Monday, April 18, 2016
PICHA 10;Huyu hapa Mtoto mwingine wa Zari anayefanana na Diamond,jionee mwenyewe hapa
Published Under
TOP STORIES
SHARE!
Mbio za Mwenge Zazinduliwa rasmi Mkoani Morogoro
MOROGORO
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo atawasha Mwenge wa Uhuru na kuzindua rasmi mbio zake ili kukimbizwa katika halmashauri za wilaya na Manispaa zipatazo 179 za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Uzinduzi huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambao utatanguliwa na shamrashamra za halaiki kutoka kwa vijana zaidi ya 1,000 na vikundi vya utamaduni kutoka wilaya za Morogoro na nje ya mkoa huo.Katika uzinduzi huo, viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa wamealikwa kushiriki wakiwemo pia mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Miongoni mwa mawaziri ambao hadi jana walikuwa tayari wamewasili mkoani hapa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Sera, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mouldine Castico.
Mawaziri hao jana waliungana na Makamu wa Rais kutembelea mradi wa vijana wajasiriamali wa mafundi seremala eneo la Mtaa wa Betero, Kata ya Sabasaba, Manispaa ya Morogoro. Kaulimbiu za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni “Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na Kuwezeshwa.”
Baada ya kuwashwa leo, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuhitimishwa wilayani Gairo ambako Aprili 25, mwaka huu utakabidhiwa mpakani mwa wilaya hiyo na Kilindi ya Mkoa wa Tanga ili kuendelea na mbio zake.
Kwa mujibu wa ratiba ya mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, utakimbizwa katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Oktoba 14, mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu
.DOWNLOAD APP YETU YA TANZANIAMPYASASA HAPA
SHARE!
Huyu Ndiye Mrithi wa Paul Makonda Wilaya ya Kinondoni
Published Under
KITAIFA
Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli amemteua ndugu Ally Salum Hapi kuwa mkuu mpya wa wilaya ya kinondoni ili kuziba nafasi nafasi iliyoachwa wazi na ndugu Paul Makonda aliyeteuliwa Mapema mwaka huu kuwa Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam.
SHARE!
PICHA 14: Mabasi mapya ya haraka Dar es salaam kwenye majaribio April 18, 2016
Published Under
KITAIFA
April 18, 2016 Mabasi
ya abiria yaendayo haraka yalifanyiwa majaribio ikiripotiwa ni
kujiandaa na kuanza kazi rasmi ya kubeba abiria na kushusha kwenye vituo
mbalimbali vya barabara zake maalum zilizokamilika.
SHARE!
PICHA:Makamu Wa Rais Mhe. Samia Azindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkoani Morogoro Le
Published Under
KITAIFA
SHARE!
Magazeti ya tanzania yalichoandika leo jumatatuya tarehe 18 april
Published Under
MAGAZETINI LEO
A
SHARE!
Subscribe to:
Posts (Atom)