Monday, May 09, 2016
LEO NI SIKU YA KUZALIWA YA MDAU MKUBWA NA MMILIKI WA BLOG HII BW.TITO EMMANUEL (PICHANI).
AJIRA!!! AJIRA!!!! AJIRA!!! NAFASI ZA KAZI KAMPUNI SIMU YA VODACOM- Application Deadline 11 May 2016
1. CORE JOB DESCRIPTION
Reporting to the Head of Department - Planning and Reporting: M-Commerce, this position is responsible for all data mining and analysis of M-Commerce products, including but not limited to reporting on M-Commerce operational performance, marketing initiatives analysis, key performance areas, Agents activities and various other areas as required by the division. The role will also involve to ensure completeness, Accuracy & validity of all data for all M-Commerce revenue streams so as to provide accurate and reliable information to the management and build ability to identify & quantify potential risk. Furthermore, the Business Analyst is expected to analyze different information to check for consistencies and alert management of trends that could imply a fundamental problem in the business. The job scope covers administration of management information reports, accuracy checks and trend analysis.
KEY ACCOUNTABILITIES
To Compile, analyze and review Daily, Monthly and ad-hoc management reports and ensure timely delivery of the same.
Automate existing manual reports as well as design and implement new reports as per the requirement.
Perform in depth analysis on M-Pesa tariff, subscriber segments, transaction corridors and, agents activities in relation to other GSM activities.
Creating and maintaining reporting cubes and ensures timely availability, accuracy and completeness of the same.
Liaise with Billing, Sales, Marketing and all other department interacting with M-Commerce on the new developments and making sure that M-Commerce reporting requirements standards are not compromised.
Support reporting system development and change management to ensure 100% business continuity along with performing end-to-end testing before implementing changes.
Constantly keeping upto date with new developments in Mobile Money Industry, Technology and overall Self development.
JOB DIMENSIONS
To develop and manage the reporting tools of the department with a professional, ethical and proactive approach ensuring that over all targets for division are met or exceeded.
To ensure timely data availability of the reports as and when required to facilitate management decision making.
4. QUALIFICATIONS AND TRAINING
BSC in Computer Science. Certification in database management will be an added advantage.
WORKING EXPERIENCE
At least 1 year work experience in a similar role in the Telecom Industry.
At least 5 years total work experience
CORE COMPETENCIES ( Knowledge Base, Skills Base and Behaviour Base)
Superior analytical skills
High level of competency in database management.
High level of competency in Microsoft office applications
Exceptional report writing skills
High level of problem solving skills
Very Good communication skills
Attention to detail
Honesty
Assertive personality
Integrity
QUALIFICATIONS AND TRAINING
BSC in Computer Science. Certification in database management will be an added advantage.
WORKING EXPERIENCE
At least 1 year work experience in a similar role in the Telecom Industry.
At least 5 years total work experience
CORE COMPETENCIES ( Knowledge Base, Skills Base and Behaviour Base)
Superior analytical skills
High level of competency in database management.
High level of competency in Microsoft office applications
Exceptional report writing skills
High level of problem solving skills
Very Good communication skills
Attention to detail
Honesty
Assertive personality
Integrity
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Online application, click HERE
Diamond, Wizkid, Flavour Kutumbuiza Barclays Center, New York, July 22
Na sasa Diamond, Wizkid na Flavour, watakuwa wasanii wa kwanza wanaofanyia muziki Afrika kuwahi kutumbuiza kwenye ukumbi huo. Mastaa hao watatumbuiza kwenye tamasha la muziki la One Africa July 22, 2016 kwenye ukumbi huo wenye uwezo wa kujaza watu 20,000.
“We are about to Make a History America!!!…. Platnumz Diamond with my Fellow African brothers and Sisters will be Shutting the Barclays Center Down! On the 22nd Jully 2016 in New York!…. 20k Seat Capacity!…Now make sure you tell your Friend to tell a Friend,” ameandika Diamond.
Barclays Center ni ukumbi unaotumika kwa shughuli mbalimbali na upo Brooklyn, New York City. Pia hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets pamoja na New York Islanders ya National Hockey League.
Show ya kwanza kufanyika kwenye ukumbi huo ilikuwa ya Jay Z, September 28, 2012.
SOURCE;UDAKU SPECIAL BLOG
WAZIRI APEWA MAJI MACHAFU ANYWE.
Wakazi wa Kijiji cha Nala na vitongoji vyake juzi walimpelekea maji machafu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde wakimtaka ayanywe kwa kuwa ndiyo wanayotumia.
Mavunde alikutana na mkasa huo muda mfupi alipoingia kwenye kijiji hicho umbali wa kilomita tisa nyakati za jioni, ambako wakazi wa eneo hilo walikuwa wakimsubiri tangu asubuhi.
Mama mmoja aliyekuwa eneo hilo, alifika na chupa ya maji akimtaka Naibu Waziri ayaonje mbele yao, kwani nao ni binadamu kama yeye na wanayatumia, lakini Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo alimzuia kuyanywa.Pamoja na taarifa ya kijiji iliyotolewa na Ofisa Mtendaji wa Kata, Mathias Ndologa, wakazi hao walilipuka na kupiga kelele wakiipinga taarifa hiyo kwamba iligusa kwa juu matatizo yao, lakini ikaacha jambo kubwa la maji.
Kwenye risala yake, Ndologa alikuwa ameelezea suala la maji, umeme, miundombinu na upungufu wa madawati, lakini kelele zilizidi kutoka kwa wananchi wakisema jambo la msingi kwao ni moja tu, yaani maji.
Muda mfupi kelele zilianza watu wakitaka kuuliza mambo waliyoyaita ni ya msingi, ndipo Mavunde akaamuru wapewe nafasi ya kuuliza kwanza kabla hajasimama kuwasalimia.Mmoja wa wauliza maswali alikuwa Daudi Lusinde, ambaye alieleza namna wakazi wa kijiji hicho wanavyopata adha kubwa katika kutafuta maji ambayo aliyaita ni kama dhahabu kwao.
Lusinde alisema wamepata tabu hiyo kwa muda mrefu na bado hawajaona mwanga wa matumaini zaidi ya kuendelea kuumia huku ndoo ya maji ikifikia bei ya Sh500.
“Bei ya sukari inapanda kila kukicha, lakini siyo shida hapa tatizo ni maji, mheshimiwa sisi tunanunua maji kwa gharama kubwa na ukishindwa kiasi hicho unalazimika kuchangia maji na mifugo sijui kama tutapona,” alisema Lusinde na kusababisha mkutano kulipuka kwa shangwe.
Uongozi wa kijiji na chama wilaya ulizu kelele za vijana waliomtaka mbunge huyo aende hadi maeneo wanayochota maji akajionee, ikiwamo uchafu wa maji pamoja na umbali wake.
Akijibu hoja hizo, Mavunde alieleza kusononeshwa na kuahidi kuanzia leo ataanza kutekeleza ahadi yake hiyo kabla ya kufanya jambo lolote.
“Kwa kweli maji ni moja ya ahadi nilizoahidi kwenu, kesho ni Jumapili siyo siku ya kazi, lakini kuanzia keshokutwa (Jumatatu) nitaleta hapa wataalamu kuanza kuchimba kisima kwa gharama zangu,”alisema Mavunde.
Huku akiwa amesimama na maji aliyopewa, alisema yuko tayari kuacha shughuli za Bunge akashirikiane nao kuhangaikia maji, hadi pale watakapoyapata na kuanza kujenga matangi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Naibu Waziri alisema katika kipindi cha kampeni alifika eneo hilo na kuahidi kuwapatia maji, lakini muda ulikuwa bado. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya tano ina miezi sita madarakani.
“Hiyo ilikuwa ni sehemu ya ahadi yangu kwenye kampeni, kwa hiyo matatizo ya maji hapa nayajua na kweli ni makubwa, ndiyo maana nimeamua kuvuruga kila ratiba ili niokoe watu hawa kweli wako kwenye mateso,” alisema.
Mhandisi wa Maji Manispaa ya Dodoma, Simon Sasala alisema kijiji hicho kina wakazi 7,600 ambao wanahitaji lita 230,000 za maji kwa siku, lakini kuna kisima kinachotoa lita 89,000 na wakati mwingine hakifanyi kazi.
Sasala alisema maji hayo hayatoshelezi kwani yapo kwa asilimia 39, hali ambayo inawapa shida hasa kina mama kutokana na wengi wao kulazimika kufuata maji ya kutumia umbali mrefu.