Burudani ya muziki ukumbini hapo ilifunguliwa na Mashauzi Classic, chini ya Isha Mashauzi, ambao waliachia vibao vyao vipya na vinavyoendelea kutamba na kuwanogesha mashabiki.
Sunday, June 05, 2016
Ni balaa Hebu cheki Show Ya SNURA alivyokinukisha Dar
Burudani ya muziki ukumbini hapo ilifunguliwa na Mashauzi Classic, chini ya Isha Mashauzi, ambao waliachia vibao vyao vipya na vinavyoendelea kutamba na kuwanogesha mashabiki.
RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KATIKA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO (Mzee wa upako)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabarainayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo‘mzee wa upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada yakuhudhuria ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini wa kanisa hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa
la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)
Watumishi 11 wa serikali Watumbuliwa kwa kuwa na Vyeti Feki Vya Kidato cha Nne.mkoani Mbeya.
Amesema waliwakilisha vyeti vingi NECTA na hivyo 11 ndio vikabainika vilikuwa vya kughushi ambao karibia wote ni wanawake Tazama Hapa:
Maaajabu!!!!! MTOTO AZALIWA AKIWA NA MIGUU NA MIKONO MINNE...AITWA MUNGU MVULANA!
Imetokea nchini India baada ya mama mmoja kujifungua mtoto mwenye miguu minne na mikono minne huku akipokelewa na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa ‘Mungu Mvulana’
Mtoto huyo amepewa jina la ‘Mungu Mvulana‘ kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo si jambo la kawaida na huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa jamii za kihindu na watu walisafiri kutoka kona mbalimbali za nchi hiyo kwenda kumshuhudia mtoto huyo wa maajabu.Katika mji wa Kaskazini
mwa nchi hiyo watu walijazana nje ya eneo la Hospitali hiyo wakiwa na hamu ya kutaka kumwona mtoto ambaye ana maana kubwa kwa jamii za nchini humo na wenyeji wa huko wana amini ataleta baraka katika jamii zao.
Mamia ya watu walikua wamejaza nje ya Hospitali hiyo wakiimba na kusali lakini hawakuweza kufanikiwa kumwona kutokana na wingi wao huku Polisi wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia.
magazeti ya tanzania yalivyoandika leo jumapili Juni 5 kwenye habari za kitaifa kimataifa, michezo na udaku.
Waliotimuliwa UDOM Waibuka, Watishia Kuishitaki Serikali
Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.
Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.
“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.
“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.
“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”
Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.
Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.
“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakamani,” alisema Lusako.
Udom yazungumza
Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.
“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.
Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.
“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.
HII NDIO HISTORIA FUPI YA ZARI THE BOSS LADY
“Habari mpya ni kwamba Diamond Platnumz atakuwa mgeni rasmi katika pati ya Zari All White Ciroc, najihisi niko sahihi kwa sababu sioni kama kuna ushindani wowote, huyu ni mtu wangu na itabaki kuwa hivyo,”
Licha ya kumzidi miaka 10, Zari atangaza rasmi kuwa ni mtu wake wa karibu kwa sasa.
Johannesburg/Dar. Baada ya kuukimbia ukweli kwa kipindi cha mwezi mmoja, mwanamuziki Diamond Platnumz amethibitisha kuwa na uhusiano baina yake na staa maarufu kutoka Uganda, Zari ‘The Boss Lady’ na kwamba atakuwa mgeni rasmi katika hafla yake ijulikanayo ‘Zari All White Ciroc’ itakayofanyika mwezihuu.
Nyota huyo aliyevunja rekodi kwa kunyakua tuzo tatu za Channel O Music Video Awards (ChoMVA) wikiendi iliyopita, amekuwa akijadiliwa katika mitandao ya Tanzania na nje ya nchi kwa kuonekana na wanawake tofauti kila wakati, hali inayowachanganya mashabiki wake. Hata hivyo, Diamond hajasita kuelezea hisia zake za sasa na kwamba yupo tayari kuhudhuria hafla hiyo, inayotarajiwa kufanyika Desemba 18. “Nitakuwapo katika hafla hiyo, ni lazima nimuunge mkono, mbona kuna wengi wanaunga mkono na watu hawasemi, kama wanavyokaa kimya kwa wengine nahuku iwe vivyo hivyo,” alisema Diamond huku akishindwa kukiri moja kwa moja kwamba ana uhusiano na Zari, “waswahili wanasema A na B yote majibu.”>>>
Walimu 5 Waishi Darasani Kwa Miaka Mitatu
FAMILIA tano za walimu wa shule ya sekondari Shishani Kata ya Migato Halmashauri ya Itilima Mkoani Simiyu, zinaishi jengo la utawala tangu mwaka 2013.
Hali hiyo inatokana na ukosefu wa nyumba za walimu ambapo sasa shughuli za utawala shuleni hapo zinafanyika chini ya mti.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Tito Kwilasa alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kikao cha maendeleo ya kata kilichojadili changamoto mbalimbali zilizopo.
Kwilasa alibainisha kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 160, iliyoanzishwa mwaka 2007 ina uhaba mkubwa wa nyumba za walimu.
Nyumba za walimu zilizopo shuleni hapo ni mbili wakati kuna walimu 15 walioajiriwa, ambapo wanawake ni watatu na wanaume 12. Kwa sasa walimu hao wanaishi jengo la utawala, ambapo shule ina madarasa manne na maabara iliyofikia usawa wa madirisha.
‘’Kipindi cha mvua za masika inabidi kutoa darasa moja likachanganywe na lingine ili walimu tukakae darasani na kufanya shughuli za utawala huku wanafunzi hao wakikosa masomo,”alisema.
Alisema kuwa kipindi cha nyuma walimu walikuwa wachache, hivyo walibanana katika nyumba hizo mbili. Mwaka 2013 walimu waliongezeka, hivyo waligeuza jengo la utawala kuwa nyumba ya kuishi. Mwalimu mmoja alisema ni kero kubwa kwa familia hizo kuishi jengo la utawala ambalo pia halina vyoo.
Diwani wa Kata hiyo, Mbuga Ntobi alieleza kuwa watahakikisha walimu wanajengewa nyumba ili waishi katika mazingira ya ufundishaji.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima, Kelisa Wambura alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo. Alisema halmashauri imepanga kwenye bajeti ya 2016/17 kupunguza uhaba wa nyumba za walimu, hasa shule ya sekondari Shishani.