KINGAZI BLOG: 08/17/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, August 17, 2016

BREAKING NEWSS :Waliotafuna Fedha za Mikopo Wapewa Siku Saba Kuzirejesha

Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu (HELSB)na wa vyuo vilivyohusika kufanikisha malipo ya fedha za mikopo kwa wanafunzi hewa kuchukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kurudisha fedha zilizochukuliwa na wanafunzi hao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Joyce Ndalichako .

“Kutokana na mambo yaliyobainika serikali imechukua hatua ikiwemo kuvitaka vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku Saba kuanzia leo, ” amesema.

Amesema vyuo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambazo fedha za mikopo hulipwa ili kuondoa udanganyifu.

“Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa zote za wanafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili,” amesema

London: Wateja wala chakula wakiwa watupu mgahawani

 Katika hali isiyokuwa ya kawaida mgahawa mmoja  jijini London Uingereza umechukua chati ya aina yake kwakuwa na huduma ya kipekee ambapo wateja wake hula  vyakula mbalimbali wakiwa utupu.

Mradi wa kujenga Mgahawa huo wa Bunyadi ulitangazwa na kampuni ya Lollipop Aprili 19 mwaka 2016 na kufunguliwa rasmi tarehe 11 Juni 2016 chini ya mwanzilishi wake Seb Lyall pamoja na timu yake.

Mgahawa huo wa Bunyadi upo kusini mwa mji wa London katika vitongoji vya Elephant na Castle ,una uwezo wa kupokea wateja takribani 42 kwa wakati mmoja na hadi sasa taarifa kutoka mji huo zinasema kuwa takribani watu 42,000 tayari wameweka oda ya kula katika mgahawa huo.

 “Naamini kuwa watu wanahaki ya kupata nafasi ya kufurahi bila vizuizi vyovyote kama rangi bandia, umeme, kemikali, simu za mkononi, na hata nguo kama wakitaka,wazo langu kuu ni ukombozi wa kweli” Alisema Lyall

Lyall pia anahusika na bar mbili za Owl Bar na Shoreditch’s Breaking Bad cocktail bar zenye utata mkubwa jijini London.Kampuni yake pia inajulikana kwa kuwa nyuma ya ugunduzi wa programu za simu kama Locappy na Hoot London ambazo ni maarufu sana katika jiji la London.




TCRA waja na kampeni hii kudhibiti makosa ya mtandaoni.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) James Kilaba amewataka wadau wa mawasiliano nchini kujiepusha na sheria za ukiukwaji wa mitandao kwa kutokusambaza ujumbe ulio na maudhui ya uchochezi na uzushi.

James Kilaba ameyasema hayo wakati akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam  juu ya matumizi sahihi na salama ya mitandao mbapo amesema kuwa watumiaji wa mitandao wanatakiwa kutotoa maudhui ya uchochezi pindi wanapo pokea ujumbe huo kwa mtu mwingine.

“Nina wataka mfute maramoja pindi mnapopokea taarifa za uchochezi na kutoa taarifa kwa wanaohusika mnazipokea taarifa hizo” Alisema Kilaba.

Kilaba ameongeza kuwa watuamiaji wa mitandao wasitengeneze akaunti kwa lengo la kufanya utapeli au kutumia taarifa zisizo za kwao na kusisitiza kuwa wanatakiwa kutunza vifaa wanavyohifadhia kumbukumbu zao.

Kufuatia hali hiyo TCRA wamezindua kampeni ya TZ-CERT(Tanzania Computer Emergency Response Team) kwa lengo la kuongeza ufahamu kwa watumiaji wote wa mtandao baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto kwa watumiaji wa mitandao, hivyo kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu kupitia mtandao wa Facebook, Twitter.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa leo Katika Magazeti na Mitandaoni

Orijino Komedi Wahojiwa na Kushikiliwa na Jeshi la Polisi Dar


Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo Agosti 17, 2016 imewahoji na kuwashikilia wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa makosa ya kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za jeshi hilo kinyume cha sheria.

Taaifa ya kusakwa kwa Orijino Komedi zilitolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kufuatia wasanii hao maarufu wa komedi hapa nchini kuvaa nguo ambazo zinashabihiana na sare za jeshi hilo wakati wakifanya vichekesho kwenye sherehe ya harusi ya msanii mwenzao, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ hivi karibuni.

 

Gallery

Popular Posts

About Us