KINGAZI BLOG: 08/28/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, August 28, 2016

Serikali yatangaza Kiama kwa Majambazi

Serikali imesema imejipanga vilivyo kuhakikisha inawalinda raia na mali zao na kwamba watakao bainika kujihusisha ama kuunga mkono vitendo vya uhalifu ukiwemo ujambazi pamoja na kulibeza jeshi la polisi, watachukuliwa hatua kali.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na maafisa wa jeshi la polisi ,uhamiaji,magereza na vyombo vingine vya ulinzi na usalama usalama,katika mkutano uliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya polisi Moshi mkoani Kilimanjaro nakusema kuwa serikali haita fumbia macho uhalifu

Aidha Waziri Nchemba amelipongeza jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa weledi huku akilitaka lishirikiane na jamii kuzidisha juhudi za ulinzi kwenye maeneo ya pipakai, ili kuthibiti mtandao wa wahamiaji haramu ,magendo ,pamoja na ule wa uingizaji wa madawa ya kulevya nchini .

Pia Waziri Nchemba,katoa angalizo  kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushiriki vilivyo katika kufanikisha zoezi la uandikishaji vitambuklisha vya uraia

66 walazwa kwa kunywa togwa harusini

Wakazi 66 wa Kijiji cha Lyangweni wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, wamelazwa katika zahanati kwa matibabu baada ya kunywa togwa inayodhaniwa kuwa na sumu.

Afya za watu hao waliokuwa kwenye sherehe ya harusi zilibadilika ghafla juzi usiku, baada ya kuanza kuharisha na kutapika kabla ya kuwahishwa katika zahanati hiyo kutibiwa.

Hilo ni tukio la pili kutokea katika eneo hilo ndani ya miaka miwili baada ya watu wengine takriban 400 kudhurika na kinywaji hicho, Oktoba 2014.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songea, Yesaya Mwasubira amesema jana kuwa wagonjwa hao walipokewa kwa nyakati tofauti na hadi saa nane juzi usiku walikuwa wamefikia 63.

Amesema wagonjwa wengine watatu walipelekwa katika zahanati hiyo jana asubuhi baada ya afya zao kozorota.



Hebu ona haya!! MWANAUME ABEBA MAITI YA MKEWE BEGANI KWA ZAIDI YA KM 12.

Mwanamume mmoja nchini India inasemekana hakuwa na uwezo kifedha ili kuweza kusafirisha maiti ya mkewe kwa kutumia gari ya kubebea wagonjwa hadi kijijini kwao na hivyo ikambidi kuibeba maiti ya mkewe kwa umbali wa zaidi ya kilomita 12, kutoka hospitali aliyofariki, kwani ilishindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alilazwa hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa. siku ya Jumanne na alifariki dunia siku inayofata kwani alikua akiugua maradhi ya kifua kikuu. katika Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilomita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.

Bwana Mahji, ilimbidi achukue maiti hiyo kwani kwa madai yake wahuduhu walimsihi kufanya hivyo, na alipowaomba wamsadie gari ya kubebea maiti hakuweza kupata ndipo uamuzi wa kumbeba mkewe begani na kuanza safari kuelekea kijijini Melghar kufuata mila na tamanduni za mwisho huku akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12

Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na wakaamua kumsaidia gari la kubebea wagonjwa mpaka wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake ambako shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.





HII NDO OFFICE YA MKE WA MENGI JACQULINE NTUYABALIWE

Anaitwa Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lynn Miss Tanzania 2000 na Mwanamuziki, Mke wa Bilione Reginald Mengi.

Nimekutana na Comments Mbali mbali Instagram Baada ya Picha hii kuzagaa mitandaoni leo hii

embu na wewe jisomee baadhi ya comments kutoka Instagram;

fetttyy 

Huyo ndo boss lady Africa nzima ndo hapigi kelele wala kujionyesha onyesha anajua anazo lakini hawa visokorokwinyo wengine ngachoka miyeeee kutwa kutuigizia insta

mariebellahfonte 

Njoen mumuone boss lady Wa ukweli

angie_jansie 

Watoto wa kigoma hatunaga makuu huwa tunasemaga papa Asante kwel wewe ni Mungu tu.....

paulina_minango 

Kwakweli huyu ndie bosslady wengine wanatafuta kiki tu mjini anajielewa huyu dada mrs mengi#jn_mengi

hallopkingu 

@kittynswe ahaha nilijua ni mm tuu ndo namkubali huyo bosslady.. woman of class

tedysilla___ 

Nampenda mnooo uyu dda anajielewa michirz angekuwa na maisha kama ya uyu dda tungekoma

Chocolate Zinavyohusishwa na ‘Uwezo wa Akili’ Kwa Wanafunzi Darasani

Wakati wazazi wengi nchini wakihaha kudhibiti ulaji holela wa vitu vitamu kwa watoto wao ili kuimarisha afya ya kinywa. utafiti mpya wa hivi karibuni umeibuia mapya baada ya kubainika kuwa ulaji mzuri wa chocolate unaweza kuongeza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoa fursa kwa watoto kufanya vizuri darasani.

Aidha, utafiti huo umebaini vilevile kuwa ulaji wa chocolate husaidia kupunguza kasi ya kawaida ya kuzeeka kwa walaji itokanayo na kuongezeka kwa umri. Ripoti ya utafiti huo ilitolewa hivi karibuni, inabebwa na utambulisho usemao ‘ulaji wa chocolate huongeza utendaji kazi wa ubongo” na kwamba ”unaweza kusaidia mtu kutozeeka haraka licha ya umri kuzid kumtupa mkono’

Utafiti huo uliochapichwa mwezi huu katika jarida la Appetite, umebaini kuwa kumbukumbu na uwezo wa kufikiria ufumbuzi wa mambo magumu kuwa katika kiwango cha juu kwa watu wanaokula chocolate kwa wingi. Matokeo hayo yameripotiwa kutoathiriwa na umri wa mlaji, uzito wa mwili wala aina nyingine za ulinganifu wa jumla wa kiafya .

Inaelezwa zidi kuwa utafiti huo unaonyesha kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ulaji wa kila mara wa chocolate na matokeo ya majaribio kuhusu uwezo wa uubongo katika kufikiri hata hivyo utafiti huo haujathibitishwa kwa asilimia 100 juu ya uhakika wa kisayansi juu ya kile kilichobainishwa.

Aidhja imeonekana watu wanotumia zaidi chocolate walikuwa na lishe bora zaidi na pia kunywa pombe kwa kiasi kidogo, na makundi yote yalitegemea uwezo wa kukumbuka mambo kupitia kiwango chao cha ulaji wa Chocolate.

SOURCE: NIPASHE

53 mbaroni wakidaiwa kufanya matukio ya ugaidi Kilindi

Tanga. Watuhumiwa 53 wa matukio yenye viashiria vya ugaidi yaliyotokea wilaya za Kilindi na Amboni mkoani Tanga, wapo katika mahabusu za magereza wakisubiri michakato ya kusikilizwa kesi zao pamoja na hukumu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema juzi kuwa idadi hiyo inajumuisha watuhumiwa waliokamatwa mwaka juzi Kilindi na wengine waliohusishwa na matukio ya uhalifu katika mapango ya Amboni jijini Tanga huku baadhi yao wakinaswa nchini Kenya.

Wakulyamba amesema hayo  wakati akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipowasili kwa ziara ya kikazi.

Amesema Aprili 20, wakazi wa Mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla walikuwa katika wakati mgumu, kufuatia kundi la wahalifu hao kuvamia duka la Central Bakery na kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wanne.

Mwimbaji Ruby Akimbilia EFM Radio Baada ya Ugomvi wa Maslahi Kati ya Mwimbaji Huyo na Clouds FM

Mwimbaji Ruby ambae alikuzwa na kulelewa na Clouds FM Baada ya Kufanya vizuri katika mashindano ya Fiesta Diva Nyota miaka kadhaa iliyopita amejikuta katika ugomvi wa kimaslahi na walezi wake Clouds FM baada ya kushindwana malipo katika Matamsha ya Fiesta yanayoendelea hivi sasa..

Ruby kwa sasa inaonekana amekimbili kwa washindani wa Clouds FM ambani ni EFM Radio, Radio hiyo mpya ambayo ni washindani wa Clouds FM kwa jijini Dar es Salaam wamechukua fursa hiyo na sasa wanamtumia katika matamasha yao ya Mziki Mnene Sehemu mbali mbali

LA HAULAH!!! MUME AKIRI KUMCHINJA MKEWE


Naveen Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa kwa mauaji 
Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao mjini LondonNaveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.
Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.Uchunguzi wa kifo chja mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa.

Tahira Ahmed alipatikana akiwa amechinjwa nyumbani kwao mjini LondonBwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Kipato Kupitia Mitandao Ya Kijamii

Mwaka jana tuliandaa semina kwa njia ya mtandao ambapo tulitoa elimu ya jinsi ya kutengeneza kipato kwenye mtandao kwa kutumia blog. Baadae tulitoa kitabu ambacho kiliendelea kutoa elimu hii ya kumwezesha mtu yeyote kutengeneza biashara yake kupitia mtandao kwa kuw ana blog ambayo inatoa elimu fulani watu wanayohitaji.

Watu wengi wamejipatia kitabu hiki na wengi wamefungua blog zao ambazo sasa zimeshaanza kupata wasomaji ambao wanazifuatilia kwa makini. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki kwa kusoma

JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. 
Ili uweze kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog kwanza itakuhitaji muda wa kuanza kujenga wasomaji wanaokuamini, itakuhitaji wewe ujifunze sana na ujiweke kama mtaalamu kwenye lile eneo ambalo umechagua kuandikia na kutoa elimu kwa watu wengine. Pia utahitaji kuwa na kompyuta ili uiendeshe blog yako kitaalamu zaidi. Sasa mahitaji haya yanaweza kuwa kikwazo kwa watu wengi ambao wanataka kutengeneza kipato kupitia mtandao.

Leo nakushirikisha njia nyingine ya kutengeneza kipato kwenye mtandao kwa kutumia mitandao ya kijamii. Wote tunajua kwamba dunia ya sasa karibu kila mtu yupo kwenye mtandao wa kijamii. Kuna mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu na watu wengi wanaitumia, hata wewe pia unaitumia. Sasa leo nataka nikupe ujanja wa jinsi unaweza kuitumia mitandao hiyo kutengeneza kipato ili uweze kubadili hali yako ya kipato.

Ni mitandao ipi ina watumiaji wengi kwa hapa Tanzania?
Kwa Tanzania kuna baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo ina watumiaji wengi sana. Kwanza kabisa ni mtandao wa kijamii unaoitwa facebook, huu ndio unaongoza duniani na hata hapa tanzania umejizolea watumiaji wengi sana.

Karibu kila mtu anayetumia mitandao ya kijamii yupo facebook. 
Mtandao mwingine wenye watumiaji wengi ni instagram. Huu ni mtandao ambao umechipukia kwa kasi sana hapa tanzania na umepata umaarufu mkubwa na watu wengi kuufuatilia. Ni mtandao ambao ni rahisi sana kutumia na kule watu wanaweka picha tu na maelezo.

Twitter nao pia ni mtandao wa kijamii ambao watanzania wengi wanatumia, ila waliomiliki sana mtandao huu ni watu maarufu kwenye jamii kama viongozi au wasanii. Twitter sio mtandao ambao unavutia wengi kuwepo kwa sababu unahitaji kuweza kutoa ujumbe kwa maneno machache sana na hivyo hii ni changamoto kwa wengi.

Linkedin pia ni mtandao wa kijamii ambao umekaa kitaaluma na kitaalamu zaidi. Kupitia linkedin mtu anaweza kuweka wasifu wake na nafasi anazoweza kufanyia kazi na ikawa rahisi wenye uhitaji kumfikia. Ni mtandao ambao haujakaa kiumbea umbea kama mingine na hivyo hauna watumiaji wengi kutoka Tanzania.

Kwa madhumuni ya makala hii nitajadili mitandao miwili ambayo watanzania wengi wanaitumia ambayo ni facebook na instagram.
Je inawezekana kutengeneza fedha kwa kupitia mitandao ya kijamii?

Watu ambao wana marafiki au wafuasi wengi kwenye mitandao hii ya kijamii wamekuwa wanatengeneza fedha kupitia mitandao hii. Watu hawa hufanya kazi na makampuni yanayohitaji kujitangaza na makampuni hayo kuweka matangazo kwenye kurasa zao kwenye mitandao hii na hivyo wao kutengeneza kipato. Na ili kuhakikisha wanaendelea kutengeneza kipato wanatafuta njia bora za kukutumia wewe.

Wanachotaka ni wewe uwe na hamasa ya kuwafuatilia na ukifika pale unakutana na matangazo mbalimbali. Watu hawa wenye wafuasi wengi wamekuwa wakitengeneza ugomvi usio na maana ili tu kuwafanya watu wengi wawafuatilie na hivyo wao kukuza biashara zao za kuuza matangazo.

Makampuni mengi yamekuwa yakitafuta njia nzuri ya kutangaza biashara zao kupitia mitandao hii ya kijamii na njia kubwa wanayoiona ni nzuri ni kutumia watu wenye wafuasi wengi.
Wewe unawezaje kutengeneza kipato kupitia mitandao hii?

Swali zuri sana, na hapa ndio ninataka nikupe maarifa ambayo yatabadili maisha yako kama utayatumia. Tumeshaona mitandao ya kijamii inayotumika sana kwa tanzania na pia tumeshaona kwamba inawezekana kutengeneza fedha kwenye mitandao hii ya kijamii kama ambavyo tayari kuna watu wanaotengeneza fedha kupitia mitandao hii.

Sasa je wewe unawezaje kutengeneza fedha pia? Kumbuka labda wewe sio mtu maarufu hivyo una
wafuasi au marafiki wachache. Na makampuni mengi yanayotaka kutangaza kupitia mitandao hii wanataka watu wenye wafuasi wengi.

Hapa ndio wakati wa kutumia akili yako vizuri na ukiweza kufanya hivi utatengeneza kipato kikubwa mpaka mwenyewe utashangaa ulikuwa wapi hukujua hilo mapema. Hivyo twende pamoja na fanyia kazi yale ambayo unajifunza hapa.

Tuseme wewe ni kijana ambayo huna kazi ila una simu yenye uwezo wa kuingia kwenye mitandao hii. Kama umeshatumia mitandao hii kwa muda umeshajijengea marafiki na wafuasi kadhaa kupitia mitandao hii. Lakini siku zote umekuwa unaingia kwenye mitandao hii na kutoka bila ya kutengeneza kipato chochote.

Sasa leo nataka uwe na mpango tofauti. Kama tulivyoona hapo juu ni kwamba makampuni mengi yanakimbilia kutangaza kupitia watu wenye wafuasi wengi. Makampuni haya yanata fedha nyingi kwa muda mfupi na tangazo lao linakaa muda mfupi pia. Wewe njoo na mpango wa kuyasaidia makampuni haya kujenga wafuasi wengi kupitia mitandao hii ya kijamii.

Badala ya makampuni haya kulipa ada kubwa ya matangazo mara moja, kwa nini yasitengeneze wafuasi wake wenyewe ambao wataendelea kuwatangazia bure kila siku? Hiki ni kitu ambacho makampuni mengi hayaelewi na unahitaji kuwaelewesha na kuwapa mpango wako wewe.

Mpango wako unakuwa ni kuyasaidia makampuni kuendesha kurasa zao kwenye mitandao hii ya kijamii. Unayasaidia makampuni haya kupata wafuasi wengi, unatoa taarifa muhimu za makampuni hayo, unaendesha mashindano madogo madogo, vyote hivi vinaisaidia kampuni kupata wafuasi na kuwatangazia, huku wewe ukitengeneza kipato.
Kwa kifupi unahitaji kuwa na mpango huu;

1. Kuwa na mpango w akuweza kuisaidia kampuni kuongeza wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii. Unaweza kuanza na mitandao miwili yenye watumiaji wengi Tanzania, ambayo ni facebook na instagram.

2. Weka ada ndogo kwa kila siku ambayo kampuni unayofanya nayo kazi itakulipa. Hakikisha ni ada ndogo kiasi kwamba kampuni unayofanya nayo kazi haioni kama inapoteza fedha.

3. Toa mpango huu kwa makampuni mengi, kila kampuni unayoijua na ambayo huwa inatangaza kwenye mitandao hii wape mpango wako huo. Na hata kama kuna kampuni haijajua kutangaza kupitia mitandao hii ni wakati mzuri wa kuwajulisha hilo. Unapotoa mpango wako kwa makampuni mengi, kuna machache ambayo yatakubali.

4. Fanya kazi vizuri sana na makampuni haya na hii ndio itakuwa wasifu wako wakati unaendelea kuomba kufanya kazi hii na makampuni mengine. Kama utaweza kuonesha kwamba umeyasaidia makampuni mengine kukuza wafuasi na kutangaza kwa wengi kupitia mitandao hiyo, itakuwa rahisi kwa makampuni mengi kutaka kufanya kazi na wewe.

Unahitaji kutengeneza mpango bora ambao utatoa thamani kubwa kwa kampuni yoyote ambayo itakuamini wewe. Mambo hayo manne hapo juu ni muhimu kuyazingatia.

Mambo yatakayokuzuia kufanyia kazi hiki ulichojifunza leo;
Kuna baadhi ya mambo ambayo yatakuzuia kufanyia kazi hiki nilichokushirikisha hapa leo. naomba niyaweke wazi hapa ili unaposhindwa ujue umeamua mwenyewe.

1. Hupo tayari kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kufikiri zaidi, kuwa mbunifu na kuongeza thamani kwenye biashara za wengine.

2. Unaogopa kutoa mapendekezo kwa kampuni usiyomjua mtu kwa sababu watakataa. Au utaongea na makampuni machache na yatakataa. Sasa kama unaogopa kwa sababu yatakataa, mpaka sasa ambapo hujatoa mapendekezo wamekataa, kwa nini usitumie mbinu nzuri kuwashawishi? Halafu ukiongea na makampuni kumi yakakataa ni kitu cha kawaida. Nitafute utakapokuwa umeongea na makampuni 100 na yote yakakataa, nitakupa mbinu za tofauti.

3. Uko tayari kushabikia timu nani na timu nani ila hupo tayari kutumia mitandao hii kwa faida yako na ya wengine. Sijui wewe kuwa kwenye timu ya mtu ambayo hata haiendi uwanjani unalipwa kiasi gani, unahitaji kuachana na huu ujinga na ufikirie kutengeneza kipato.

4. Uko tayari kuendelea kuona wivu kwenye maisha ya kuigiza kuliko kufikiria ni kipi ufanye ili kutengeneza fedha kwenye mitandao hii ya kijamii. Umekuwa unaona watu wanavaa vizuri kuliko wewe, wanaonekana kuwa kwenye ofisi nzuri kuliko wewe, wamepiga picha wakiwa wanacheka na kufurahi, wakiwa wanakula vyakula vizuri, wakiwa wapo kwenye sehemu nzuri za mapumziko.

Na huenda kwa kuona wengine kwenye picha hizi unaona wewe ndio hujielewi. Sasa achana na mambo hayo ya kuonea wivu kwa sababu sehemu kubwa ya mambo unayoona kwenye mitandao ya kijamii ni maigizo.

Au angalau watu hawakuoneshi wakiwa wanapitia matatizo yao binafsi, wakiwa wanakazana kupata fedha, wakiwa wanapambana na ugumu wa maisha. Wewe fikiria jinsi ya kuweza kuongeza thamani kwa wengine kupitia mitandao hii.

BAADA YA DAVIDO WIZKID NAYE APATA DILI LA KUFANYA KAZI KAMPUNI YA SONI MUSIC

Baada ya January mwaka huu mkali kutoka Nigeria Davido kutangazwa kupata deal la kusaini mkataba na kampuni kubwa ya muziki Duniani Sony Music Worldwide sasa ni zamu ya Wizkid.
Kwa mujibu wa TheNETng ni Exclusive mkali Wizkid anaenda kusaini mkataba wa kimataifa na kampuni ya Sony Music Worldwide muda wowote kuanzia sasa.
Hatua hiyo itakuwa ni muendelezo wa harakati za msanii Wizkid katika kuufikisha muziki wake katika uso wa Dunia. Na pia ni hatua kubwa kwa kwa muziki wa Nigeria ukiangalia miezi michache iliyopita pia mwanadada Tiwa Savage kutoka nchini humo pia alidondosha wino kwenye karatasi za lebel kubwa ya muziki Duniani Roc Nation ambayo inamilikiwa na mtu mzima Jay Z.
Kipindi Davido akidondosha sain kwenye kampuni hiyo

PICHAZ + INASHANGAZAA!!! MTOTO ALIYENENEPA ZAIDI DUNIANI ARUDI SHULENI BAADA YA KUPUNGUZA UZITO

Mtoto wa miaka 10 kutoka Indonesia, ambaye ametajwa kuwa mtoto aliyenenepa zaidi duniani alianza kupewa chakula cha kupunguza uzito Arya Permana ameorodheshwa kuwa na unene usio wa kawaida kwa kuwa alikuwa na uzani wa kilo 188.
Mtoto huyu hatimaye ameweza kurudi shuleni baada ya kupunguza uzito wa kutosha wa kumwezesha yeye kutembea kwani siku zote alikuwa akillala na hakuweza kutembea na kusababisha yeye kukatisha masomo.
Mtoto huyu unaambiwa amekuwa akila milo mitano kwa siku lakini baada ya ushauri wa kufanya diet na mazoezi makali Arya ameanza kupunguza uzito ndani ya wiki chache sasa anaweza kukaa lakini pia kutembea kwenda shule na kucheza na wenzake darasani

 











SABABU ZA JPM KUMTEUA DKT KILIMBA KUWA DG WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA

Tarehe 24 mwezi huu, Rais Dokta John Magufuli alimteua Dokta Modestus Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu (DGIS) wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Uteuzi huo umefanyika kufuatia kustaafu kwa mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Othman Rashid.
Makala hii inajikita katika uchambuzi wa uteuzi huo kwa kuangalia changamoto na fursa zinazomkabili kiongozi huyo mkuu wa taasisi hiyo nyeti kabisa. Kwa mtizamo wangu, kama kuna kitu ambacho kinaweza kuzua maswali kuhusu uteuzi huo basi ni wadhifa wa Director of Risk Management alioshikilia Dokta Kipilimba huko nyuma alipokuwa mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Sote twafahamu jinsi Benki Kuu yetu imekuwa ikiandamwa na matukio mfululizo ya ufisadi, kuanzia EPA hadi Tegeta Escrow. Kwa wadhifa wake katika taasisi hiyo, kuna uwezekano wa bosi huyo mpya wa mashushushu kuonekana ‘sehemu ya mfumo ulioshindwa kudhibiti ufisadi.’ Hata hivyo, utetezi unaweza kuwa huenda yeye alitekeleza majukumu yake vema lakini walio juu yake hawakuchukua hatua stahili.
Kadhalika, huko mtandaoni kuna ‘tuhuma’ kadhaa kuhusu Dokta Kipilimba, lakini itakuwa sio kumtendea haki yeye, blogu hii na mie mwenyewe kujadili tuhuma ambazo hazina ushahidi wowote. Ni muhimu kutambua kuwa Tanzania yetu licha ya kuwa kisiwa cha amani pia ni kisiwa cha majungu, uzandiki, fitna, umbeya na uzushi.

Changamoto kubwa kwa Dokta Kipilimba ni pamoja na kurejesha hadhi na heshima ya Idara ya Usalama wa Taifa. Katika miaka ya hivi karibuni, taasisi hiyo muhimu kabisa imekuwa ikishutumiwa kuwa inachangia ustawi wa ufisadi, ujangili, biashara ya madawa ya kulevya, nk. 

Wanaoilaumu taasisi hiyo hawamaanishi kuwa watumishi wake wanahusika katika matukio hayo ya kihalifu as such bali kushindwa kwa Idara hiyo kukabiliana na kushamiri kwa matendo hayo ya kihalifu, ambayo kimsingi ni matishio kwa usalama wa taifa, na kazi kuu ya Idara hiyo ni kukabiliana na matishio kwa usalama wa taifa la Tanzania.

Ninaamini kuwa Dokta Kipilimba anafahamu kanuni muhimu kuhusu ufanisi au mapungufu ya idara ya usalama wa taifa popote pale duniani, kwamba “kushamiri kwa vitendo vinavyotishia usalama wa taifa lolote lile ni kisheria cha mapungufu ya idara ya usalama wa taifa ya nchi husika, na kudhibitiwa kwa vitendo vinavyotishia usalama wa taifa popote pale duniani ni kiashiria cha uimara wa idara ya usalama wa taifa ya nchi husika.”

Kwahiyo, kwa kuzingatia kanuni hiyo, kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya, ujangili, rushwa, na ufisadi mwingine ni viashiria vya mapungufu ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa.

Changamoto nyingine kwa Dokta Kipilimba ni tuhuma za mara kwa mara dhidi taasisi hiyo muhimu kabisa kuwa katika utendaji kazi wake imegeuka kuwa kama ‘kitengo cha usalama cha chama tawala CCM.’ Idara hiyo imekuwa ikituhumiwa kuwa kwa kiasi kikubwa imeweka kando taaluma ya ushushushu (tradecraft) na kutekeleza majukumu yake kisiasa.

Madhara ya muda mfupi ya kasoro hiyo ni taasisi hiyo kujenga uhasama na vyama vya upinzani na kwa namna flani kupoteza heshima na uhalali wake. Lakini la kuogofya zaidi ni madhara ya muda mrefu, ambapo watu wanaoweza kuwa ni matishio kwa usalama wa taifa letu wanaweza kutumia ‘urafiki’ unaodaiwa kuwepo kati ya Idara ya Usalama wa Taifa na CCM, wakitambua bayana kuwa ‘Idara haina muda na makada wa chama tawala,’ na hatimaye kufanikiwa kutimiza azma zao ovu.

Baadhi ya watumishi wa zamani wa taasisi hiyo walijikuta matatizoni kwa vile tu walitekeleza majukumu yao dhidi ya wanasiasa wa chama tawala, na wakaishia kuonekana kama wahaini.

Changamoto nyingine kwa Dokta Kipilimba ni tuhuma zinazoikabili taasisi hiyo kuhusu mfumo wa ajira ambapo inadaiwa kuwa zimekuwa zikitolewa kwa upendeleo kwa ndugu na jamaa za ‘vigogo.’ Tatizo kubwa hapa ni kwamba utiifu wa ‘ndugu na jamaa hao wa vigogo’ haupo kwa taifa bali kwa vigogo hao waliowaingiza Idarani. Pengine sio vibaya kufikiria ‘utaratibu wa wazi’ katika ‘recruitment’ kama inavyofanywa na wenzetu wa CIA, NSA, MI5, MI6, HGCQ, nk wanaotangaza nafasi za ajira kwenye vyombo vya habari.

Pia kuna tatizo la baadhi ya maafisa usalama wa taifa ‘kujiumbua’ kwa makusudi kwa sababu wanazojua wao wenyewe, kubwa ikiwa kutaka sifa tu, au waogopwe ‘mtaani.’ Hii inaathiri sana ufanisi wa maafisa wa aina hiyo kwani ni vigumu kutekeleza majukumu yao ipasavyo pasi usiri.

Sambamba na hilo ni kasumba ya muda mrefu ambapo baadhi ya maafisa wa Idara hiyo waliopo kwenye vitengo mbalimbali kuwepo huko kwa muda mrefu mno kiasi cha kuathiri utendaji wao. Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na ‘vituo muhimu’ na kwenye ofisi za balozi zetu nje ya nchi. Ikumbukwe kuwa unless afisa ametengeneza deep cover, uwepo wake kwa muda mrefu katika sehemu aliyokuwa ‘penetrated’ au kituo chake cha kazi kwingineko (mfano ubalozini) unaweza kupelekea ‘akaungua’ (burned).

Changamoto nyingine kubwa ni uwepo wa majasusi kibao nchini mwetu, hususan kutoka nchi moja jirani, huku wengi wa majasusi hao wakiwa wameajiriwa katika taasisi za umma na binafsi. Hili ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa wa Tanzania yetu. 

Kwa upande fursa kwa Dokta Kipilimba, licha ya kuwa ‘mwenyeji’ katika taasisi hiyo muhimu, wasifu wake kitaaluma unamweka katika nafasi nzuri sana kukabiliana na changamoto za karne ya 21 ambayo imetawaliwa zaidi na teknolojia ya kisasa.

Dokta Kipilimba ni msomi aliyebobea kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na yayumkinika kuamini kuwa anaweza kutumia usomi wake kuibadilisha Idara yetu ya Usalama wa Taifa kwenda na wakati, kufanya kazi kama taasisi ya kishushushu ya karne ya 21, ambayo licha ya kutegemea HUMINT inaweza pia kutumia njia nyingine za kukusanya taarifa za kiusalama kwa kutumia teknolojia (GEOINT, MASINT, SIGINT, CYBINT, FININT na TECHINT kwa ujumla.

Fursa nyingine kwa Dokta Kipilimba ni matarajio ya sapoti ya kutosha kutoka kwa Rais Dokta Magufuli ambaye kama alivyoahidi wakati wa kampeni za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana, mapambano dhidi ya ufisadi yamepewa kipaumbe cha hali ya juu kabisa. Kama ‘sponsor’ na ‘consumer’ wa taarifa za kila siku usalama, inatarajiwa kuwa Dokta Magufuli atatekeleza ushauri wa Idara katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama wa taifa letu.

Dokta Kipilimba ana fursa ya kuleta mageuzi kwa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kuangalia uwezekano wa kuwafikia watu walio nje ya taasisi hiyo, hasa pale uwezo wa Idara yetu unapokuwa limited. Nitoe mfano. Katika kupata taarifa mwafaka wa kudumu kuhusu, kwa mfano, mgogoro wa kisiasa huko Zanzibar, Idara inaweza ku-reach out wanazuoni wa historia ya taifa letu walipo ndani na nje ya nchi yetu. 

Ikumbukwe kuwa sio rahisi kwa taasisi hiyo kuwa na maafisa au watoa habari katika kila eneo. Wenzetu wa nchi za Magharibi wamekuwa wakikabiliana na hali hiyo kwa kufanya kazi na ‘makandarasi’ (contractors), ambao of course, wamekidhi taratibu kama vile vetting.

Sambamba na hilo ni Idara hiyo kuangalia uwezekano wa kutumia hazina kubwa tu ya maafisa wake wa zamani, hususan wastaafu Ikumbukwe kuwa wengi wao ni watu wanaowindwa na ‘subjects’ mbalimbali wanaolenga kulihujumu taifa letu.

Nimalizie makala hii kwa kutoa pongezi za dhati kwa Dokta Kipilimba na Naibu wake (DDGIS) Robert Msalika, sambamba na kumtakia mapumziko mema Mkurugenzi mstaafu Othman, na kumkaribisha ‘uraiani.’ 

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI IDARA YETU YA USALAMA WA TAIFA

Chadema wadaiwa kuhonga vijana Sh 40,000 kuelekea siku ya UKUTA

POLISI Kanda ya Dar es Salaam imekituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwalipa fedha kiasi cha Sh 40,000 baadhi ya vijana ili washiriki katika maandamano ya Ukuta ya Septemba Mosi yaliyopigwa marufuku.

Aidha, imesisitiza imejipanga kikamilifu kukabiliana na watu watakaovunja sheria kwa kufanya maandamano hayo ambayo yamepigwa marufuku kwa lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro wakati akizungumza jijini Dar es Salaam ambapo alisema, kwa sasa jiji hilo liko shwari na hata baada ya Septemba Mosi, litaendelea kuwa shwari.

“Naomba niwasihi Wana Dar es Salaam hasa vijana wasiingie barabarani hiyo tarehe moja, tuwaachie wachache ambao nia yao ni kuleta fujo, wote tunajua madhara ya fujo, wote tunajua hasara ya fujo, siku hiyo imetolewa katazo hakuna maandamano,” alisema Sirro.

Alisema kwa taarifa za intelijensia walizonazo zinaonesha kuna watu wanapewa fedha kwa ajili ya kuandamana na kufanya fujo, ambapo alitoa rai kwa wazalendo wa nchi wasiopenda kupambana na Jeshi la Polisi ambalo linawalinda wao na mali zao wasithubutu kuingia barabarani.

Akizungumzia tuhuma hizo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema, chama hicho hakina fedha za kuwalipa vijana ili kufanya maandamano na kusisitiza; “Tukutane tarehe moja Septemba.”

Julai 27, mwaka huu Chadema ilizindua operesheni iliyopewa jina la Ukuta ikiwa na lengo la kupambana na kile ilichokiita udikteta nchini, huku ikitangaza kushirikiana na wale watakaoona umuhimu wa kuwepo kwa haki na demokrasia nchini.


WEMA SEPETU YAMEMSHINDA,AAMUA KUJIRUDI KWA IDRISS,CHECK ALICHOMFANYIA IDRISS SULTAN


Uhusiano wa Wema Sepetu na Idris Sultan unaanza kutukumbusha ule wa Chris Brown na Karrueche Tran ule wazungu wanauiita ‘off and on.’
Baada ya hivi karibuni kuzinguana tena hadi kumfanya Idris ajiondoe Instagram hadi sasa, wawili hao wanaonesha kuanza kutafuta suluhu.
Wema amepost picha hiyo juu Instagram inayoonesha walikuwa wakiwasiliana kutumia app ya Facetime, aliandika: That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi basi… hata kidogo tu… 😔
Wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya Wema kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika mwezi uliopita.
Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo yalipoharibika.
Mashabiki wa Wema walikasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia Instagram. Kutokana na kuandamwa, Idris amelazimika kuongea:
Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?
Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja.
“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa.
Hata hivyo Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao ni Diamond.

Hebu muone GIGY MONEY picha hizi za utata mtandaoni.



 


 

Magazeti ya leo jumapili ya tar 28


 


 
 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 



 

Gallery

Popular Posts

About Us