KINGAZI BLOG: 04/25/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, April 25, 2016

Wiki nne zilizopita Diamond Platnumz alikuwa na Papa Wemba Studio


Asubuhi ya Jumapili April 24 2016 headlines za taarifa za kifo cha mwimbaji Mkongwe kutoka Congo DRC Papa Wemba aliripotiwa amefariki baada ya kuanguka jukwaani akiwa anatumbuiza huko Ivory Coast.
Sasa leo April 25 2016 Diamond Platnumz anaingia kwenye list ya wasanii walioguswa na msiba huo ambapo kupitia kwenye mtandao wake wa  instagram alipost video akiwa na Marehemu Papa Wemba wakitayarisha wimbo wao mpya ambao ulirekodiwa kipindi Diamond yuko Ufaransa kwenye ziara yake iliyopewa jina la From Tandale to the World. DIAMOND aliandika haya hapa instagram

Jus four weeks ago we were in Paris, featured me in his song and we planned alot for the song and Suddenly got the news….dah! still don’t want to believe that you are really Gone Legend….We will always miss you 🙏… #RipPapaWemba (Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, Akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halaf ghafla naskia habari ya Msiba…Dah! nimesikitika sana, Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndio Mpangaji…Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka🙏 #RipPapaWemba )

Picha: Diamond na P-Square washoot video SA


P-Square walitawala vichwa vya habari kwenye redio, TV, magazeti na blogs za Afrika kwa kuingia kwenye vita vikubwa vya maneno kati yao kiasi cha kundi kudaiwa kuvunjika.
12940912_1799083410377084_825748254_n

HIZI HAPA NAFASI MASOMO KATIKA VYUO VYA MAFUNZO YA AFYA TANZANIA

 

Hii Hapa Taarifa ya Utekelezaji Ya Kamati Ndogo ya PAC Kuhusu Mkataba wa Lugumi

Hii ndiyo Taarifa ya utekelezaji wa kamati ndogo ya PAC kuhusu mkataba wa lugumi.Kama ilivyowasilishwa bungeni  soma hapa.

Hili Hapa Tamko La Jukwaa La Wahariri Tanzania Juu Ya Matangazo Ya Bunge





Bodi ya Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyokaa Ijumaa Aprili 22, 2016 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine ilijadili hali ya mwenendo wa tasnia ya habari nchini hasa juu ya haki ya wananchi kupata habari.


Katika kujadili hali hiyo, TEF imeguswa kwa namba ya kipekee kabisa na mwenendo mzima wa urushaji wa bahari za Bunge kwa njia ya redio na luninga, hususan katika mkutano wa tatu wa Bunge la 11 unaoendelea mjini Dodoma kwa sasa.


Itakumbukwa kwamba Muhimili wa Bunge kupitia Kitengo chake cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Aprili 15 2016 ulitoa taarifa kwa umma ikieleza utaratibu mpya ambao sasa umeanza kutumika katika kurusha matangazo ya redio na luninga kutoka Bungeni.


Katika taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge ilisema kuwa imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea sasa.


Ofisi hiyo ilisema kuwa mfumo huo mpya ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio zake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao. Kwa maana hiyo, Bunge lilisisitiza kuwa chini ya utaratibu huo mpya, jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.


Katika kutekeleza uamuzi huo na mfumo huo mpya, kila kituo cha Televisheni na Redio sasa watatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa maalum ambayo pia yaliwekwa wazi.


Kwa mantiki hiyo, Bunge sasa limezuia vituo vyote vya televisheni nchini kupeleka kamera zake ndani ya Bunge kwa kuwa habari hizo zitapatikana kwenye feed maalum ambayo ni ya Bunge ambayo inasimamiwa na waandishi wa Bunge ambao pia ndio wanaamua nini kionyeshwe kwa utashi wao.


Baada ya kutafakari hatua hizi mpya za Bunge na baada ya kufuatilia kile kinachorushwa, mambo kadhaa yamethibitika:-


Mosi, habari kutoka ndani ya Bunge sasa zinachujwa mno kupitia mfumo huu mpya wa feed maalum;


Pili, ubora za picha zinazorushwa kupitia feed hii nao ni wa kiwango cha chini pia;


Tatu, kwa mantiki ya kawaida kabisa, hatua hizi zote zimepunguza na kukwaza haki ya wanahabari kufanya kazi yao kwa uhuru, lakini pia inawanyima wananchi haki ya kupata kwa uhakika na bila kuchujwa kile kinachofanywa na wawakilishi wao.


Kwa kuzingatia haya yote, TEF inasema bayana kwamba:


Hatua hizi mpya za kuzuia kamera za televisheni kuingia Bungeni ni hatua za dhahiri kabisa za kukwaza uhuru wa habari nchini na kukuza censorship nchini. Hali hii haisaidii siyo Bunge tu, bali hata wabunge, wananchi na taifa kwa ujumla katika kupiga hatua za kweli katika kujenga demokrasia na kulinda haki za kupata habari na uhuru wa kujieleza nchini;

TEF imeanza kuingiwa na hofu kwamba sababu za awali zilizokuwa zimetolewa za kuzuia utangazaji wa moja kwa moja wa Bunge kupitia TBC kwa sababu ya gharama, huenda hazikuwa za dhati. Hali hii imejionyesha hasa baada ya vituo binafsi vya televisheni kujitokeza na kuendelea kuonyesha vikao vya bunge moja moja, lakini navyo sasa vimenyimwa fursa hiyo kwa utaratibu huu mpya wa feed maalum.


Ni dhahiri sasa, ushiriki wa wananchi katika kufuatilia mwenendo wa Bunge na wabunge wao umekwazwa sana kwa hatua hizi mpya na kwa maana hiyo, kupunguza ushiriki wa wananchi katika mfumo wa utawala wa nchi yao.


Kwa kuzingatia haya yote, TEF inatoa rai kwa uongozi wa Bunge kufikiria upya hatua hizi za kuzidi kufunika shughuli za Bunge kwenye blangeti zito la usiri na censorship, hivyo uruhusu kituo chochote cha televisheni chenye nia, uwezo na utayari wa kurusha matangazo ya Bunge moja moja bila kulazimika kujiunga na feed maalum iliyoanzishwa.


Tunaamini kwamba kama hali hii ya kutumia feed maalum itaachwa iendelee hakika Tanzania kama taifa tunapiga hatua nyuma kwa yale mazuri machache tuliyokuwa tumeyafikia, mojawapo, uhuru wa Bunge kuendesha mambo yake kwa uhuru na uwazi mkubwa hivyo kuwa mfano mojawapo wa taasisi za umma zinazojiendesha kwa uwazi.


Imetolewa leo, Jumapili Aprili 24 2016 jijijni Dar es Salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania.


Theophil Makunga-Mwenyekiti

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 25 2016 kwenye,Habari zaUdaku, Kitaifa,kimataifa na michezo.


  April 25 2016 naanza kwa kukuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa karibu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamiiyaani facebook/tanzaniampyasasablog na twitter@tanzaniampyasasa.


























 

Gallery

Popular Posts

About Us