KINGAZI BLOG: 08/01/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, August 01, 2016

Ongeza Nguvu za Kiume kwa Viagra za Kiasili



Image result for Natural Viagra photos


Kujiamini kwa mwanaume lijali ni pale anapomtosheleza mwenzi au mpenzi wake wakati wa kufanya mapenzi. Na furaha ya mwanamke ni pale anapofikishwa kwenye utoshelevu anaoutarajia kutoka kwa mwanaume au mwenzi wake wakati wa kufanya mapenzi. Kutokana na uhitaji na shauku ya kutaka kuwafikisha wapenzi wao kwenye utoshelevu imewalazimu baadhi ya wanaume kutumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume ikiwemo Viagra. Madawa hayo licha ya kuwa na athari kiafya kwa wanadamu hususan wanaume wanayoyatumia lakini pia imekuwa ni chanzo cha vifo vya baadhi ya wanaume wanaotumia madawa hayo hasa pasipo kufuata ushauri wa kidaktari. Si aghalabu kusikia matukio ya vifo vya wanaume kwenye nyumba za kulala wageni na watu wengi wamekuwa wakijiuliza nini tatizo au chanzo cha vifo hivyo. Wengine wamekuwa wakihisi pengine chanzo cha vifo hivyo ni kuzidiwa na dozi za mapenzi wakati wa kungonoka kutoka kwa wapenzi wao.

Watu wengi hawajui kwamba vyakula vyetu vya asili ni Viagra tosha kabisa ambavyo vikitumiwa katika mchanganyiko fulani wanaume wanapata msisimko wa kufanya mapenzi kwa maneno rahisi vyakula hivi vikitumiwa kwa kufuatisha mchanganyiko fulani ni Viagra tosha tena ya asili na iliyo salama kabisa kwa asilimia 100. Hapa nitakwenda kueleza baadhi ya vyakula au michanganyiko ya vyakula ambayo mwanaume akiitumia jongoo litapanda mtungi sawasawa na kuwafanya wenzi wao kuwa na furaha kwa kufikishwa wanapotaka wafikishwe.


Moja: Mwanamke mtengenezee mpenzi wako ‘Banana Milkshake’ mida ya jioni ili usiku akupandishe kileleni. Aidha jenga tabia ya kumtengenezea mwanaume wako milkshake hii kila siku. Namna ya kutengeneza: Osha matunda ya strawberries kama 5-10, ondoa vikonyo vyake na kata katikati vipande viwili kila tunda. Menya ndizi mbivu 2-3 na kata kata vipande. Weka maziwa glasi moja kwenye blender na pia tia strawaberries na ndizi. Weka asali vijiko 2 vikubwa badala ya sukari. Funika blenda na tengeneza milkshake yako . Weka milkshake kwenye glasi na mpe mwenzi wako anywe taratibu. Hii licha ya kuongeza msisimko wa kufanya tendo la ndoa (libido) pia ni mahususi kwa kuzalisha homoni za mapenzi (sex hormone production).

Pili: Changanya asali na unga wa iliki na na unga wa pilipili kiasi. Mwanaume tumia mchanganyiko huo na unaweza kuboresha zaidi kwa kula pamoja na yai moja la kuku wa kienyeji lililochemshwa kiasi (half boiled) kila siku hadi mambo yawe sawasawa.

Nne: mwanaume tumia maziwa yaliyotiwa unga kiasi wa pilipili na lozi (almond) au maziwa yaliyotiwa asali na samli (ghee).

Tano: Mwanaume kula nanasi lililowekewa asali na unga kidogo wa pilipili au chill. Kadhalika tumia pine nuts au mbegu za maboga (pumpkin seeds) ambazo huongeza madini ya zinki mwilini. Madini hayo ni muhimu kwa uzalishaji wa shahawa.


Sita: Kama hujisikii hisia za kufanya mapenzi hebu chemsha na kula mboga iitwayo Asparagus kwa siku tatu tu utaona hisia kali za kufanya mapenzi iwe ni kwa mwanume au mwanamke.

Mrema akutana na Madereva Bodaboda wa Kinondoni........Awataka wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa

Mwenyekiti wa Parole Augustino Mrema amewataka madereva bodaboda kote nchini kujiepusha na tabia za kushiriki maandamano ya kisiasa yanayoandiwa na baadhi ya wanasiasa kwa lengo la kuvunja sheria za nchi.

Pia amewaagiza waendesha bodoboda Kinondoni wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa ili ayakabidhi kwa rais Magufuli

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.

Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo

Taarifa Toka Ikulu: Rais Magufuli Katoa Maagizo Mazito Kwa Viongozi Wote Hapa Nchini........Pia Katoa Onyo Kali Kwa Walimu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wote wa kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 01 Agosti, 2016 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na Buseresere Mkoani Geita.

Katika agizo hilo Dkt. Magufuliamewaonya walimu ambao wameanza kufanya udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

"Ninafahamu mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo, wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za wanafunzi laki moja wagawane.

"Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali" Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na agizo hilo, Rais Magufuli pia ametaka viongozi wa ngazi zote katika Mikoa kuhakikisha wana takwimu za idadi ya wanafunzi katika shule zote zilizopo katika maeneo yao ili kurahisisha ufuatiliaji wa fedha hizo na amesema kuwa kuanzia sasa ataanza kutembelea shule kwa kushitukiza na kwamba kiongozi atakayeonekana kutojua takwimu itakuwa ni uthibitisho kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa alionao.

"Na nitoe wito kwa viongozi wa Mikoa, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, kila mmoja awe na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule zao, hatutaki kuwapunja wanafunzi hela ambayo wanatakiwa kupata, lakini pia hatutaki kutoa hela ambayo haitakiwi"Amesisitiza Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ametumia mkutano huo kueleza juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali yake ya Awamu ya Tano, kutekeleza ahadi yake ya kujenga Tanzania Mpya pia amewataka viongozi na watendaji wa Serikali kutekeleza wajibu wao kwa kutembelea wananchi wanaowaongoza badala ya kukaa muda mwingi ofisini huku akisisitiza ofisi hizo kuwepo katika maeneo yenye shughuli husika.

Aidha, Dkt. Magufuli amekosoa utaratibu unaotumiwa na Halmashauri nyingi za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kutumia mawakala katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri akisema mawakala hao wamekuwa wakitumia utaratibu huo kukusanya fedha nyingi na kisha kuwasilisha kiasi kidogo katika Halmashauri husika.

"Hivi kwa nini Halmashauri msingekuwa na maafisa wenu wazuri na mkawa na mashine za kielektroni kwa ajili ya kukusanya fedha? Amehoji Dkt. Magufuli na kuongeza kuwa;

"Tena mawakala wengine ndio hao hao wamekuwa wakikusanya kodi hata kwa wananchi wanyonge wenye vibiashara vidogo vya kuuza mchicha bila hata kuwaonea huruma"

Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amemaliza ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita na yupo nyumbani kwake Chato Mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Chato

01 Agosti, 2016

Mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia


GHENT, Ubeligiji
WATUMIAJI wa pombe sasa wataweza kupata auheni ya bei ya vinywaji hivyo, baada ya wanasayansi kugundua kifaa maalumu kitakachotumika kubadilisha mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia.

Kugunduliwa kwa kifaa hicho ni mkombozi kwa wamiliki wa viwanda vya pombe ambapo wataweza kupata malighafi ya kutengenezea bia kwa urais.

Kinatarajiwa kufungwa kwenye vyoo vya baa mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa mikojo hiyo ya walevi.

Kifaa hicho ambacho kitakuwa kikitumia umeme wa jua pia kitakuwa na uwezo wa kubadili mikojo hiyo kutumika kama maji ya kunywa.

Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubeligiji, walisema kifaa hicho kitaanza kutumika hususan maeneo ya mijini kwenye nchi zinazoendelea.

Licha ya kuwepo kwa mashine maalum yenye uwezo wa kutibu maji machafu ikiwemo mkojo kisha kutumika kwa matumizi mengine muhimu ya binaadamu, wataalamu hao wamesema kifaa hicho walichokigundua kinauwezo zaidi wa kuyatibu maji hayo bila kutumia nguvu ya umeme.

Dk. Sebastiaan Derese, alisema kifaa hicho kitakuwa kikitunza mikojo kwenye tangi maalum ambalo litatumika kutibu kisha kutumika kama malighafi ya kutengenezea bia.

Kwa mara ya kwanza kifaa hicho kilianza kutumika kwenye tamasha la muziki ililofanyika mjini humo ambapo jumla ya lita 1000 za mikojo, zilikusanywa kisha kutengenezewa bia.

Alibainisha kuwa, bia zilizotengenezwa kupitia mikojo hiyo imewavutia wanywaji wengi hususan kwenye matamasha mbalimbali.

Waziri Mkuu: Wakurugenzi Watakaotoa Taarifa Za Uongo Kufutwa Kazi


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitasita kuwaondoa katika nyadhifa zao Wakurugenzi wote watakaoshiriki katika kutoa taarifa za uongo kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

“Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo  kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakiandika taarifa za uongo kuwa mradi umekamilika wakati haujajengwa, hivyo wakurugenzi watakaoshiriki kutoa taarifa zisizokuwa sahihi wataondolewa,” alisema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana jioni (Jumapili, Julai 31, 2016) wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Alisema alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakurugenzi katika halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatembelea miradi yote inayojengwa katika maeneo yao ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama thamani yake inalingana na kiasi cha fedha kilichotolewa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali aihitaji Halmashauri kutoa ajira za mikataba kwenye kada zilizopo katika muundo wa ajira hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya mapitio ya watumishi wa mikataba.

“Tumeruhusu kuajiri kwa mikataba walimu wa masomo ya sayansi kwa kipindi cha miaka miwili tena kwa waliostaafu. Kuna kada zilizoko katika muundo wa ajira hizo hatuhitaji watumishi wa mikataba wakiwemo madereva msiwatumikishe kwa mikataba watakosa stahili zao,” alisema.

Akizungumzia suala la watumishi hewa mkoani Morogoro Waziri Mkuu alisema ni vema wakaendelea kufanya uchunguzi na ifikapo mwisho wa mwezi huu wawe wamekamilisha taarifa na kuanza kuchukua hatua kwa waliohusika kwa waliohusika.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe katika taarifa yake aliyoiwasilisha kwa Waziri Mkuu alisema mkoa unaendelea kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuzitaka taasisi zote za Serikali kufanya uhakiki wa mishahara hewa na malipo batili ya watumishi.

Alisema mkoa umebaini watumishi hewa 315 ambao wameisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 2.132 ambapo timu ya uhakiki bado inaendelea na zoezi hilo na taarifa kamili itatolewa mara kazi hiyo itakapo kamilika.

Jibaba lapatikana likifanya mapenzi na 'Bomba la gari' (Video)

Mwanamume mmoja kutoka Brazil amewashangaza wengi baada ya kupatikana aki’fanya mapenzi’ na bomba la moshi la gari.

Jamaa huyo anaonekana akiifanya shughuli yake kwa pupa hata baada ya mpiga picha kufika karibu.

Hata baada ya mpicha kumfikia, jamaa huyo anaendelea na kazi yake.

Kuona video ingia kwenye Link hapa chini:

https://web.facebook.com/today.viral.videos/videos/vb.1692784074338489/1756943344589228/?type=2&theater

Chadema wajipanga kuandamana nyumbani kwa JPM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake.

“Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.

“Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwaonya Chadema kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila kufuata utaratibu kwani hatawavumilia.

Nafasi 6 za AJIRA Pact Tanzania tuma maombi kabla ya tarehe 5 August2016



EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

Pact Tanzania is a field office of “Pact” an international non-governmental and non-profit making organization with its headquarters in washington DC. Pact Tanzania exists to build local capacity to enable systematic solutions that allow those who are poor and margainalized to earn a dignified living, be healthy and enjoy the benefit nature provides. For effecient execution of its duties, Pact Tanzania is looking for enthusiastic, creative, energetic individuals to fill the below mentioned positions:

1. Senior M&E Officer
– University degree in public health, sociology, demography, statistics, or other social science area, Masters Degree preferred
– Academic qualification in Monitoring and Evaluation will be an added advantage.

2. Senior Data Analyst
– Masters in Statistics or related field (social sciences, public health, demography)

3. Senior Health Informatics Officer
– Bachelors Degree in Computer Science or Health Informatics. Masters Degree preferred

4. M&E Officer
Locations: dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mbeya

– Bachelor’s Degree in public health, sociology, demography, statistics, or other social sciences area; Masters Degree preferred

5. Senior Data Manager

– Bachelors degree in statistics, Information technology or health and social sciences eg. sociology demography, public health, development management related field is required.
– Academic qualification in monitoring and evaluation will be an added advantage.

6. Data Manager
Locations: dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mbeya

– Advance Diploma or Bachelor’s degree in statistics, Information Technology or Health and social sciences eg sociology, demography, public, development management related field is required.
– Academic qualification in monitoring and evaluation will be an added advantage

If you believe you are he ideal person we are looking for, submit your application letter describing why you are right candidates for this position and curriculum vitae detailing your experience with three referees tohumanresourcesTZ@pactworld.org.

Note: The subject of your email should mention the position you applying for and your choice of location.

Closing date for applications 5th August, 2016 (Only shortlisted candidates will be contacted)

Source: The Guardian July 27, 2016

MREMBO JOKATE MWEGELO ADAIWA KUSHURIKI PATI YA MASHOGA


Tuhuma nzito! Ubuyu ulionyooka mjini unadai kwamba, mwanamitindo the big name Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ anadaiwa kushiriki kwenye pati ya wanaume wanaojihusisha na ngono ya jinsi moja almaarufu mashoga ambayo imeelezwa kuwa hufanyika kwa siri kila Jumamosi moja ya mwezi.

Habari hizo zilidai kwamba, shughuli hiyo hufanyika kwa siri kubwa kwenye jumba moja la kifahari lililopo Masaki jijini Dar. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kuna shirika moja lina mpango wa kuendeleza ushoga hapa nchini hivyo limekuwa likikutana na mashoga mbalimbali kwa kuwaandalia pati na kuwawezesha ambapo ndani ya pati hiyo kuna mambo yasiyo ya kawaida yanayofanyika. 



KISIKIE CHANZO    “Ninyi waandishi wa habari hivi mnajua kuna maovu mengi ambayo yanaendelea hapa nchini? Hivi mnajua kuwa kuna ufuska unaendelea kwenye pati zinazofanywa kila Jumamosi moja ya kila mwezi? Huko huwa wanaalikwa wanawake na wanaume lakini walengwa

wakubwa ni mashoga,” alinyetisha mtoa ubuyu wetu na kuongeza: “Wamo pia mastaa na watu maarufu kama Jokate.” Baada ya chanzo chetu kutoa ubuyu huo, Wikienda lilituma kachero wake wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambaye alijipenyeza na kuingia ndani ya pati hiyo ambapo alishuhudia mambo kibao ya aibu kwani anakuambia kuna kipindi kinaitwa kujichanganya (mixing time) ambapo inabidi wanaume wajichanganye na wanawake wakati huo ndiyo watu huutumia kufanya mambo ya kifuska ambayo hayaandikiki gazetini. MSIKIE OFM: “Dah! Ingekuwa inaruhusiwa kupiga picha, ningefanya hivyo kwani ni mambo ya kushangaza ambayo yanaendelea kule ndani kwenye jengo (jina linahifadhiwa) ambalo liko jirani na Ufukwe wa Coco (Dar) na linalindwa saa zote. “Cha kushangaza ambacho sikukitarajia ni pale nilipomuona mwanamitindo Jokate Mwegelo naye amekuja kwenye sherehe. Yeye hakuniona na wala asingenijua huenda alipoalikwa hakujua kinachoendelea lakini alikuja na alisherehekea kama kawaida na mwingine yupo ana jina

ya kuulizwa swali hilo, Jokate alikaa kimya kwa zaidi ya dakika ishirini ambapo mwandishi wetu alimtupia swali lingine akimuuliza sababu ya ukimya ni nini? Ukimya huo ulikoma baada ya saa moja ambapo alijibu akisema kuwa kuwa hapajui sehemu hiyo na wala hakwenda huko. Mwandishi aliendelea kumbana kwa maswali na kumkumbusha watu aliotajwa kuwa nao ambapo alisema kuwa, hakumbuki ni lini kisha akaongeza kuwa hayupo Dar huku akisisitiza kuwa amekuwa akinyamaza kwa sababu anasingiziwa vitu vingi. “Mimi sipo Dar, hiyo pati ilifanyika lini? Mimi sijui lolote, kwani unaongelea nini? Hata hivyo, naomba msiniandike kwa mambo hayo machafu, mimi sielewi,” alisema Jokate. TUJIKUMBUSHE Hivi karibuni kuliibuka tafrani kati ya mashoga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo baadhi walikamatwa baada ya kukutwa kwenye pati yao maeneo ya Kinondoni ndipo kukaibuka maneno kuwa kuna watu wanaotaka kumkwamisha Makonda kwa kuwafadhili watu hao kwa ajili ya kuendeleza uchafu huo ambao unapigwa vita kote nchini. NENO LA MHARIRI Gazeti hili bado linaendelea kufuatilia sherehe hizo zinazotajwa kufanyika kila Jumamosi moja ya mwezi na  kama litajiridhisha litafikisha sehemu husika lengo ikiwa ni kukemea mambo ya kishoga ambayo hayakubaliki nchini kwetu.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA


Wafanyabiashara Wawili Wauawa Gesti Dar es Salaam.............huku miili yao ikiwa imeungua moto

Watu wawili wamekutwa wamefariki katika nyumba ya wageni ya Kings Rest House iliyopo Mtaa wa Bumila, Gongo la Mboto jijini Dar  huku miili yao ikiwa imeungua moto.

Mmiliki wa gesti hiyo, Damian Mng’ong’o alisema alifuatwa kanisani jana saa 1.30 asubuhi na kuambiwa kuna chumba kimoja katika gesti yake kinafuka moshi na aliondoka kanisani kuelekea ilipo nyumba hiyo.

Alisema alipofika aliona moshi bado unafuka huku nje kukiwa na umati mkubwa wa watu wakishangaa.

“Tulifanya uamuzi wa kufungua mlango lakini hatukuona mtu yeyote chumbani, ndipo mmoja wa wafanyakazi alipofungua mlango wa choo ndani ya chumba tukakuta maiti mbili zikiwa zimechomwa. "

Alisema mhudumu wa gesti alitueleza kuwa jana (juzi) saa tano asubuhi alikuja mwanamume mmoja akachukua chumba na baadaye jioni alikuja kijana mwingine wakawa wameingia wote katika chumba hicho.

“Baada ya muda nilipiga simu polisi kuripoti tukio hilo nao waliwasili ndani ya muda mfupi wakafanya uchunguzi wao na kuhoji baadhi ya watu, baadaye wakawaleta madaktari kupima, kisha wakaondoka na maiti hizo mbili kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya hatua nyingine.”

Mfanyakazi wa jikoni katika gesti hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema watu hao waliofariki ni wafanyabiashara wanaouza ng’ombe katika mnada wa Pugu na mara nyingi wakija Dar es Salaam hufikia hapo.

“Wengi wanaofanya biashara ya ng’ombe wakija hufikia hapa, mpaka sasa sijajua kilichotokea kwa hawa waliokufa, lakini tukio hili limewashtua wenzao kwani baadhi walipoona tukio hili wameingiwa na hofu na kuondoka,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema wanaendelea kuchunguza na taarifa za awali hazijathibitisha kama waliuawa hapo gesti au sehemu nyingine na kupelekwa hapo.

“Kuna viashiria kuwa huenda waliuawa wakaletwa pale kwani wana alama ya kamba katika shingo kama vile kuna mtu aliwanyonga na katika matumbo yao kuna majeraha kama wamechomwa kitu chenye ncha kali,” alisema na kuongeza:

“Mpaka sasa uchunguzi unaendelea na Jeshi la Polisi linafanya kazi yake na tunasubiri taarifa kutoka kwa wataalamu wa masuala ya uchunguzi na alama za vidole ambayo itaeleza kwa nini wao waungue lakini nguo zao zisiungue. Pia kitanda na vitu vingine visiungue na kwa nini watu waende kuzima moto, wakati watu wameshafariki,” alisema Hamduni.

Hamduni alisema mmoja wa waliofariki alijiandikisha kama Lameck Ludovick, mfanyabiashara na mkazi wa Dar es Salaam.

Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe 

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitotekeleza mpango wa kuhamia Dodoma kwani ni wa kukurupuka.

Msimamo huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alipozungumza na gazeti hili wakati wa kutoa heshima za mwisho za aliyekuwa mpigapicha mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga ambaye anatarajiwa kuzikwa leo huko Kwimba, Mwanza.

“Serikali inaendeshwa kwa kukurupuka. Ni mpango usiotekelezeka,” alisema Mbowe.

Alisema uhamaji unaotekelezwa sasa haukuwa na maandalizi wala mkakati kwenye ilani ya chama tawala wala Bajeti ya Serikali hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukwama huko mbele.

Miongoni mwa vitu vinavyoufanya mpango huo usitekelezeke kwa ufanisi, kwa maoni yake, alisema miundombinu ya kutosheleza watendaji wote na wadau wengine muhimu ambao watalazimika kufuata huduma muhimu za wizara na idara za Serikali.

“Huku ni kuwaumiza wananchi. Watumishi wa Serikali, wanahabari na wadau wengine wakihama wote watapata wapi malazi katika mji ule?”

Muda mfupi baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuiongoza CCM, Julai 23, Rais John Magufuli alieleza nia yake ya kutekeleza uhamisho wa makao ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na kwamba atahakikisha, ndani ya miaka minne anatimiza ndoto hiyo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya tangu mwaka 1973.

Siku moja baadaye, akihutubia kwenye hafla ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza kuhamia mjini humo Septemba na kusema kuwa wizara nyingine zitamfuata.

Tangu kutolewa kwa matamko hayo ya viongozi waandamizi wa Serikali; wizara, taasisi, mashirika ya umma, idara na baadhi ya ofisi binafsi, mabalozi na wanadiplomasia zimeanza kuandaa mazingira ya utekelezaji huo.

Lakini, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alionyesha wasiwasi wake juu ya umakini wa Serikali kutekeleza azma hiyo akisema kutakuwa na usumbufu mkubwa kwa watumishi na familia zao suala linaloweza kupunguza morali yao ya kazi. “Watu wana familia zao. Watoto wanasoma... Dodoma hakuna shule za kutosha watoto watakaohama na wazazi wao.”

Alisema wakati wazo hilo linatolewa na kuungwa mkono enzi za Mwalimu Nyerere kulikuwa na sababu za msingi lakini hivi sasa kuna mabadiliko makubwa yaliyochagizwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Alisema wakati huo mindombinu ya mawasiliano haikuwa rafiki tofauti na iliyopo sasa inayowezesha watu walioko New York, Marekani kufanya mkutano na wenzao waliopo popote duniani kwa kutumia miutano kwa njia ya masafa. “Sababu zimepitwa na wakati,” alisisitiza.

Alishauri, mpango huo ungetekelezwa kwa utaratibu maalumu, akitoa mfano kwa wizara moja au mbili kuhama kwa kila mwaka mpaka zitakapokamilika ili kupunguza gharama zisizo na ulazima.

Alisema kuhamisha wizara siyo waziri au katibu mkuu pekee, bali ni watumishi wote na miundombinu yote iliyopo ambayo ni muhimu kwa utekelezaji wa majukumu yake: “Kwa mfano, Wizara ya Kilimo ina watumishi 2,000 na maelfu ya mafaili yenye taarifa za kiutendaji… unawahamishaje watu wote hawa na mindombinu iliyopo unaifanyaje? Namshangaa IGP anaposema anahama wakati mifumo yote ya uchunguzi na taarifa imejengwa hapa kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi.”

Wiki iliyopita, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Marijani alisema jeshi hilo litahamia Dodoma mwezi huu na watakaohusika ni Inspekta Jenerali na baadhi ya makamishna.

Mo Dewji akabidhi barua yake Simba, kununua hisa asilimia 51

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema tayari ameandika barua kwa uongozi wa Simba kueleza kuhusiana na uamuzi wake wa kutaka kununua hisa za Simba kwa asilimia 51.

Mo amesema ameandika barua hiyo leo asubuhi baada ya kusikia baadhi ya viongozi wa Simba wakisema hakuwa amefanya hivyo.

“Kweli hatukuwa tumeandika barua kwa kuwa nilitaka mchakato uchukue hatua. Baada ya hapo lingefuata suala labarua, lakini kwa kuwa wanasema lazima barua, basi acha tufanye hivyo.

“Tayari barua imeandikwa na imepelekwa kwenye klabu, kukawa hakuna mtu na sasa imepelekwa ofisini kwa Aveva,” alisema Mo.

“Nilichoeleza kwenye barua yangu ni kilekile kwamba ninatoa ofa ya Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51. Niko tayari kushirikiana na uongozi wakati wa mchakati kama ambavyo nilieleza awali,” alisema.

 

Gallery

Popular Posts

About Us