KINGAZI BLOG: 07/01/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, July 01, 2016

RAIS KAGAME AWASILI NCHINI-APOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Rwanda Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame.PICHA KWA HISANI YA IKULU NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Kodi ya Miamala ya Tigopesa, M-Pesa, Benki na Airtel Money Kuanza Kutozwa Rasmi Leo Julai Mosi


Leo ndiyo mwanzo wa utekelezaji wa Sheria Fedha (Finance Act, 2016) iliyopitishwa katika Bajeti ya 2016/17 ambapo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) itatozwa katika huduma za mitandao ya simu, benki na taasisi za fedha.
Akisoma hotuba ya bajeti bungeni hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango pamoja na mambo mengine, alipendekeza kuongeza kodi hiyo katika huduma za kibenki zinazotozwa na benki hizo ili kupanua wigo wa kodi isipokuwa riba kwenye mikopo.
Vilevile, Waziri Mpango alieleza azma ya Serikali kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma katika kutuma na kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye kutuma fedha pekee.
Akizungumzia uamuzi huo, mtaalamu wa kodi wa kujitegemea, Deogratias Peter alisema ongezeko hilo litawakatisha tamaa wateja wa benki na watumiaji wa miamala ya simu.
“Kwa zaidi ya miaka 10 sasa, Serikali inafanya jitihada za kuongeza watumiaji wa benki kwani katika nchi za Afrika Mashariki ilikuwa nchi ya nne mbele ya Burundi kwa kuwa na idadi ndogo ya watu wanaotumia benki. Lakini hatua hii inaweza kurudisha nyuma jitihada hizo,” alisema Peter.

Alisema Serikali ilianzisha utaratibu wa Saccos, Vicoba na kulegeza masharti ya kuwa na akaunti ya benki ili kuwawezesha wananchi wa kawaida kumudu kuweka fedha kwenye taasisi za fedha na ilianzisha Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), wakala wa benki na miamala ya simu ili kuongeza watumiaji wa benki.


“Watanzania wengi wasio na utamaduni wa kuweka fedha benki watakubali kukatwa fedha zao kiasi hicho?” alihoji.


Alisema mfumo huo kwa sasa haueleweki hasa kwa watumiaji wa miamala ya simu kwa kuwa mawakala wake hawatoi risiti kama ilivyoagizwa na Serikali.


Aliongeza kuwa hata katika mashine za ATM, hakuna mashine za kukata kodi ya VAT hivyo hakuna maandalizi ya kukokotoa kodi hizo.


Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alipoulizwa kuhusu makato hayo, asisitiza azma ya Serikali kukusanya mapato kwa njia yoyote ile, bora tu iwe ni ya kisheria.


“Sina tafsiri yoyote ya kodi hiyo. Sisi kazi yetu ni kukusanya tu mapato… Sheria zinaruhusu kuwa na mabadiliko ya kodi kama hayo, kwa hiyo sisi tunatekeleza maagizo tu ya Serikali, haturuhusiwi kutafsiri kwa njia yoyote,” alisema Kayombo.

Jana, benki za CRDB,NMB na Standard Chartered zilitoa maelekezo kwa wateja wake juu ya kuwapo kwa makato hayo zikisema kuwa kutakuwa na ongezeko la asilimia 18 litakalotozwa katika gharama za huduma za benki kunzia leo, zikiungana na NBC ambayo ilitangaza azma hiyo wiki iliyopita.

“Kufuatana na Sheria ya Fedha (Finance Act, 2016) ongezeko la asilimia 18 litatozwa katika gharama za huduma za benki kuanzia Julai 1, 2016. Ongezeko hili (VAT) litakatwa kutoka katika akaunti na kama muamala hautapia kwenye akaunti, mteja atalipa kwa fedha taslimu,” ilisema sehemu ya taarifa ya Benki ya CRDB.

Hata hivyo, kama zilivyo taarifa za benki nyingine, ilisema ongezeko hilo halitahusika katika riba kwenye mikopo. Benki ya NMB, ilisema katika taarifa yake kuwa ongezeko hilo litakuwa katika gharama zote za miamala ya kibenki kuanzia leo.

Hata hivyo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa NMB, Vicent Mnyanyika alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo hasa kiasi ambacho wateja watakatwa alijibu kupitia ujumbe mfupi wa simu: “Sipo ofisini ila nahisi tangazo linajitosheleza.”

MARUFUKU WANANCHI KUKATWA ASILIMIA 18 YA VAT KATIKA HUDUMA MBALIMBALI ZA TAASISI ZA FEDHA NA SIMU

Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi habari juu zuio la taasisi za fedha na kampuni za simu kukata miamala ya kodi ya ongezeko la thamani VAT leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kamishina wa Mapato ya Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya .

Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imezuia taasisi za fedha (Benki) pamoja na kampuni za simu za mikononi kutoza ongezeko la thamani (VAT )kwa walaji (wananchi).

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidatta amesema kuwa fedha ambayo walikuwa wanakata haina ongezeko la thamani hivyo taasisi za fedha (Benki) kampuni za simu zimetakiwa zisiongeze miamala kwa wateja kwa kizingizio cha ongezeko la thamani.

Amesema kuwa fedha iliyokuwa ikikatwa imekuwa haikatwi hivyo kwa sheria hiyo inataka miamala hiyo iliyokuwa ikikatwa ikatwe asilimia 18 ya thamani ya ongezeko.

Aidha amesema TRA haijaweka muongozo wa juu ongezeko hilo kwa taasisi za fedha na kampuni za simu, hivyo kwa watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.

Kidata amesema kuwa wananchi wametakiwa wasiguswe kabisa katika ongezeko hilo kutokana na kutohusika na kufanya hivyo ni makosa.

Ukitaka kufanikiwa katika maisha hebu fanya haya

Safari ya kuelekea kwenye mafanikio inahitaji ujasiri, sio ujasiri tu bali ujasiri wa hali ya juu sana, kama ilivyo ujasiri alionao simba awapo mwituni, katika kusaka riziki yake ili kuhakikisha ya kwamba halali au hafi kwa sababu ya njaa.

Ujasiri huo huo alikuwa nao simba ndio ambao unauhitaji wewe ndugu yangu, katika safari ya kujifunza, chukua muda wa kujivika taswira ya kiujasiri ili ufanikiwe zaidi.
Nafahamu ya kwamba ipo haja ya wewe kuendelea kujua mbinu ambazo zitakufanya upate ujasiri huo. Hata hivyo niweze kushukuru Mungu kwa kunipa kalama hiyo ya kuweza kutumia fikra chanya ambazo zinanifanya nikupe baadhi ya mambo yatakayokusaidia kwa namna moja ama nyingine katika kusaka mafanikio hayo.

Kama alivyo simba kuishi katika misingi ya kujiamini ,basi ndivyo ambavyo nilivyo na hasira juu ya neno mafanikio.

Laiti ungelifanya uchunguzi siku moja kumchunguza simba ungaligundua  ya kwamba simba anaishi kwa kujiamini ili aendelee kuishi miaka mingi zaidi, pia simba huyo huyo anaishi kwa hofu ambayo itafanya  asilale au afe njaa.
Kupitia hilo ifike mahali na wewe pia uishi kwa kujiamini ya kwamba unajua ambacho unakihitaji, pia uishi kwa hofu ya kushindwa katika mafanikio pia uishi kwa kuwa na hofu ya Mungu kwa kila hambo ambalo unalifanya siku zote.

Watu wengi ambao wamefanikiwa na ambao hawajafanikiwa wanafanana katika masuala ya kuishi bila hofu ya Mungu. Wapo wale ambao licha ya kwamba maisha yao ni kitajiri, lakini bado wanaishi katika misingi ya kutenda mambo yao bila kumshirikisha Mungu, maisha ambayo kiukweli yanafanya waishi kwa wasiwasi licha ya maisha yao kuwa mazuri.

Nikija upande wa pili wa shilingi ambapo  watu wengi wanaishi maisha ya duni, ambapo wengi wetu tupo pia tumekuwa ni watu wa kukata tamaa siku zote na imefiki mahali tumejikuta tunamsahau Mungu, sio kumsahau Mungu tu bali imefika kipindi mpaka tunakufuru, unaweza kusema leo nahubiri la hasha ila ukweli ubaki palepale kwa jambo lolote ambalo unalifanya ili uweze kufanikiwa unatakiwa uishi kwa kuwa na HOFU YA MUNGU.
Zifuatazo ndizo kanuni ambazo unatakiwa kuzitumia kufanikiwa;

1. Kuwa tayari kujifunza.
Moja ya njia ya kukusaidia kufanikiwa zaidi ni lazima uweze kujifunza, huenda ukawa hajanipata vizuri ila ukweli wenyewe ndio huu hapa, watu wengi wanataka kupanda ngazi ya kimafanikio, bila kujua namna ya kuitumia ngazi hiyo ya kupata mafanikio.
Kwa mfano leo hii utamkuta mtu anataka kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini ukimwambia kuwa jambo hilo linahitaji ulazima wa kujifunza, utakuta mtu huyo hayupo tayari kujifunza juu ya biashara hiyo.

Lakini mimi huwa naamini jambo lolote ukitaka kulifanya kwa weledi ni lazima uwe tayari kujifunza, fikiria kwa umakini kisha uone ni kitu gani ambacho hauitaji kujifunza ambacho kinahusiana na mafanikio?

Ukitafakari kwa umakini utagundua ya kwamba hakuna jambo hata moja. Mambo ambayo hutakiwi kujifunza labda matendo ya hiari na yasiyo ya hiari yanayotokana na msukumo wa mwili tu yatokanayo na mawazo ya binadamu hasa hisia.

Kujifunza huku hakuhitaji wewe kukaa darasani miaka mingi, mpaka ufanikiwe ila inahitaji kujua unataka nini? Baada ya hapo ndio utagundua unatakiwa kujifunza nini.
Nikuibie siri ambayo hajawahi mtu yeyote kukuambia kwamba siri ya utajiri ipo kwenye "maandishi" siri hii usimwambie mtu bali chukua hatua pindi utakapopata ukweli juu ya jambo hilo, wengine wakikuuliza  juu ya mafanikio yako ndipo uwambia siri ya mafanikio ilipo.

2. Kuwa tayari kulipa gharama.
Mara kadhaa niwehi kuandika ya kwamba "chochote bila chochote huwezi kupata chochote" wengi walikuwa hawajanielewa ila leo ndio uwanja wako wa kuweza kunielewa juu ya jambo hilo.

Iko hivi kwa chochote kile ambacho unakitaka leo kina gharama zake, kama maelezo ya hapa juu yanavyojieleza kwamba unahitaji kuwa tayari kujifunza, basi jambo hili huenda sambamba na kulipa gharama, gharama hizi ni kama vile za kujifunza kwenye makongamono, kununua vitabu, majarida, magazeti ,vipeperushi kulipa ada za mafunzo mbalimbali ikiwemo semina au shule.

Ukiyafanya hayo utakuwa kwa ubora na weledi wa hali ya juu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao wanafanya mambo ya kimaendeleo kila siku, pia jamii ambayo inakuzunguka watatamani kwa kiwango kikubwa kitu ambacho unafanya wewe.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) atakiwa kuchukia Hatua Stahiki Dhidi ya Aliyemtukana Magufuli

SERIKALI imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchukua hatua stahiki katika shauri la kesi ya jinai namba 100 ya Jamhuri dhidi ya Isaac Emily aliyeadhibiwa kulipa faini kwa kumtukana Rais John Magufuli mtandaoni.

Hayo yamesemwa jana bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe wakati akitoa kauli ya serikali baada ya mwongozo ulioombwa na wabunge wa CCM, Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba na Livingstone Lusinde wa Mtera, baada ya hukumu hiyo kutolewa hivi karibuni. Hata hivyo, hatua stahiki hizo hazikuelezwa.

Alisema nia ya maagizo hayo kwa DPP ni kulinda dhana na dhamira ya adhabu katika mfumo wa haki jinai ambayo hutaka mhukumiwa kujutia kosa lake na wengine kujifunza kutoka kwake.

Katika maelezo yake, Waziri Mwakyembe alisema kwa hali ilivyo katika shauri hilo, dhana na dhamira ya adhabu haikuweza kufikiwa kwa mwenendo wa kuingiza siasa katika utekelezaji wa hukumu.

Alisema serikali imejiridhisha na kilichotokea katika shauri hilo na kauli za wabunge walioomba mwongozo kwamba masharti ya adhabu yalikuwa mepesi mno usiolingana na shauri lenyewe.

Alisema aliyehukumiwa analifanyia siasa suala hilo na kuigeuza adhabu rafiki aliyopewa kuwa burudani ya kisiasa katika mitandao ya kijamii.

“Mheshimiwa spika, nimejiridhisha na kilichotokea. Madhara ya mwelekeo huu mpya katika haki jinai, ni kuchochea vitendo zaidi vya ukaidi kwa mamlaka za nchi na hivyo kujenga msingi wa vurugu. Hili halikubaliki katika utawala wa sheria. Mdharau mwiba mguu huota tende,”alisema..

Alisema kosa kama hilo lilitokea Kenya mwaka jana ambapo mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, Alan Okengo (25) alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya dola 2,000 (Sh milioni 3.2) kwa kumtukana rais wa nchi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema pamoja na umri wake na uwezo wake mdogo wa kulipa faini, adhabu ilibaki palepale ili mkosaji ajutie kosa lake asije akarudia na jamii ijisikie salama.

Alisema pamoja na kutokuingilia mhimili wa mahakama na taratibu zake kitendo cha kuwapo kwa adhabu ambayo haijutiwi inakiuka dhana na dhamira ya adhabu.

Alisema kwa shauri la Emily, pamoja na kutiwa hatiani wakili wake aliomba mtuhumiwa alipe faini kwa kuwa hakusumbua mahakama na pia ni kosa lake la kwanza na ana familia.

Alisema wakati hakimu anamuuliza wakili wa serikali aliiachia mahakama kutoa maamuzi ambayo ilimpatia wakili wa utetezi maombi yake.

Mwakyembe alisema pamoja na maagizo ya serikali kwa DPP amewakumbusha waendesha mashitaka nchini kuwa macho na waweke mbele weledi na maslahi mapana ya taifa na kamwe wasiyumbishwe na mihemko ya kisiasa katika jamii.

HEBU SOMA KAULI HII YA DIAMOND PLATINUMZ!!! LAZIMA UTAMKUBALI TUU CHIBU


Msanii wa muziki, Diamond Platnumz ametoa kauli tata kuhusu uchawi na kuibua minong’ono mingi katika mitandao ya kijamii kuhusu wasanii kurogana.
Muimbaji huyo ambaye ana tuzo nyingi za kimataifa kuliko msanii yeyote nchini licha ya kukosa tuzo ya BET na kwenda kwa Black Coffee wa Afrika Kusini , alipost ujumbe wa ujio wa kazi yake mpya aliyowashirikisha wasanii wa kundi laP Square wa Nigeria huku akiwataka wenzake kutoa taarifa kwa waganga wao.

“Haya ongeeni vizuri na waganga wenu, baada ya siku nne naachia mashine nyingine,” aliandika Diamond kupitia twitter.

 Follow


Chibu Dangote @diamondplatnumz

Haya Ongeeni Vizuri na waganga wenu Baada ya siku nne simba Anaachia ile Mashine....

7:14 PM - 26 Jun 2016

  1821  4414


Kauli hiyo ya uchawi ambayo amekuwa akirudia rudia mara kadhaa katika mazungumzo yake, imewafanya mashabiki wa muziki kuamini kumbe wasanii wanatumia ndumba katika muziki wao.

Juni 5 mwaka huu, Diamond wakati akimtambulisha Rich Mavoko WCB, aliwataka waandishi wa habari kuacha kuchochea migogoro ya wasanii ili waganga na wao wapumzike.

“Watu wanapogombana tunaleta vita katika sanaa, familia, tuwapumzishe waganga na wao wanachoka, tunapeleka hela za bure,” alisema Diamond huku akicheka.

Mbowe: Alichokisema Lissu Kuhusu Dikteta Uchwara ni Kauli ya CHADEMA


Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe mara baada ya Wakili msomi wa CHADEMA Tundu Lissu kupata dhamana. (amezungumza na wandishi wa Habari)

Freeman Mbowe amesema kauli hiyo niyawapenda demokrasia wote Tanzania na nikauli ya CHADEMA kwa hiyo chama kitakua kila hatua kwenye kesi hiyo.....

RUBY AFUNGUKA MENGI KUHUSU YAMOTO BAND WALIVYO MFANYIA (AJUTA)


Msanii Ruby ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Yamoto Band unaofahamika kwa jina la 'Suu' amefunguka na kupinga kauli iliyotolewa na maneja wa Yamoto Band, Mkubwa Fella kuwa yeye ana stress ndiyo maana maana alishindwa kutokea kwenye video.

Akiongea na Planet bongo ya East Africa Radio Rubby amesema Yamoto Band hawakuona umuhimu wake kwenye video hiyo ndiyo maana waliweza kushoot video hiyo siku ambayo yeye alikuwa busy na mambo yake mengine, na kusema kutokana na wao kutaka video hiyo ifanyike ndani ya siku hiyo na kupinga wazo la kumsubiri kidogo inatosha kuonyesha kuwa hawakuona umuhimu wa yeye kuwepo kwenye video hiyo, kwani angekuwa na umuhimu wangeweza kumsubiri.

"Unajua siku ambayo wao walikuwa wakishoot video hiyo mimi nilikuwa na mambo yangu mengine hivyo nilikuwa busy, niliwaomba kama wanaweza wanisubiri kidogo nimalizane na hizo kazi zangu lakini wao wakafanya video hiyo. Hilo linatosha kuonyesha sikuwa na umuhimu kwani ningekuwa na umuhimu wangeweza kunisubiri, mimi sikukataa na nilikuwa na uhakika asilimia mia nitakuwepo kwenye video ile sema kwa kuwa walikuwa na haraka ndiyo maana imetokea hivyo." alisema Rubby

"Kiukweli mimi nimeumia sana maana Audio ile tumefanya muda mrefu na waliweza kusubiri mpaka tukakamilisha iwaje kwenye video washindwe kunisubiri, maana hii kazi tunasaidiana mimi niliwaambia niko busy nisubirini wangeweza kunisubiri tu kisha tukafanya video pamoja" aliongeza Rubby

Waziri Mkuu awataka wabunge wa upinzani kurejea Bungeni .


SeeBait

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo, Bungeni Mjini Dodoma amewataka wabunge wa upinzani ambao wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30 kuingia Bungeni na kuacha kususia vikao vya Bunge kwani hakuna tija kwa Taifa.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.

“Kitendo cha baadhi ya waheshimiwa wabunge kususia vikao vya Bunge hakitoi picha nzuri kwa wananchi waliotuchagua kuwasilisha matatizo yao katika Bunge hili, hivyo natoa rai kwa waheshimiwa wabunge hao kutafakari upya uamuzi wao na niwasihi kwa busara zao waingie ili kwa pamoja na kwa ushirikiano tuweze kutoa ushauri kwa Serikali,” alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha Mhe. Majaliwa alitoa ufafanuzi juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili kujadili na kuhoji utendaji wa Serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushitakiwa wanapotimiza wajibu wao wakiwa Bungeni.

Aliendelea kwa kusema kuwa kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule Nchini ila kwa Wabunge, hivyo basi hakuna mbunge aliyefungwa mdomo labda aamue kujifunga mdomo yeye mwenyewe.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa Bunge linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge, hivyo ni vyema zikafuatwa kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na endapo kuna utata katika jambo lolote ndani ya Bunge zipo taratibu zilizowekwa na kanuni za kufuata ili kupata ufumbuzi na si kwa kususa kuingia Bungeni kwani hakuna tija kwa Taifa.

Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30, 2016 mpaka leo Juni 30 ambapo Bunge limehitimishwa.

Aidha wabunge hao wamekuwa wakiingia Bungeni kila asubuhi na jioni kisha kutoka mara tu Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson anapomaliza kusoma Dua maalum la kuliombea Bunge na Taifa.

HII HAPA JOINING INSTRUCTIONS KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO (FORM 5) MWAKA 2016

Video!!!! ALICHOKISEMA TUNDU LISSU BAADA YA KUPEWA DHAMANA JANA NA KUTOKA MAHABUSU.


June 30 2016 Mbunge wa Singida Mashariki, ‘CHADEMA’ Tundu Lissu amesomewa shitaka lake la kutoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu June 28 2016 kinyume cha kifungu namba 32 ya sheria ya magazeti. Lissu amekana shtaka hilo na ameachiwa kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.
Inadaiwa Lissu alitoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya Kisutu kwa kumuita Rais ‘dikteta uchwara’, mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili na kesi imeahirishwa mpaka August 02 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa. Nje ya mahakama ya Kisutu, Lissu ameyazungumza haya……….
>>>>’mimi nilidhani kwamba baada ya kauli yangu wenye busara wangenyamaza kimya lakini inaelekea busara inaonekana ni bidhaa adimu wameyaleta mahakamani, mimi na jopo langu la mawakili tutapata fursa ya kumuita huyo niliyemuita dikteta ‘uchwara’ kuja mahakamani kuiambia mahakama kuwa yeye si dikteta uchwara




MILLARD AYO

Magazeti ya tanzania yalichoandika leo JUNI 1 kwenye habari za kitaifa kimataifa michezo na stori za Udaku.

Karibu tunakuletea headlines za magazeti ya leo Julai  1 kwenye habari za kitaifa kimataifa michezo na udaku,Usisahau kulike  Page yetu ya facebook hapo chini ili ujue kilichojiri muda wowote 

IMG_20160701_044856

IMG_20160701_044958

IMG_20160701_045014

IMG_20160701_045030

IMG_20160701_045047

IMG_20160701_045102

IMG_20160701_045121

IMG_20160701_045137

IMG_20160701_045153

IMG_20160701_045212

IMG_20160701_045230

IMG_20160701_045248

IMG_20160701_045307

IMG_20160701_045327

IMG_20160701_045353

IMG_20160701_045417

IMG_20160701_045438

IMG_20160701_045502

IMG_20160701_045521

IMG_20160701_045541

IMG_20160701_045618

IMG_20160701_045648

IMG_20160701_045703

IMG_20160701_045810

IMG_20160701_045841

IMG_20160701_045903

IMG_20160701_045917

IMG_20160701_045937

IMG_20160701_045954

IMG_20160701_050010

IMG_20160701_050029

IMG_20160701_050048
IMG_20160701_050107

 

Gallery

Popular Posts

About Us