Saturday, March 26, 2016
Mkenya aliyejiweka katika picha za wengine
Mwanamke mmoja kutoka Kenya amejiweka katika msururu wa picha za likizo za watu wengine katika mtandao wake wa facebook.
Baada ya kushindwa kuwa na uwezo wa kusafiri kwenda
barani Asia,Sevelyn Gat alijiweka katika picha karibu na ndege,katika
ukuta mkubwa wa Uchina na hekalu moja.Picha hizo zilizowekwa kwa njia ya nzuri ili zisiweze kubainika kuwa za uongo zilikuwa mbaya zaidi na hivyobasi kuweza kupendwa na mara nyingi sana.
Mfanyibiashara wa Nairobi sam Gachuru amejitokeza na kumsaidia kutafuta fedha ili kwenda likizo.
Kulingana na Sich Chirpse Sam aliwasumbua rafikize kuchangisha fedha za mahala pa kulala,nauli bima na pesa za kutumia.
Seve pia amepata kibali chake cha kuzaliwa anemtuma ombi la pasipoti na amepata kufunzwa kama meneja wa mradi.
SHARE!
Video za Justin Bieber zatazamwa mara bilioni 10
Published Under
TOP STORIES
Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara bilioni 10.
Msanii
huyo wa Canada ambaye alitoa kibao kipya Purpose in Novemba alipata
idadi hiyo katika kipindi cha miaka sita na miezi mitatu au siku 2,316.
SHARE!
Wanariadha wala sabuni wakidhania ni chakula
Published Under
STORI KALI
Wanariadha
waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijipata wamekula sabuni
baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa
lugha ya kiingereza.
Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za
Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata
zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na
gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily.Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinuka harufu nzuri .
Walioshuhudia wanasema kuwa sabuni nyingi zilitupwa kandakando ya barabara huku zikiwa zimeumwa.
Tatizo ni kwamba sabuni hizo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na hivyobasi wanariadha hao hawakuelewa lugha hiyo kulingana na gazeti hilo.
Hatahivyo walioandaa mbio hizo waliomba msamaha.Pakiti za sabuni hizo zilikuwa kama zile za chakula.
Pia kulikuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya majeraha katika mbio hizo huku wanariadha 12,200 wakihitaji kupatiwa matibabu wakati na hata baada ya mbio hizo.
Haijulikani ni majereha mangapi yalisababishwa na kisa hicho cha sabuni.
SHARE!
Wagombea warushiana matusi Marekani
Published Under
US Election
Wagombeaji wawili wa Urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamegombana vikali na kurushiana matusi juu ya wake zao
SHARE!
MAALIM SEIF AREJEA ZANZIBAR BAADA YA MAPUMZIKO HOTELINI DAR.
Published Under
ZANZIBAR
Siku
chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada
ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya
upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, amerejea Zanzibar.
Maalim Seif ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam kwa takribani siku 17, jana alirejea Zanzibar kuendelea na mapumziko yake.
Maalim Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari wake kupata mapumziko ya muda mrefu.
Kurejea kwa Maalim Seif visiwani humo kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya Wazanzibar kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.
Maalim Seif aliugua wakati Wazanzibar wakiwa katika maandalizi ya kurudia uchaguzi mkuu uliofanyika March 20, mwaka huu baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar( ZEC), Jecha Salim Jecha kwa madai kuwa uligubikwa na dosari nyingi.
Gharama za Hotelini
Taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari siku chache zilizopita zilidai kuwa kila siku aliyokaa kwenye hoteli hiyo, Maalim Seif alikuwa akitumia wastani wa Sh. 6,162,500.
Kutokana na takwimu hizo, hadi kufikia jana, Maalim Seif atakuwa ametumia kiasi kisichopungua sh. Milioni 92.4
Chumba alichokuwa akilala Maalim Seif katika Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano kinalipiwa dola za Marekani 2,500 kwa usiku mmoja.
Maalim Seif alikuwa akiishi hotelini hapo na wasaidizi wake watano, ambao wote gharama zao zinalipwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ
SHARE!
Haya hapa Magazeti ya leo March 26 2016 kwenye,habari za`kitaifa kimataifa Udaku, na michezo
Published Under
MAGAZETINI LEO
March 26 2016 nakuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa
Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa
karibu yangu kwenye facebook/tanzaniampya news blog, pia kwenye twitter @tanzaniampysasa.
SHARE!
Subscribe to:
Posts (Atom)