisimamia menejimenti na kuishauri ifanye kazi kwa kuzingatia sera na sheria,” alisema.