Thursday, March 24, 2016
9, wajitosa uspika Zanzibar.
Published Under
ZANZIBAR
VITA ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imepamba moto, huku mchuano mkali ukionekana kuwa kati ya Spika aliyemaliza muda wake, Pandu Ameir Kificho,
SHARE!
Wabunge wahojiwa Takukuru
Published Under
KITAIFA
*Asema vyombo vya dola kufanya uchunguzi
*Kamati iliyosusa yaendelea na vikao Dar
SIKU moja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, kupangua wenyeviti na makamu wenyeviti kwa kuwaondoa kwenye kamati walizokuwa wanaziongoza, hatimaye Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), imewahoji wabunge watatu ambao wanatajwa kuhusika na mgawo wa fedha.
SHARE!
Askari wanaswa wakiiba mafuta ya ndege
Published Under
MATUKIO
VITA ya kutumbua majipu kwa watumishi wa Serikali wasiokuwa waaminifu imeendelea kushika kasi, baada ya jana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni kuagiza kusimamishwa kazi mara moja askari watatu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa tuhuma za wizi wa mafuta ya ndege na mizigo ya abiria.
SHARE!
Mwili wa Sarah Dumba kuletwa Dar leo
Published Under
TANZIA
Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi alisema, ibada ya kumuaga rasmi ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lililopo mkoani humo.
“Tumemuaga na safari ya kwenda Dar es Salaam itaanza muda mfupi kuanzia sasa (jana jioni), tutasafiri usiku mzima tunatarajia kuingia Dar es Salaam kesho (leo) asubuhi tayari kwa mazishi,” alisema Dk Nchimbi.
Kwa mujibu wa taarifa ya ndani ya familia, mwili wa Dumba unatarajiwa kuwasili saa 4:00 asubuhi na taratibu za mazishi zitafanywa nyumbani kwa baba yake, Mzee Dumba eneo la Kigamboni Midizini.
Baada ya chakula itafanyika ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Magogoni lililopo Kigamboni na maziko yatafanyika kwenye makaburi ya Magogoni. Wakati huo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa wanahabari wote kutokana na kifo cha ghafla cha mkuu huyo wa wilaya ambaye pia alikuwa ni Mtangazaji Mwandamizi wa zamani wa Redio Tanzania (RTD), Dar es Salaam.
“Pokeeni salamu zangu za rambirambi za dhati kwa kuondokewa na mwanahabari mahiri Dumba aliyekuwa mfano wa kuigwa. Mbali na utangazaji wake mahiri, alikuwa mzalendo wa kweli aliyetumikia tasnia hii ya Habari na Serikali kwa uadilifu na upendo wa kweli, tutamkumbuka na tutaukosa mchango wake,” alisema Nape.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante ole Gabriel alituma salamu za pole na kuwatakia moyo wa subira na uvumilivu ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu. Baadhi ya wafanyakazi waliowahi kufanya kazi naye walisema, kifo chake ni pigo na pengo lisiloweza kuzibika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba akizungumzia uhusiano wake na Dumba, alisema yeye alianza kazi RTD mwaka 1971 na kumkuta Dumba akiwa tayari kazini hivyo walifanya naye kazi kwenye Idhaa ya Kiingereza ya External Services wakati Dumba akiwa msaidizi wake.
SHARE!
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS YA TAR 24 MARCH 2016 KWENYE HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA UDAKU NA MICHEZO PIA STORI NYINGINE KALI.
Published Under
MAGAZETINI LEO
SHARE!
Subscribe to:
Posts (Atom)