KINGAZI BLOG: 05/19/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, May 19, 2016

WAREMBO WANAOWANIA U 'Miss' WAANZA KUIUIFUA ARUSHA.

WALIMBWENDE JIJI LA ARUSHA WAAHIDI KUTOACHIA TAJI LA MISS TANZANIA 2016

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha wakiwa katika pozi

warembo hao wakiwa wanacheza hii ikiwa ni moja ya mazoezi yao wanayoyafanya ndani ya ukumbi wa hoteli Naura Spring Arusha ambapo wameweka kambi

Kusimamishwa kwa shindano la umrembo Tanzania (Miss Tanzania ) kwa mwaka mmoja imekuwa ni changamoto kubwa kwa waandaaji wa shindano hilo, kwani warembo wengi wamesahau mambo kibao ndani ya mashindano hayo pia kueleza kuwa shindano hilo limepoteza umaarufu wake.

Hayo yamebainishwa na muaandaaji wa shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha kutoka katika kampuni ya Tour Visual Entertainment, Penda Simwita wakati akiongea na mwaandishi wa habari jana katika kambi ya kumuandaa Miss Arusha.

Alisema kuwa kwa upande wake shindano hilo limekuwa gumu kidogo, kwani warembo wengi walibweteka na kujisahau kuwa kuna shindano kama hili kwa mwaka huu, hivyo ilimlazimu kutembelea katika vyuo mbalimbali vya hapa mkoani Arusha kwa ajili ya kuwasaka warembo watakaoshiriki shindano hili.

"Pamoja na kuwatafuta,tumefaniwa kuwapata warembo wazuri wenye sifa na naamini wataweza kutetea taji la Miss Tanzania,kwani wana uwezo na kizuri zaidi najiamini naweza kuwaandaa maana hata mrembo ambaye anashikilia taji sasa hivi alitoka mkoa wa Arusha" alisema Mwandaaji huyo.

Mmoja wa warembo wanaoshiriki shindano hilo ,Maurine Ayubu alieleza hisia zake za kufurahi kushiriki shindano hilo,alisema kuwa ana uwezo wa kufanya vizuri,na kwamba ana uhakika wa kufanya vyema kwa sababu sifa zote za kuwa mrembo wa Mkoa wa Arusha anazo na kwamba anaamini atatetea taji la Miss Tanzania libaki Arusha kama linavyoshikiliwa kwa sasa na mrembo wa Tanzania Lilian kamazima

Jumla ya warembo 17 kutoka katika mitaa mbalimbali na wilaya mkoani hapa wanatarajiwa kupanda jukwaani mapema May 28 mwaka huu katika ukumbi wa Hotel ya Naura Spring kwa ajili ya kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha ambaye atawakilisha mkoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania na tukumbuke mpaka hivi sasa taji hilo la mrembo wa Tanzania linashikiliwa na mrembo kutoka mkoa wa Arusha Lilian Kamazima .

MATUKIO YALIOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA LEO.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Mei 19, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka kwa Kiongozi wa upinzani bungeni  Freeman Mbowe , mjini Dodoma Mei 19, 2016.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo akiwasilisha Makadirio ya Matumizi ya wizara hiyo bungeni mjini Dodoma Mei 19, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kwenye viwanja vya bunge jini Dodoma Mei 19 , 2016. Wapli kushoto  ni Waziri wa Ardhi,, nyumba  na Maendeleo ya Makazi,, William Lukuvi na watatu kushoto ni Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Rwakatare kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 19, 2016.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hollande: Ndege ya Misri ilianguka

 Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja wa Charles de Gaulle, Paris

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema habari zilizopatikana kufikia sasa zinaashiria ndege ya shirika la ndege la EgyptAir iliyotoweka ikiwa safarini kutoka Paris kwenda Cairo ilianguka.

Hata hivyo amesema bado ni mapema kusema kwa ufasaha kabisa nini kiliisibu ndege hiyo safari nambari MS804, na kwamba bado kuna uwezekano kwamba ilitoweka kutokana na sababu nyingine.

"Taarifa tulizokusanya kufikia sasa, mawaziri, maafisa wa serikali na, bila shaka, maafisa wa Misri, zinathibitisha, kwa huzuni, kwamba ndege ilianguka. Ilitokomea.”

Ndege ya Misri yatoweka ikitoka Paris

Moja kwa Moja: Ndege ya Misri yatoweka

Bw Hollande ameahidi kwamba serikali yake itatoa usaidizi unaohitajika na maafisa wa Ugiriki na Misri wanaoendelea na juhudi za kuisaka ndege hiyo.

Afisi ya mwendesha mashtaka wa Paris nayo imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu kutoweka kwa ndege hiyo iliyokuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.

Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmoja mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Chad na Ureno.

Waziri Mkuu wa Misri Sherif Ismail ameambia wanahabari kwamba juhudi za kuitafuta ndege hiyo bado zinaendelea.

Maafisa wa Misri na Ugiriki wanatumia ndege na meli kuitafuta ndege hiyo katika bahari ya Mediterranean.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba watu 66 ilipotoweka kilomita 16 ndani ya anga ya Misri.

Hiki ndicho kilichomkuta Msanii Malaika


Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Malaika Exavery

STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Malaika Exavery hivi karibuni yalimkuta makubwa baada ya gari lake (Toyota Harrier Lexus) kunasa kwenye tope maeneo ya Kigamboni, Dar na kushindwa kutoka kwa muda na kusababisha umati umzunguke.

Akizungumza na Tzmpya blog Malaika anayetamba na Wimbo wa Raruararua alisema siku hiyo alikuwa akitoka kurekodi Kigamboni hivyo hakujua sehemu anayopita kutakuwa na matope mazito yatakayo-sababisha garilake likwame.

“Sijawahi kutokewa na tatizo kama lile, sikuwa nikijua chochote kuhusiana na njia ile mara nikajikuta gari likishindwa kutoka. Kila mtu alinionea huruma ila nashukuru kuna gari lilitokea na kunivuta,” alisema Malaika.

Sakata la Lugumi: CHADEMA Yajipanga Kumng'oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uzito wa Rais John Magufuli kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na kutajwa kuhusika na Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kulitapeli Jeshi la Polisi, utasababisha waanze harakati za kumng’oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais John Magufuli hana budi kuchukua hatua haraka kumwajibisha Waziri Kitwanga kama alivyofanya kwa watumishi wengine wa umma katika operesheni ya kutumbua majipu.

Waziri Kitwanga anadaiwa kuwa na hisa kwenye Kampuni ya Infosys Ips Tanzania Limited ambayo ilipewa zabuni ya kutoa huduma za kitaalamu na Kampuni ya Kimarekani ya Biometrica kuhusu uwekaji wa mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi. 

Mkataba wa kuweka mashine hizo uliingiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo ililipwa Sh34 bilioni kati ya Sh37 bilioni za mkataba, wakati kazi ya kufunga mashine hizo ilifanyika kwenye vituo 14 tu hadi wakati Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipofanya ukaguzi.

Hata hivyo, kampuni hiyo inadai kuwa Kitwanga, ambaye ni mmoja wa waasisi wa Infosys, alijiondoa kwenye uendeshaji tangu mwaka 2010, wakati mkataba huo ulisainiwa mwaka 2011.

Chadema bado inaona kuwa Rais Magufuli anatakiwa kumwajibisha waziri huyo wa Mambo ya Ndani.

“Kama Rais akishindwa kuchukua hatua katika hili, Serikali itang’oka madarakani. Sisi Chadema tutaiondoa. Haiwezekani wakati Lugumi inachunguzwa mhusika mkuu (Kitwanga) aendelee kuwa waziri, tena wa wizara inayohusika na mkataba wa Lugumi,” alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema, Rais anapaswa kujitokeza hadharani na kueleza uhusiano wake na Kitwanga na awaeleze Watanzania kuwa kutokana na uswahiba wao ndiyo sababu ya kutomchukulia hatua.

“Mbona anawatumbua marafiki wa wenzake? Kwa nini marafiki zake anashindwa kuwatumbua? Ukiwa kiongozi mwenye kubagua katika uamuzi ni hatari kwa uchumi wa Taifa, ni sawa na baba anayewabagua watoto wake matokeo yake ni kuzalisha chuki tu.”

Licha ya Mwalimu kutotaka kuweka wazi mpango huo, kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.

 Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.

Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 372, kati yao wabunge wa upinzani ni 118.

“Hilo tutalifanya iwapo tu Rais atashindwa kumwajibisha Kitwanga. Ila huyu waziri naye anapaswa ajipime mwenyewe ili kumlinda bosi wake (Waziri Mkuu). Afanye kama Edward (Lowassa-waziri mkuu mstaafu) aliamua kujiuzulu wadhifa wake ili kumlinda Jakaya (Kikwete-Rais wa Awamu ya Nne) kwa kosa ambalo yeye hakulifanya,” alidai Mwalimu.

Mwalimu alidai kwamba Serikali imezuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kuhofia uchafu wa viongozi, likiwamo sakata la Lugumi.

“Ndiyo maana tunasema CCM ni ileile maana wametumbua majipu, sasa imebaki mitoki. Ni kama imewashinda maana ipo sehemu mbaya,” alisema.

Licha ya mkakati huo wa Chadema, Aprili 19 mwaka huu, Kitwanga alisema kuwa hahusiki katika sakata hilo na juzi alijibu hoja ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) lililomtaka ajiuzulu, akisema hawezi kuwajibu watoto ili kuonyesha tofauti yake na wao.

Katika maelezo yake, Mwalimu aliorodhesha utumbuaji ambao Rais Magufuli ameufanya tangu aingie madarakani, ukiwamo wa watendaji waliofanya vurugu tu katika vikao kwa kusisitiza kuwa ni ajabu kuona mpaka sasa hajamchukulia hatua yoyote Kitwanga wakati ukweli uko wazi kuwa anahusika na sakata la Lugumi. 

Baada ya ripoti ya CAG kuibua udhaifu huo kwenye mkataba, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge iliunda kamati ndogo kufuatilia tuhuma hizo baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kuhusu mkataba huo.

Kampuni ya Infosys ni wakala wa kampuni maarufu duniani ya kutengeneza kompyuta ya Dell, ikijihusisha na usambazaji wa vifaa hivyo, matengeneza na utoaji huduma za kitaalamu.

Kaimu katibu mkuu huyo wa Chadema alisema, chama hicho pia kinajipanga kuanza ziara yake nchi nzima na ajenda kuu itakuwa kuanika mambo yote mabaya yanayofanywa na Serikali.

Edward Lowassa na Fredrick Sumaye Watajwa Katika Sakata la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali.......Mbowe Atoa Ufafanuzi


Uuzwaji wa nyumba za serikali umegeuka mwiba huku wabunge wakiendelea kuhoji hatua zilizochukuliwa kutokana na kadhia hiyo

Hatua hiyo iliyotekelezwa mwaka 2002  hadi 2004 ilizusha malalamiko mengi tangu wakati huo na sasa imeibuka tena bungeni

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano jana, mbunge wa Nachingwea, Hassani Masala (CCM) alihoji mfumo uliotumika kuuza nyumba za serikali

Alisema haungi mkono kwa vile umesababisha viongozi wapya wa serikali wanaoteuliwa kujikuta wakiishi katika nyumba za wageni.

Mjadala huo uliibuliwa juzi na msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni kupitia kwa waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema kabla ya Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka kuondoa baadhi ya maneno katika hotuba yake likiweo suala la uuzwaji wa nyumba za serikali.

 Ritha Kabati Amvaa Lowassa
Akichangia mjadala huo jana, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritha Kabati alimtaja aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa alinunua nyumba ya serikali iliyouzwa mwaka 2002 yenye jengo namba 68.

Alisema hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilisema nyumba za serikali 7,921 ziliuzwa tangu mwaka 2002 hadi 2004 na kutaka serikali ya awamu ya tano kurejesha nyumba hizo kutokana na walionunua kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Naomba niwaambie usiangalie boriti lililo katika jicho la mwenzako wakati kwako lipo, kwani hata mgombea wao wa urais Edward Lowassa alihusika kwa kununua nyumba ya plot namba 68 na Fredrick Sumaye alikuwa Waziri Mkuu na kuhusika kuuza nyumba hizo,” alisema Kabati.

Baada ya kueleza hayo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliomba kumpa taarifa mbunge huyo kuwa taarifa hiyo ni kwa maslahi ya taifa, hata kama mhusika atakuwa katokea kambi ya upinzani sheria itachukua hatua.

"Kambi ya upinzani tunapoibua jambo huwa linakuwa kwa maslahi ya Taifa, hivyo ni vyema wabunge wote mtambue kuwa kosa likifanywa na kiongozi  ni lazima hatua zichukuliwe bila kujali ni wa Chadema, CUF au CCM.

"Tunapokuwa tunatoa uamuzi kama kambi ina maana sheria ifuate mkondo wake." Alisema Mbowe huku akishangiliwa na wabunge wa UKAWA

Awali katika michango mbalimbali ya wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamikia kuuzwa nyumba hizo za serikali na kudai kuwa watumishi wapya wengi walioajiriwa, wamekuwa wakikosa maeneo ya kuishi.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) akichangia mjadala huo alilalamikia kuuzwa kwa nyumba hizo pamoja na nyingine za Tazara zipatazo 500 na kuamua kumpatia Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ripoti aliyodai inaonesha nyumba hizo zilivyouzwa.

NDEGE YA MISRI YATOWEKA IKIWA NJIANI IKIWA NA ABIRIA 69 


EgyptAir flight MS804 heading from Paris to Cairo has gone missing. There were 66 people on board the A320 that vanished 20 minutes before it was set to land (model of plane that went down is pictured)
EgyptAir flight MS804 heading from Paris to Cairo has disappeared from radar with 63 people on board.
The Airbus A320 left the French capital's Charles De Gaulle Airport at 11:09pm local time on Wednesday night and then went missing, three hours and 40 minutes into its journey.
The plane vanished 10 minutes into Egyptian airspace over the Mediterranean Sea, 20 minutes before it was due to land.
It was supposed touch down at 3:05am local time. There were 56 passengers, including two infants and a child, and 10 crew on the flight.The airline tweeted: 'An informed source at EGYPTAIR stated that Flight no MS804,which departed Paris at 23:09 (CEST),heading to Cairo has disappeared from radar.'

They added that the plane disappeared 10 miles into Egyptian airspace at 37,000ft.

The airline said it was fading when air traffic control lost contact with the plane at 02:45 Cairo time.

The airline revealed that the flight had gone missing after posting this Tweet early on Thursday morning 

Egyptian officials have already sent out search and rescue teams.

Ahmed Abdel, the vice-chairman of EgyptAir holding company, told CNN that no distress signal had been sent, as far as he knew.

BREAKDOWN OF PEOPLE ON BOARD 

56 passengers (including two infants and a child)

3 security personnel

2 cockpit crew

5 cabin crew crew 

He added that there had been no reported problems with the plane when it left Paris. 

The captain of the plane, Abdel said, had more than 6,000 flying hours.

This includes 2,000 on an A320.
He also said there was no special cargo on board and the airline was not informed about any dangerous objects on board. 
As the plane was in Egyptian airspace, their air traffic controllers should have been in contact with the flight team.
However it does not necessarily mean the plane was over land at the time, as Egyptian air space stretches over the Mediterranean Sea. 
According to flight schedules, it was the plane's fifth flight of the day. 
Shortly after news of the disappearance broke, the Egyptair website crashed.
The Airbus A320 is a short-to-mid range aircraft is one of the most commonly used in the world that first entered circulation in 1986. 

They then confirmed that the flight lost contact with air traffic controllers 10 miles inside Egyptian airspace
It has a capacity of 150 passengers and a range of more than 3,000 miles. 
An EgyptAir plane was hijacked and diverted to Cyprus in March. A man who admitted to the hijacking and is described by Cypriot authorities as 'psychologically unstable' is in custody in Cyprus.
The incident renewed security concerns months after a Russian passenger plane was blown out of the sky over the Sinai Peninsula. 
The Russian plane crashed in Sinai on Oct. 31, killing all 224 people on board. Moscow said it was brought down by an explosive device, and a local branch of the extremist Islamic State group has claimed responsibility for planting it.
In 1999, EgyptAir Flight 1990 crashed into the Atlantic Ocean near the Massachusetts island of Nantucket, killing all 217 people aboard, U.S. investigators filed a final report that concluded its co-pilot switched off the autopilot and pointed the Boeing 767 downward. 
But Egyptian officials rejected the notion of suicide altogether, insisting some mechanical reason caused the crash.

A radar map shows the plane's path travelling from Paris and then stopping in the Mediterranean Sea before reaching Cairo, where it lost contact with air traffic control 

A closer locator map shows where the flight lost contact with radars. The Egyptian coast is at the bottom and Cairo is towards the bottom right corner

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo alhamis tar 19 Mei kwenye habari za kitaifa kimataifa udaku na michezo.


Naanza kwa kukuletea kilichoandikwa kwenye magazeti ya leo.usisahau kukaa  karibu nasi kwenye mitandao ya kijamii yaani twitter@tanzaniampyasasa facebook/tanzaniampyasasa blog.


 

Gallery

Popular Posts

About Us