KINGAZI BLOG: 04/26/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, April 26, 2016

Chris Brown feat. Young Thug & Jeezy – ‘Wrist (Remix)’(AUDIO)


Haitham Ft. Mwana FA - Fulani (Official Video)


BARNABA - WANIFAA(AUDIO)


MAUA SAMA - SISIKII(AUDIO)


Yamoto Band & Salamu TMK (Mkubwa na Wanawe) - Dar ya Makonda (AUDIO)

Al-Shabab wavamia na kudhibiti kambi ya jeshi Somalia

 Shabab 
Wapiganaji wa al-Shabab wamekuwa wakishambulia kambi za jeshi miezi ya karibuni 
 
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab walishambulia kambi ya jeshi nchini Somalia na kuidhibiti kwa muda mapema asubuhi kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Wapiganaji hao walishambulia kambi ya Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) katika eneo la Daynuunay, wilaya ya Baidoa katika jimbo la Bay.
Taarifa zinasema magari zaidi ya kumi ya jeshi la Somalia yaliuawa wakati wa shambulio hilo.
Msafara wa wanajeshi wa Somalia kutoka mji wa Baidoa, waliokuwa wakipelekwa kuwasaidia wenzao, pia ulishambuliwa.
Taarifa zinasema kulitokea vifo na majeruhi pande zote.
Afisa mmoja wa serikali eneo hilo ameambia BBC kwamba watu zaidi ya 10 walifariki.
Mwandishi mmoja wa eneo hilo ameambia BBC kwamba wanajeshi 20 waliuawa wakati wa shambulio hilo.
Kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom) kimesema kupitia Twitter kwamba shambulio hilo lilitokea lakini kikakanusha taarifa kwamba kambi hiyo ilidhibitiwa na wapiganaji hao.
Kambi hiyo inapatikana kilomita 30 kutoka mji wa Baidoa.
Al-Shabab wamezidisha mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Amisom na Somalia tangu katikati mwa mwaka jana.
Mapema mwaka huu, walishambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya Amisom.
Al-Shabab wamesema kwamba waliua zaidi ya wanajeshi 200 katika shambulio hilo eneo la El-Ade katika jimbo la Gedo tarehe 15 Januari mwaka huu.

NewAUDIO: Nuh Mziwanda ft Alikiba ‘Jike Shupa’


TAHADHARI KUBWA!!!!!Kuna Mvua kubwa inashuka, taarifa imetolewa na mamlaka husika.


April 26 2016 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa taarifa  kwa umma ya kuwepo kwa mvua kubwa na upepo mkali, taarifa hiyo ya mamlaka ya hali ya hewa imetaja maeneo yatakayoathirika kuwa ni pamoja na Tanga, Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba ambapo mvua hizo zinatarajiwa kusambaa katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro na mashariki mwa Manyara.
IMG-20160426-WA0017

Breaking News: Rais Magufuli Aivunja Bodi ya TCRA na Kumsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hiyo Dr Ally Yahaya Simba


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Aprili, 2016

VIDEO: SNURA - CHURA(Official video)


Aliyekuwa mke wa rais wa zamani nchini Kenya Lucy Kibaki afariki dunia.


Aliyekuwa mke wa rais wa zamani nchini Kenya Lucy Kibaki amefariki. Lucy alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London. 
 
Alisafirishwa hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.
 
Akithibitisha kifo chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki.
 
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja .
 
Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hususan katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.
 
Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.
Via>>BBC

Ripoti ya CAG yaanika majipu lukuki.


MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametoa ripoti ya ukaguzi wa hesabu ya mwaka 2014/15 iliyoibua kasoro nyingi kwenye taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali huku halmashauri zikibainika kuwa na ‘madudu’ mengi.

Ripoti hiyo inaonesha kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia zina hati zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu. Kwa upande wa mashirika ambayo ripoti hiyo imeyagusa, Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limebainika mauzo ya hisa zake yalikuwa batili, hivyo CAG ameshauri lirudi chini ya usimamizi wa serikali hadi hapo mgogoro wa mgawanyo wa hisa utakapotatuliwa.

Kuhusu Wakala wa Usafiri wa Mwendo wa Haraka Dar es Salaam (DART), ripoti ya CAG imebaini kuwa kwa mwaka wa fedha 2014/15 wakala huyo aliingia mkataba na UDA-RT wa kutoa huduma ya usafiri wa mpito wa kuendesha mabasi 76 kulingana na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.

Lakini, Sheria ya Manunuzi ya Umma, mkataba huo ulitoa ongezeko la ununuzi wa mabasi na kufikia 84 ili kulingana na matakwa ya DART. Hata hivyo kwenye ukaguzi wa hesabu zao, CAG alibaini kuwepo na ununuzi wa mabasi 140 ambayo ni sawa na ongezeko la mabasi 56 yasiyo ndani ya mkataba.

Na kwamba pamoja na makosa hayo, pia ilibainika kuwa mabasi hayo yalikuwa na nembo ya UDART badala ya DART, kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba na kuiagiza DART kuendesha UDA-RT kwa kuzingatia taratibu zilizoainishwa kwenye mkataba.
Aidha, ripoti hiyo imepigilia msumari kwenye suala la watumishi hewa na kusema tatizo hilo limekuwa sugu na serikali za mitaa zinaongoza kwa kulipa mishahara watumishi waliofariki na waliotoroka huku Sh bilioni 2.7 zikiwa zimetumika mwaka wa fedha 2014/15 kwa malipo hayo.

Jambo lingine ambalo limejitokeza kwenye ripoti ya CAG, ni utoaji wa misamaha ya kodi kwa kiwango cha juu huku ikionesha Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa, zilisamehewa katika kipindi kilichoishia Juni 30, 2015.
Madudu halmashauri
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa baada ya ripoti kuwasilishwa bungeni, CAG Mussa Assad alisema wamebaini kasoro nyingi katika taasisi mbalimbali za serikali, huku udhaifu mkubwa ukiwa kwenye serikali za mitaa.
Alisema kwa mwaka unaoishia Juni 30 ,2015, jumla ya hati za ukaguzi 465 zilitolewa kwa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na mashirika ya umma. Ripoti imeonesha kuwa mashirika ya umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri kwa kupata hati nyingi safi, huku zile za mashaka zikiwa chache.

Aidha hakuna hati mbaya wala isiyoridhisha. Akifafanua alisema katika ukaguzi huo, halmashauri ndizo zinaongoza kwa kufanya vibaya . Kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia ni zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu.

“Mashirika ya umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri hakuna wenye hati isiyoridhisha au hati chafu, ila halmashauri bado kuna udhaifu mkubwa kutokana na kutokuwepo na mifumo madhubuti ya kutekeleza mapendekezo ya ukaguzi tunayoyatoa,” alisema Profesa Asaad.

Ripoti hiyo imeweka hadharani udhaifu wa Serikali za Mitaa katika kutekeleza mapendekezo ya CAG kutokana na kubainika kuwa asilimia 63 ya maagizo ya mkaguzi huyo kwa halmashauri nchini hayajatekelezwa.
Misamaha ya kodi
Wakati huo huo, akizungumzia misamaha ya kodi kwa kipindi kilichoishia Juni 30, 2015, Profesa Assad alisema ripoti yao inaonesha kuwa kiasi cha misamaha kilichotolewa ni Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa.

Kiwango hicho kwa mujibu wa Profesa Asaad, ni cha juu ikilinganishwa na lengo la serikali la kupunguza misamaha hiyo isizidi asilimia moja ya pato la taifa. Ripoti hiyo pia inabainisha uwepo wa bidhaa zilizohifadhiwa katika maghala kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi ambazo zilipewa misamaha ya kodi ya Sh bilioni 9.1 lakini hakuna ushahidi ulioonesha mauzo hayo kama kweli yalifanywa nje.

Katika misamaha hiyo, pia kuna utata kwenye mafuta yenye dhamana ya kodi ya Sh bilioni tano ambayo yalionekana kwenye mfumo wa forodha wa (TANCIS) kuwa yamesafirishwa nje kupitia nchini lakini hakuna ushahidi wa hilo.

“Sasa ukiangalia hayo na mengine utaona udhaifu mkubwa , tumeshauri serikali iweke mkazo usimamizi wa misamaha ya kodi na itolewe tu kwa mambo yanayostahili na uwepo ufuatiliaji kujua mrejesho wake, ili serikali ikusanye kodi na kujiimarisha kiuchumi”, alisema Profesa Asaad.

Deni la Taifa
Akizungumzia deni la taifa, Profesa Asaad alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka 2015, deni la taifa lilikuwa Sh trilioni 33.54. Deni la ndani lilikuwa Sh trilioni 7.99 na deni la nje likiwa Sh trilioni 25.5 hivyo jumla ya deni lote likiongezeka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na deni lililoishia Juni 30, mwaka 2014.

CAG ameshauri serikali kuongeza jitihada za ndani za kuhamasisha ukusanyaji wa mapato kujenga wigo mpana wa kulipa madeni na kuwa na mpango wa kupunguza gharama za kuongeza mikopo yenye masharti nafuu.

CAG :Deni la Taifa Lazidi Kupaa,Lafikia Shilingi Trilion 33. 5




Deni la Taifa limeongezeka kwa Sh7.05 trilioni, kutoka Sh26.49 trilioni Juni 30, 2014, hadi Sh33.54 trilioni sawa na ongezeko la asilimia 27.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad, deni la ndani ni Sh7.99 trilioni huku deni la nje likiwa ni Sh25.55 trilioni.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 26 2016 kwenye,Habari zaUdaku, Kitaifa,kimataifa na michezo.



   April 26 2016 naanza kwa kukuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa karibu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamiiyaani facebook/tanzaniampyasasablog na twitter@tanzaniampyasasa  ;

Lady Jaydee: Sijawahi kuwa na uhusiano na msanii




Lady Jaydee ameweka bayana kwamba hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote.
Jaydee1-e1430308550256
Alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV wakati akizindua video ya wimbo wa ‘Ndindindi.

TAKUKURU Yaanza Kuchunguza "Mabilioni ya JK"





Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima.

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli alisema jana kuwa taasisi hiyo imechukua jukumu hilo kwa sababu moja ya majukumu yake ni kuchunguza masuala ya rushwa na kutoa rai kwa mtu mwenye ushahidi au taarifa kuhusu suala hilo kuzitoa kwa taasisi hiyo.


“Takukuru ipo wazi kuzipokea taarifa hizo ili zitusaidie kwenye uchunguzi,” alisema Tunu.


Kati ya Sh50 bilioni zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni Sh43 bilioni tu zilizorejeshwa, huku Sh7 bilioni zikidaiwa kutafunwa.


Fedha hizo zilitolewa na Kikwete kwa ajili ya kuwawezesha kimitaji, wajasiriamali nchi nzima, mikopo ambayo ilipitia benki za CRDB, NMB, Community Bank na Benki ya Posta Tanzania.

Fedha hizo kutoka Mfuko wa Rais, zilikuwa zikikopeshwa kwa riba ya asilimia 10, ambapo asilimia mbili ilikuwa inaingia serikalini na nane ilikuwa inabaki kwenye benki hizo.


Hata hivyo, baadhi ya vyama vya Akiba vya Kuweka na Kukopa (Saccos), vilivyopewa fedha hizo, vilitoa mikopo hiyo kiholela, huku baadhi ya viongozi wakidaiwa kutengeneza majina feki na kukopeshana fedha hizo.


Imedaiwa kuwa Saccos nyingi ambazo zilifuja fedha hizo katika mikoa mbalimbali, viongozi wake wengi walikuwa pia ni viongozi wa kisiasa na wengine wakiwa na nyadhifa serikalini.


Kwa mujibu wa uchunguzi huo, baadhi ya waliokopeshwa fedha hizo na Saccos mbalimbali, hawakuwa wanachama, bali walichomekwa baada ya kuonekana kuna fursa ya ‘kupiga dili’.


Chanzo kutoka Takukuru, kimedokeza kuwa makamanda wa taasisi hiyo katika mikoa mbalimbali, wamepewa maelekezo ya kuchunguza mahali yalipo mabilioni hayo na nani waliyafuja.


“Ni kweli tumepewa maelekezo ya kuchunguza fedha hizo. Unajua hizi ni fedha za umma haziwezi kutafunwa tu hivihivi na Serikali ikakaa kimya,” alidokeza mmoja wa maofisa wa Takukuru.

Machi mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Christopher Chiza aliagiza kufanyika kwa ukaguzi wa kina wa fedha hizo.


Alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (Neec), ambako aliagiza watakaobanika kuhusika na ubadhirifu wa fedha hizo wachukuliwe hatua za kisheria.


“Lazima tuangalie mabilioni ya JK yalipotelea wapi, yalivyofujwa na wahusika wapo wapi ili sheria ichukue mkondo wake. Nimeambiwa kuna zilizobaki tujue ziko wapi,” alikaririwa Chiza akisema.

Lakini Desemba 24, 2013, mtangulizi wa Chiza, Mary Nagu alikaririwa akisema Sh43 bilioni kati ya Sh50 bilioni za mabilioni ya JK zilizokopeshwa kwa wajasiriamali 74,701 zilikuwa zimerejeshwa.


Nagu alitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya Serikali ya Rais Kikwete katika, utaratibu uliofanywa pia na wizara nyingine.

Suala la mabilioni hayo ya JK limekuwa likiibuka mara kwa mara bungeni na katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku wananchi wakitaka zirejeshwe.

Gigy Money Aopoa Kigogo wa Madini..Mwenyewe Adai Wameshibana


Kazi ipo! Video Queen asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kuopoa kigogo ambaye ni mfanyabiashara wa madini, mkazi wa jijini Arusha ambaye ndiye mwandani wake anayempa jeuri kwa sasa.

‘Ubuyu’ kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mwanadada huyo unatonya kuwa, licha ya ‘umapepe’ wa Gigy ambaye kwa sasa safari za Dar na Arusha hazikauki, ukweli ni kwamba jamaa huyo hapindui kwake.

Ili kupata mzani wa ubuyu huo, Over Ze Weekend lilimsaka Gigy, alipopatikana kwa njia ya kilongalonga alikiri kuwa na kigogo huyo na kudai kwamba wameshibana sana.

Breaking News :Rais Magufuli Ateua Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania majina haya hapa>>



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

KUWA MAKINI SANA!!!!! Aina Mpya ya Uwizi wa Magari Dar es Salaam...Soma Hapa



Gari imeibiwa jana , 23/4/2016 Shopper plaza- Mikocheni, mida ya saa 9 mchana.Ni Volkswagen Tourge, Blue color... Kama umeiona au unajua ilipo au unajua chochote tafadhali piga number hii ‪+255 715 066 278‬ au toa ripoti polisi.
.
Hii story ntaiandika in full ili na wengine muwe makini mnapokuwa mnauza magari. Dada alieibiwa alitaka kushare ili isije kumtokea mtu mwingine. Na tafadhali kama unajua lolote kuhusu hili gari pls piga 0715 066 278‬
.
Story iko Hivi. Gari ilipostiwa www.kupatana.com . Jumamosi akapigiwa simu na muhindi Kuwa kaipendaKufika muhindi akampigia akasema yuko busy Ila Fundi wake ataangalia gari, basi Fundi akafika akaangalia gari akaongea na muhindi akaondoka. Baadae accountant akampigia wakutane waangalie contract. Accountant kufika akatoa mkataba feki then akamuuliza Fundi si alitest drive gari? Akasema Hapana aliangalia tu. Basi akajifanya kupanick Yani hajatest drive ?akampigia muhindi, muhindi akampigia huyo dada anajifanya kahamaki Fundi wake haki test drive wakati yeye anajua VW zina Tatizo la shock up . Basi wakapanga wakutane Kesho yake ambayo ndo jana Kwa ajili ya kutes5 drive na kulipana kabisa.
.
Kesho yake dada wa watu akaenda shoppers plaza. Accountant akaja wakaingia wote kwenye gari wakadrive kidogo. Basi wakapaki accountant akamrudishia dada funguo yake wakashuka, akamwambia muhindi nae keshafika shoppers anataka aone mwenyewe so yeye anaenda kumtafuta upande wa pili wa shoppers then anakuja nae so awasubiri pale juu Art Cafe. . Dada wa watu akawa amekaa anawasubiri. Kasubiri mpaka kachokaaaaaa, jamaa hajarudi. Kuchungulia chini gari yake haipo.
.
.
Sasa unajua kaibiwaje?siku ya kwanza Fundi wa gari alipokuja alikuwa kaja kuangalia funguo wa gari ukoje. Wakaenda kutengeneza similiar looking key. So siku alipoibiwa jamaa alivyosema anataka kutest drive gari ni kwamba alitaka tu funguo ya gari. Then akamrudishia funguo fake ambayo imefanana na yake, Then wao wakabaki na original
.
.
Number aliokuwa anatumia muhindi ni 069 271 3707 na imesajiliwa TIGo Kwa Jina la Aleej Khimji. Number ya accountant ambae ndo aliiba gari alisema anaitwa Omar ni +255 715 936 985 na number ya Fundi aliejiita Joseph ni +255 715 937 547

VIDEO:Maswali na majibu bungeni leo, ishu ya wafanyakazi wa viwanda imemsimamisha Waziri


April 25 2016 Bunge la 11 mkutano wa tatu limeendelea, na Waziri wa Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage alikuwa akijibu maswali ya wabunge.
 

Gallery

Popular Posts

About Us