KINGAZI BLOG: 07/18/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, July 18, 2016

Rais Magufuli aibua ufisadi mwingine wa mabilioni ya shilingi ndani ya Jeshi la Polisi

Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika jamii huku akisema kuwa ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya kifisadi ya mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna hata sare moja ya iliyonuuliwa.

Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo hakuna hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko bandarini.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe mbele ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.

Amelitaka pia Jeshi la Polisi kuachana na utaratibu wa kuwa na watumishi ambao ni raia wa kawaida na badala yake polisi wenyewe ndio washike nafasi hizo kulingana na taaluma husika na kushangazwa na taarifa kuwa  Mhasibu Mkuu wa Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za ubadhirifu alikuwa raia wa kawaida na sio polisi.

Wema, Idris wamwagana rasmi


Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan

UBUYU: Waandishi Wetu, Wikienda

 DAR ES SALAAM: Ubuyu wa motomoto wa mjini ni kwamba, zile mbwembwe zote za penzi la mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan, zinadaiwa kufikia ukingoni na sasa imebaki stori kwani Wema, Idris wamwagana rasmi.


Wikienda limeng’atwa sikio kuwa, kitendo cha wawili hao ‘kushoo lavu’ kwenye ile Pati ya Black Tie iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa King Solomoni pale Namanga, Dar ilikuwa ni geresha tupu kwani walishamwagana kitambo.

Hata hivyo, kama utakumbuka au hukuipata ni kwamba iliwahi kuvujishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema na Idris wamemwagana lakini baadaye zilivunjwa picha zikiwaonesha wakiwa wameshikana mikono na mahaba tele ili kuua soo.


Sasa ubuyu ulionyooka kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao unadai kwamba, kilichotokea kwenye pati hiyo zilikuwa ni mbwembe za kuzuga zilizotokana na

 huruma ya Idris.

Ilidaiwa kwamba, Idris alilazimika kufika kwenye sherehe hiyo kwa sababu ilishatangazwa kuwa atakuwa ni miongoni mwa ‘ma-hosti’ lakini ukweli ni kwamba mambo yalishaharibika.


“Unajua watu wengi hawakujua kuwa Wema na Idris walishaachana kitambo na pale (King Solomoni) walikuwa wanafanya maigizo tu, japokuwa haijulikani moja kwa moja sababu ya kuachana kwao lakini Wema anadaiwa kuwa tatizo kwa Idris kutokana na kutokea kwa migogoro ya kila kukicha,” alitonya sosi huyo.

Hata hivyo, katika kuonesha kwamba kuna kitu kinaendelea, wana-ubuyu wetu walifuatilia akaunti zote za mastaa hao katika mitandao ya kijamii kuona kama mbwembwe zao zinaendelea na kubaini kuwa hawako sawa baada ya kusoma ujumbe wa Wema unaoonesha kumbembeleza Idris huku jamaa huyo akionesha wazi kuwa hakuna mapenzi bali ni drama tu.

Ili kuleta ushahidi, tunakukaribisha hapa kusoma nukuu zao mtandaoni;

MANENO YA WEMA

“Having you as a friend, a brother, a lover and of course a shoulder to cry on every time, i’m at my worst has been the best feeling ever… I wouldn’t want to lose this feeling over anything…

“I realized without u

 then i ain’t complete…. You have stood by me in good times and bad and even when i messed up so bad you would look me in the eyes and tell me, “Baby, its okay, we gona fix this”…

“Idris you have been one of a kind and losing u is the last thing i want on this earth… I will love you until forever, until death do us part we will be together…

“I will hold on to you till da last minute because together we will get there…. I love you with my life…. For I believe you are my true love, my baby and inshallah! The Man that my kids will call daddy…” alimalizia kuandika Wema akimlilia Idris.

IDRIS NAYE ALIANDIKA:

“Kumbuka kurekebisha kiatu kila hatua ya maisha unayopiga kisije kuchomoka ukakanyaga mwiba ukapunguza spidi.”

WEMA ASAKWA

Wikienda halikuishia hapo kwani lilimsaka Wema anayedaiwa kubwagwa, alipopigiwa simu hakupokea, akaandikiwa ujumbe mfupi wa sms ambao pia hakuujibu.

Pia alitumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini pia hakujibu.

 UBUYU WAKAMILIKA KWA IDRIS MWENYEWE

Wikienda liligeuza dira yake na kuielekeza kwa Idris ambaye alifunguka bila kuacha lolote.

Kwa mujibu wa Idris, yeye na Wema walishasahau kuwa waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwani kwa sasa kila mtu ana ‘biashara’ zake.

“Mimi nilikwenda kwenye ile pati kwa sababu ya kuwaonea huruma tu kwani ndiyo kwanza wameanzisha kampuni na mbaya zaidi walikuwa wakiniweka kwenye matangazo. Unadhani watu wangewachukuliaje? Sikutaka kuwaharibia shoo lakini mimi nilishaachana naye na nina biashara zangu nyingine,” alifunguka Idris.

Idris alienda mbali zaidi na kusema kuwa kwa sasa ana mwanamke mwingine anayempenda na siku si nyingi mambo yakikaa sawa, atamuanika.

“Mwenzenu nina kifaa kingine soon nitawafahamisha,” alisema Idris.

WEMA NA IDRIS

Awali Wema na Idris walificha uhusiano wao lakini baadaye waliamua kujiachia ambapo mlimbwende huyo alidai kushika ujauzito lakini kwa bahati mbaya ukachoropoka.

Askofu Gwajima Aibuka kanisani kwake.


KIONGOZI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, amefunguka kwa kuelezea safari yake aliyoifanya nje ya nchi hivi karibuni, baada ya taarifa mbalimbali kudai kuwa alilikimbia Jeshi la Polisi.

Akiongoza ibada kanisani kwake, Ubungo, jijini Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema aliondoka nchini kwenda Japan Juni 15, mwaka huu, kwa ndege ya Emirates.

Akitoa mahubiri katika ibada jana, Gwajima alisema alifika mjini Osaka Juni 16 na kuanza mkutano wa kuhubiri injili na siku zilizofuata alikwenda katika miji mbalimbali.

Askofu Gwajima ambaye aliingia kanisani hapo saa 5:00 asubuhi na kuanza kuhubiri dakika 15 baadaye, asubuhi alitumia muda wa saa tatu hadi saa 8:20 kumaliza mahubiri yake.

Baada ya kuanza kuhubiri, alielezea safari hiyo kwa kutaja miji aliyekwenda ikiwamo Nagoya alikohubiri kwa siku mbili, Karuizawa, Ibaraki, Hiloshima na Yanakochi.

“Safari yangu ilikuwa ya mafanikio sana. Tulisafiri salama na kuzunguka miji mbalimbali na tulirudi Jumatatu ya wiki iliyopita,” alisema Askofu Gwajima.

Kadhalika, katika mahubiri hayo, Gwajima aliwakumbusha waumini wa kanisa hilo kuhusu kuhama kwa kanisa hilo, kwa kuwatajia siku ya mwisho ya kumalizia michango kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya kuwa ni Julai 30, bila ya kutaja sehemu ambayo kanisa hilo litahamia.

Hata hivyo, Askofu Gwajima wakati wote wa mahubiri, hakuzungumzia suala la kuhojiwa kwake na Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, mwandishi alizungumza na Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kuhusu tetesi za kufungiwa kwa kanisa hilo na kusema taarifa hizo si za kweli bali ni maneno ya mitaani.

“Hayo maneno si ya kweli. Si umeona ibada imeendelea kama kawaida na Askofu amehubiri? Maneno ya mtaani usiyalete kanisani,” alisema Bihagaze.

Julai 12, mwaka huu, Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kilimkamata Askofu Gwajima wakati akitokea Japan kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.

Baada ya kukamatwa, alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa, akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.

Jeshi la Polisi lilikuwa likimtafuta Askofu Gwajima baada ya kusambazwa mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake.

Katika mkanda huo, Gwajima anapendekeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake, ambayo kwa sasa Rais Magufuli anayashughulika kwa staili ya utumbuaji majipu.

Pia Gwajima alisikika akimshauri Rais John Magufuli, kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwapo watakataa kumkabidhi uenyekiti na kwamba apeleke muswada bungeni, kuondoa kinga ili rais ashtakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

Tangu kusambaa kwa mkanda huo, Jeshi la Polisi lilikuwa likipiga kambi katika moja ya nyumba za Askofu Gwajima, iliyoko Mbezi Salasala jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kupiga kambi, jeshi hilo halikufanikiwa kumkamata na baadaye ilielezwa kuwa amekwenda nje ya nchi kuhubiri.MUUNGWANA

AJIRA!! Nafasi ya kazi Synarge Group of Companies mwisho 20 Aug 2016


Job Vacancy >Godown/Stores Assistant Supervisor
Location > Dar Es Salaam 
Position Type > Full Time 
Organization Type >Company

Application Deadline: 20 Aug 2016

GODOWN/STORES ASSISTANT SUPERVISOR POSITION DESCRIPTION:

Position Description Document (download) 

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Please e-mail your CV & certificates via APPLY NOW below for further consideration.

IF YOU ARE QUALIFIED FOR THIS POSITION

 Apply Now

 report abuse or errors

AVOID SCAMS: NEVER pay to have your CV / Application pushed forward. 
Any job vacancy requesting payment for any reason is a SCAM. If you are requested to make a payment for any reason, please use the Report Abuse, or call +255 768 982 800 to report the scam. 

EPUKA UTAPELI. Kazi yoyote inayopendekeza malipo ya aina yoyote ukiwa unaomba kazi, sio halali. Ukiombwa kulipia chochote kile wakati wa kuomba kazi, tafadhali toa ripoti Report Abuse au piga +255 768 982 800 kututaarifu.

NISHA AELEZA MAJUNGU NA WIVU VILIVYOMTENGA NA MARAFIKI ZAKE


 

Stori: Hamida Hassan, Wikiend
DAR ES SALAAM: Staa wa sinema za vichekesho Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka sababu za yeye kutokuwa na marafiki wa kike kuwa ni majungu na wivu tofauti na marafiki wa kiume.
Nisha ameliambia Wikienda kuwa, watu wengi wamekuwa wakimuuliza sababu ya kuwa na marafiki wa kiume pekee na siyo wa kike ambapo amekuwa akiwajibu kuwa si kwamba hakuwahi kuwa nao lakini aliachana nao kwa sababu wanawake wengi hawawapendi wenzao kwani wakiona wanafanikiwa huwa wanaumia.“Niliyoyapitia kwa marafiki wa kike ni tofauti na wa kiume, wa kike wana wivu na majungu mengi, mtu ukimpita kidogo tu kimaendeleo anakuwa na chuki tofauti na wanaume,” alisema Nisha.
Nisha aliweka wazi kuwa marafiki wa kiume ni muongozo mzuri kwa sababu ukishuka wanakuongoza na ukiwa nacho bado mnasaidiana tofauti na baadhi ya wanawake.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 18 KWENYE HEADLINES ZA UDAKU,KITAIFA,KIMATAIFA MICHEZO.

U

 

Gallery

Popular Posts

About Us