Tuesday, July 12, 2016
Sijakurupuka uteuzi wa wakurugenzi - Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, amesema uteuzi wake wa wakurugenzi hakubahatisha kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu katika maendeleo ya nchi kwa kukuza uchumi na kuondoa kero za wananchi.
Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati Wakurugenzi hao wakila kiapo cha maadili, ambapo amesema ametumia muda mwingi ikiwa ni pamoja na kukesha usiku kuwafuatilia mmoja baada ya mwingine ili asifanye makosa katika uteuzi wake.
Rais Magufuli ameongeza kuwa amezingiatia vigezo vya kila mmoja katika utendaji kazi wake huku akitolea ufafanuzi suala la mkurugenzi mmoja kuwa na cheti cha Hotel Menejiment, na kusema kuwa majina kufanana sio kosa hivyo anaezungumzia kwenye mitandao sio aliemteua yeye.
Amesema kuwa ametumia zaidi ya miezi minne kwa kuvihusisha vyombo mbalimbali ili kuwa fahamu vizuri watu atakaowateua ambao wataweza kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi.
Ameongeza kuwa hapo awali ilikua kupata Ukurugenzi kuwa baadhi ya wau walikuwa wanahonga pesa kwa ajili ya kupata nafasi hiyo ambapo amesema kutokana na kulisimamia suala hilo kwa umakini katika kipindi chake hakijatokea kitu kama hicho.
Mhe Magufuli amesema ,Magufuli amesema kuwalikua na mtandao ambao umeundwa kwa ajili ya kupenyeza wakurugenzi wanaowataka hasa katika ofisi za TAMISEMI na tayari ameshaungudua na ameanza kuwaondoa baadhi ya watu waliokuwa wahahusika kufanya udanganyifu huo.
Hakuna Ubaya Mimi Kutoka Kimapenzi na Kajala- Msami
Msanii Msami ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa ‘Mabawa’ amefunguka na kusema kuwa yeye ni mwanaume na Kajala ni mwanamke hivyo kwa kile ambacho kinazungumzwa na watu kuwa huenda anatoka naye kimapenzi
‘Si jambo baya kwani Kajala ni mtoto wa kike na yeye ni mwanaume hivyo chochote kinaweza kutokea kati yao’.
Msami alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWS na kudai kuwa maneno yanazungumzwa juu yake na Kajala huenda yapo na kama hayapo labda yanaweza kuja kutokea, ila anadai yeye na Kajala ni washikaji, ambao wamekuwa wakishirikiana na kusaidia mambo mengi.
“Unajua Kajala ni mtu wangu wa karibu sana, tunaongea mengi na kushauriana vingi japo ukaribu wetu umetafsiriwa tofauti na baadhi ya watu wakidhani tunatoka kimapenzi, japo si vibaya kwani sioni kama kuna ubaya mimi kutoka na Kajala. Sijasema nina mahusiano na Kajala ila ikitokea tukawa wapenzi tunaweza kuzungumza mimi na yeye kujua hatma yake na mume wake ambaye anatumikia kifungo kwa sasa” alisema Msami
Wanafunzi Chuo Kikuu Kizimbani Kwa Mauaji
WATU watatu wakiwemo wanafunzi wawili wa vyuo vikuu vilivyoko jijini Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Wanafunzi hao ni wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Hussein Mustafa (26) na wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Haruna Nkuye (24) ambao wanashitakiwa pamoja na fundi makenika Rajabu Ally (41) wote wakazi wa Dar es Salaam.
Washitakiwa hao wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo kwenye tukio la ujambazi katika Benki ya CRDB eneo la Chanika Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, walisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Jackson Chidunda mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi.
Akisoma hati ya mashitaka, Chidunda alidai Desemba 8, mwaka jana katika eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, washitakiwa walimuua Ramadhani Halili, Shan Rajabu na Thomas Otemu.
Hakimu Shahidi alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo isipokuwa Mahakama Kuu.
Upande wa jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ili wamuunganishe mshtakiwa Mohamed Ungando ambaye jana hakuwepo mahakamani.
Awali, mshitakiwa Mustafa aliiomba mahakama imsaidie apate matibabu kwa kuwa viungo vinamuuma kutokana na adhabu alizopewa akiwa mahabusu.
Hakimu Shahidi alisema gerezani kuna utaratibu wa matibabu, kama hatatibiwa kesi itakapotajwa tena aijulishe mahakama. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 14, mwaka huu.
WEMA SEPETU AMWANDIKIA IDRISS SULTAN UJUMBE HUU
Mrembo Wema Sepetu ambaye jina lake July 11 2016 liliingia kwenye headlines baada ya kutoa viatu vyenye brand ya jina lake, ameingia tena kwenye headlines baada ya kuamua kumuandikia ujumbe Idris Sultan ambaye ni mpenzi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram.Wema Sepetu na Idris Sultan kulikuwa na tetesi kuwa hawapo katika maelewano mazuri lakini usiku wa July 11 Wema Sepetu aliamua kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake instagram uliyolenga kudhihirisha furaha yake kuwa na Idris Sultan.
“Having you as a friend, a brother, a lover & ofcourse a shoulder to cry on everytime Im at my worst has been the best feeling ever… I wouldnt want to lose this feeling over anything… I realised Without u then I aint complete…. You have stood by me in good tyms and bad, & even when I messed up soooo bad you would look me in the eyes and tell me, “Baby, its okay, we gon fix this”… Idris you have been one of a kind and losing u is the last thing I want on this earth… I will love you, until forever, until death do us part we will be together… I will hold on to you till da last minute because together we will get there…. I love you with my life…. For I believe you are my True Love, My baby, and Inshallah The Man that my Kids will call Daddy…
“
Askofu Gwajima Akamatwa na Jeshi la Polisi Muda Mfupi Baada ya Kutua Uwanja wa Ndege
Hatimaye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye amekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi kwa siku kadhaa alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) alipowasili akitokea Japan.
Baada ya Askofu Gwajima kukamatwa na Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa JNIA alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.
Akizungumzia kukamatwa kwake, Kamanda wa Polisi Uwanja wa JNIA, Martin Otieno alisema askofu huyo aliwasili saa 2.45 asubuhi akitokea Japan kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.
Otieno alisema mara baada ya kukamatwa alipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
“Ni kweli tulimkamata Askofu Gwajima hapa uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kuwasili kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya na tulipomuhoji alidai kuwa alikuwa nchini Japan,” alisema Otieno.
Mwanasheria wake Peter Kibatala alisema Gwajima alifika Kituo Kikuu cha Polisi saa 4.45 asubuhi kwa mahojiano mafupi na aliruhusiwa kuondoka baada ya kujidhamini yeye mwenyewe.
“Askofu Gwajima amehojiwa leo (jana) na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu na amejidhamini yeye mwenyewe, ameruhusiwa kuondoka hivyo tunasubiri chochote kitakachoendelea,” alisema Kibatala bila kueleza mahojiano yalivyokuwa.
Askofu Gwajima alikuwa anatafutwa na polisi tangu mwezi uliopita baada ya kusambazwa mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake akipendekeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo sasa Rais John Magufuli anayashughulikia kwa mtindo wa kutumbua majipu.
Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Rais Magufuli asipewe uongozi wa chama hicho kwa sasa kama ilivyo utaratibu wa chama hicho na kwamba hilo likifanyika basi Rais abadili katiba ili mstaafu huyo aweze kufikishwa kortini.
Tangu ulipotolewa mkanda huo, makachero wa polisi wamekuwa wakipiga kambi nyumbani kwa Askofu Gwajima kwa lengo la kumkamata lakini hawakumpata.
Baadaye ilikuja kufahamika kwamba askofu huyo alikuwa amekwenda nje ya nchi lakini haikujulikana ni nchi gani.
Hata hivyo, baada ya kutafutwa na polisi, Gwajima kupitia wakili wake Kibatala alisema atakaporejea nchini atakwenda moja kwa moja polisi kwa ajili ya mahojiano.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amekuwa akisisitiza kwamba jeshi litaendelea kumtafuta askofu huyo kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa, Interpol.