KINGAZI BLOG: 07/17/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, July 17, 2016

Mtoto aliyewekewa ‘mashine’ kwenye moyo aanza mazoezi

Mtoto Happiness John Mkazi wa Seliani Arusha aliyefanyiwa upasuaji kwenye moyo na kupandikiziwa kifaa cha kusaidia kudhibiti mapigo ya moyo (pacemaker), ameanza mazoezi. 

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Sulender Kuboja aliyeshiriki upasuaji huyo alisema jana kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na wameanza kumfanyia mazoezi mepesi. 

Dk Kuboja alisema kwa kawaida mgonjwa yeyote aliyefanyiwa upasuaji anapaswa kufanyiwa mazoezi mepesi na kwamba kwa mtoto, mazoezi anayofanyiwa ni ya kukaa, kusimama na kutembea kidogo. 

“Hali yake inaonekana kuendelea vizuri sana... nimetoka kumfanyia vipimo muda mfupi uliopita kifaa kile kinafanya kazi vizuri na maendeleo yake yanaridhisha sana,” alisema Dk Kuboja. 

Alisema mtoto huyo anaweza kuongea na hata kula chaku- la, hali aliyosema inaonyesha nafuu nzuri kwake. 

Mama mzazi wa mtoto huyo, Elitruda Malley alisema anaridhishwa na maendeleo ya afya ya mwanaye kwa kuwa tangu afanyiwe upasuaji huo juzi, hali yake imeonekana kuimarika kwa haraka. 

Mama huyo alisema tangu awekewe kifaa hicho, mwanaye amekuwa mchangamfu, hali aliyosema inamtia moyo na kumpa matumaini makubwa. 

“Ingawa yupo kwenye oxygen, lakini namshukuru Mungu kwani anaonekana anapata nafuu nzuri, anatabasamu na kuongea vizuri kabisa na ana furaha sana, shauku yake ni apone ili aende shule kama watoto wengine,” alisema Malley. 

 Aliongeza kuwa mtoto huyo amekuwa akila vizuri na kumpa moyo kwani mwili wake unaonekana kuwa na nguvu na afya nzuri. 

Madaktari wapo karibu wakifuatilia afya ya mtoto kwa ukaribu, wanampa chakula, wanamfanyia mazoezi ya kukaa na kushuka chini, anaonekana kuwa na nguvu na mwenye maendeleo mazuri. "

Alisema jambo linalompa faraja ni kuona jinsi madaktari wote wanaomuhudumia mtoto huyo wanavyofanya kazi hiyo kwa upendo na bidii. 

Juzi, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ilifanikiwa kumpandikiza mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano kifaa cha kusaidia kudhibiti mapigo ya moyo (pacemaker) kinachoendeshwa kwa betri. 

Hayo ni mafanikio ya pili kwa taasisi hiyo ya kisasa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya Mei 24 na 25, mwaka huu kufanikisha operesheni kwa wagonjwa 18 bila kuusimamisha moyo.

Tume ya vyuo vikuu(TCU) yatoa ufafanuzi kuhusu alama za kudahiliwa vyuoni

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi kwa kukosa sifa na vigezo.

Utaratibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Sifa hizo ziliwekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa jana. Taarifa hiyo inaonyesha kutolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Eliuta Mwageni.

Akizungumza na  mwandishi wetukwa njia ya simu jana, Ofisa Habari Mwandamizi wa TCU, Edward Mkaku, alithibitisha taarifa ya utaratibu huo mpya.

Mkaku alisema utaratibu huo umetolewa baada ya mwaka jana kutumika mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ambao Januari, mwaka huu, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, aliagiza ufutwe na kurudishwa ule wa madaraja (division) uliotumika siku zote.

“Mfumo wa udahili uliotumika mwaka jana ulikuwa ni GPA na mwaka huu utatumika mfumo wa divisheni, ndiyo maana utaratibu huo ukawekwa,”alisema Mkaku.

Moja ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo (2016/2017), ni wahitimu wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa (D mbili) pointi 4.0.

Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokana na ufaulu wa A = 5; B= 4; C= 3; D = 2; E = 1.

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa ili wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 wawe na sifa za kudahiliwa, watatakiwa kuwa na alama za ufaulu wa (C mbili ) pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1.

Pia tovuti hiyo ilionyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu, watahitajika kuwa na ufaulu wa alama (D mbili) 4.0 kupitia mchanganuo wa A = 5; B = 4; C= 3; D= 2; E = 1.

Mbali na sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa  na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne za D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A =75-100, B+ = 65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F= 0-38.

Sifa nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama nne za D za kidato cha nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) au Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Pia watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada (NTA) daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi (FTC) katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu, au wastani wa daraja la B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.

Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA.

Pamoja na hayo, TCU ilisema hakutakuwa na usajili wa mafunzo ya awali pamoja na yale ya UQF6 yaliyozuiwa kuanzia mwaka wa masomo wa 2016/2017.

Taarifa ya tovuti hiyo iliendelea kusema kuwa maombi yote ya usajili wa wanafunzi hao wanaotaka kuchukua shahada yanatakiwa kupitia TCU pekee.

“Kwamba tume hiyo imeamua kuwa kuanzia mwaka 2016/2017, maombi yote ya usajili kwa makundi yote yanayoanzia aya ya 3.0 kwenda juu wataunganishwa na TCU pekee na walio chini ya hapo hawatahusika na tume hiyo,” ilisema taarifa hiyo.

Pia TCU ilisema taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kipengele cha 5(1)(c)(i) cha katiba ya vyuo vikuu, kifungu cha 346 cha sheria nchini.

“Msingi wa kubadili viwango vya kujiunga na elimu ya juu ni kutokana na kuwepo maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya uwezo wa wahitimu wanaojiunga na vyuo vikuu mbalimbali,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mei, mwaka huu, Profesa Ndalichako aliwasimamisha kazi Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, kwa kushindwa kuisimamia tume hiyo kutokana na kuwapo kwa wanafunzi wasiokuwa na sifa, kisha wakadahiliwa katika vyuo vikuu na kupata mkopo.

Wengine aliowasimamisha kazi ni Mkurugenzi wa Ithibati na Udhibiti Ubora, Dk. Savinus Maronga, Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka, Rose Kiishweko na Ofi sa Msimamizi Mkuu wa Taarifa, Kimboka Stambuli.

Pia Mei mwaka huu, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idrisa Kikula, alitangaza kuwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya stashahada ya ualimu ambao hawakuwa na sifa.

Alipozungumzia sakata hilo Juni, mwaka huu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Dk. John Magufuli, aliwaita wanafunzi hao kuwa ni vilaza, na kwamba idadi kubwa ya waliofukuzwa hawakuwa na sifa stahiki za  kudahiliwa kusoma kozi hiyo.

UTAFITI:WANAUME WANAPENDA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA

Je wajua kwanini wanaume wanawapenda wanawake waliojaliwa na makalio makubwa ?
Katika majarida mengi umewaon wanaume wakikodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni kim Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj na Vera Sidika kutoka Kenya .Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.Kulingana na utafiti wa chuo kikuu Bilkent , chuo kikuu cha Texas, na chuo kikuu cha American University kilichoko mjini BeirutWanaume wanakisia kuwa mwanamke mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke ambaye hana makalio makubwa.Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.

Utafiti huo unasema kuwa upinde wa 45.5 ndio unaovutia wanaume zaidi.
Wanaume walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake wenye makalio yaliyopinda kwa kiwango cha 45.5Aidha zaidi ya asilimia 30% walisema wangalimchukua mwanamke mwenye makalio makubwa zaidi ya yule waliye naye sasa.Kwa mujibu wa utafiti huo katika miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni.
Isitoshe mwanamke kama huyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.
Aidha mwanamke mwenye makalio makubwa angeweza kustahili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata kustahilimi makali ya uzazi kuliko wale wenye makalio wastani.
BBC

BASATA WATOA TAMKO KALI KWA MASTAA WALIOTOA BEI ZA KUJIUZA  


DAR ES SALAAM: Wakati serikali ikitangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara ya ngono, ripoti mpya iliyokusanywa inaonesha viwango vya fedha vinavyolipwa na wahitaji ili kuweza kupata huduma hiyo kutoka kwa mastaa wa fani mbalimbali nchini.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba mastaa hao wa Bongo Fleva na filamu ambao wamekuwa wakijiuza kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Instagram na mingine, ambako huweka picha zao zinazoonesha pozi mbalimbali, wanaweka bayana jinsi walivyo tayari kushiriki tendo na mwanaume wasiyemfahamu, ilimradi mifuko yao imetuna.

“Unajua kutokana na maisha magumu, mastaa wetu wanajilipua kabisa, wanataja waziwazi kiasi wanachotaka wapewe, sema ndiyo wengine wanachukua mkwanja mrefu na wengine hela mbuzi tu, sanaa hailipi ndiyo maana wapo tayari kujiachia,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilidokeza majina kadhaa ya mastaa hao walio tayari kujitoa kwa yeyote mwenye fedha za kutosha ambazo zitamhakikishia maisha bora, ingawa baadhi ya mastaa waliotajwa, waliruka kimanga kujihusisha na mchezo huo unaokiuka maadili ya Kitanzania.

GIFT STANFORD ‘GIGY MONEY’

Video Queen huyu aliyeuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, alisema hali ya maisha inamlazimu kuwa tayari kukabiliana na mazingira yoyote ili mradi mambo yake yanaenda ‘supa’ hivyo hana kinyongo kama mwanaume yeyote,  awe ni wa kwenye mitandao au barabarani, atakayempatia kiasi cha shilingi milioni tatu.

GLASNOST KALINGA ‘GILLA’

Chipukizi huyo anayefanya vizuri kwa sasa katika filamu, naye alijianika wazi kuwa yupo tayari kuangukia mikononi mwa mtu kwa kiasi cha shilingi milioni mbili unusu hadi tano, kwani kama suala ni kupatwa na magonjwa, binadamu wote ni lazima watakufa.



ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’

Staa huyu wa filamu Bongo alisema hawezi kujiuza kwa njia yoyote ile kwani kitendo chake cha kuweka picha zake za aina mbalimbali katika mitandao ni kwa ajili ya kujifurahisha na pia mashabiki wake.

“Huwa napigiwa simu sana, unakuta nyingine napokea nikisikia mtu anachoongea ni ujinga namkatia na sipokei tena hata akiendelea kupiga.”

 ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’

FATUMA AYUBU ‘BOZI’

Bozi naye alisema; “Kama jamaa akija na shilingi milioni kumi niko tayari lakini hata hivyo itategemea na afya ya huyo mtu maana siko tayari kufa kwa milioni kumi.”

TIKO HASSAN

“Sijawahi kufikiria kujiuza wala kujaribu, lakini kama kuna wanaojiuza na kuona ina masilahi, basi waendelee ila ina madhara makubwa sana katika maisha yao, kwani kama wamekutana kwenye mitandao ya kijamii wanaenda kuwa na mtu wasiyemfahamu vizuri au hata kama ni barabarani mmekutana bado ni hatari pia.”

ESTER KIAMA

“Kiukweli sijawahi kujiuza na sina mpango kwa sababu nina mwanaume wangu anayeniridhisha kwa kila kitu, mimi sitaki fedha, ila nataka mapenzi na tayari mlango huo nishaufunga hata aje nani na fedha zake siwezi kujiuza.”

Ester Kiama akiwa katika pozi.

ISABELA MPANDA

“Sijawahi kujiuza na nimekuwa nikiweka picha za kuacha mwili wangu wazi kwenye mitandao kwa sababu kazi yangu inaruhusu, wapo wanaume wanaingia kingi na kunitafuta, lakini nimekuwa nikiwachuna tu, hawajawahi kufanikiwa kuwa nami kimapenzi.

“Kwa siku huwa nawachuna hata watu sita, wakishatuma fedha zao nawa-block na wale ninaowabakiza wananimwagia mitusi tu, lakini ndiyo hivyo nakuwa nimeshakula fedha zao tayari.”

MWAKIFWAMBA ANASEMAJE?

Paparazi wetu alimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba na kumwelezea hali hiyo ambapo alisema hakuwahi kujua kama wapo baadhi ya wasanii wanaojiuza na kuanika wazi kiasi cha malipo wanayotoza.

Kutokana na sababu hiyo, alisema shirikisho lake litayafanyia kazi maelezo hayo na litakapojiridhisha, hatua muafaka zitachululiwa.

“Ngoja nitalifanyia kazi, maana siwezi kutoa maamuzi peke yangu, nitakaa na bodi na kujiridhisha kwamba ni kweli hapo ndipo tutajua la kufanya.”

SERIKALI YAJIPANGA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa ‘Basata’, Godfrey Mngereza alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo, alisema aachiwe muda ili akishajiridhisha ndipo atakapolifanyia kazi.

“Siwezi kuzungumza kitu ambacho sijakiona au ambacho sina ushahidi nacho, naomba muda nikishajiridhisha ndipo nitakapotoa ufafanuzi,” alisema Mngereza.

KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI

Ni kweli kwamba hali ya maisha ni ngumu, lakini ni jambo la hatari kwa mtu kuishi kwa kutegemea kuuza mwili wake, kwani licha ya hatari ya kiafya, pia jambo hilo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.

Maisha mazuri yanaweza kupatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na ubunifu. Tunaishauri serikali kupitia vyombo vyake, kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayepatikana akiufanya biashara mwili wake.

IMEANDIKWA NA: Gabriel Ng’osha, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya - GPL

VIDEO YA "KIDOGO" YA Diamond Platnumz YAFIKISHA WATAZAMAJI ZAIDI YA MILLIONI 1.

Diamond Platnumz ameendelea mkushika hisia za watu baada ya kuendelea kuongeza idadi ya watazamaji wa video ya wimbo wake mpya wa KIDOGO aliowashirikisha  PSQUARE  hatimaye imefikisha watazamaji millioni moja kwa siku nne pekee.

Video ya wimbo huo imetoka katika kipindi ambacho kundi la P-Square bado halina maelewano mazuri.kama hukuiona video ni hii hapa chini.bofya kuona

BREAKING NEWS:PICHA 3 !!!!AJALI ENEO LA MIKUMI LEO

LORI LIKIWA LIMEACHA NJIA NA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA HIFADHI YA MBUGA YA MIKUMI LEO JUMAPILI TAR 17 JULAI MPAKA SASA BADO TUNAENDELEA KUFUATILIA CHANZO NA TAARIFA TUTAENDELEA KUKUJULISHA



BONYEZA HAPA KUONA MATOKEO YA ACSEE KIDATO CHA SITA,UALIMU(DSEE NA GATCE ) 2016>>>>>>>PDF

VIDEO:DARASA --Too Much | Watch/Download

 

Gallery

Popular Posts

About Us