
Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Kinondoni limeendelea kuwakamata wananchi wanaotumia umeme wa wizi kujiunganishia umeme kinyume cha sheria pamoja na kuwekewa mita za Luku na Vishoka ambao siyo watumishi wa Shirika hilo.
Katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam, Mfanyabiashara wa Chakula Mariam Mjema amejikuta matatani baada ya kubainika kuwa mita ya Luku aliyowekewa ilikuwa ya wizi na haina kumbukumbu...