Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Uingereza
klabu ya Leicester City, leo May 7 2016 baada ya mchezo dhidi ya Everton
katika uwanja wao wa King Power walipokea Kombe lao la kwanza la Ligi
Kuu Uingereza baada ya wiki iliyopita Chelsea kuwa kutoa sare ya 2-2 na
Tottenham Hotspurs, hivyo Leicester ikatwaa taji hilo moja kwa moja.
Hili ndio Kombe la kwanza kwa klabu ya
Leicester City iliyoanzishwa miaka 132 iliyopita, lakini hili ndio taji
la kwanza la Ligi Kuu kwa kocha wao Claudio Ranieri ambaye amewahi
kuvifundisha vilabu ya Napoli, Inter Milan, Chelsea, Atletico Madrid na
Juventus bila kuvipa taji la Ligi Kuu.
Leicester City wamekabidhiwa taji lao
baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Everton, uliyomalizika kwa
Leicester City kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ya Leicester City
yalifungwa na Jamie Vardy dakika ya 5 na 65 kwa
mkwaju wa penati na Andy King dakika ya 33, goli pekee la Everton
lilifungwa na Kevin Mirallas dakika ya 88.