KINGAZI BLOG: 04/21/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, April 21, 2016

Diamond Platnumz, Mrisho Mpoto Walivyotajwa Bungeni Leo


Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea tena Dodoma leo April 21 2016 , shughuli nzima iliyoanza asubuhi ni maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Pia baadhi ya Wizara zilihusishwa katika maswali hayo, ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara hizo walilazimika kuyatolea majibu.

Video fupi Toyota Hiace iliyozama baharini Dar es Salaam namna ilivyotolewa



Baada ya Jumatano ya April 20 2016 kuzama kwa gari ndogo aina ya Hiace ikiwa na watu wa wawili katika bahari ya Hindi eneo la Kigamboni, nimekutana na video fupi ikionesha namna kikosi cha uokoaji kilivyotoa Hiace hiyo baharini.
HIECEEEE122
Kama utakuwa unakumbuka vizuri usiku wa siku ambayo Daraja lilizinduliwa April 19 2016 ilitolewa taarifa ya gari moja aina Toyota Hiace yenye namba za usajili T271 CRG  kuserereka kutoka kwenye pantoni na kuzama baharini. Pantoni hilo lilikuwa likivuka kutoka Posta kuelekea Kigamboni Alfajiri ya April 20 2016.

Gari Aina ya Toyota Hiace Lililozama Majini Kivuko cha Kigamboni na Kuua Watu Wawili Lapatikana


Picha likiwa linatolewa majini hii hapa:
Lile Gari Aina ya Toyota Hiace lililozama kwenye bahari kivukoni Kigamboni na kuuwa watu wawili limepatikana na kutolewa majini na wana maji baada ya Jumatano ya April 20 2016 kuzama  ikiwa na watu wa wawili ambao wote walipatikana wakiwa wameshafariki...

Hatimaye kikosi cha ukoaji cha baharini kimefanikiwa kuitoa gari aina ya Hiace ambayo jana ilizama katika bahari ya hindi eneo la Kivukoni na kuua watu wawili.

Picha 7 za Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Diamond Platnumz...Timu Zari Waendelea Kumuandama instagramu


Mashabiki wa Zari the Bosslady wanamshambulia Lynn, mrembo aliyetumika kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii wa WCB, Raymond kwasababu wamesikia tetesi kuwa amechepuka na Diamond Platnumz.

MATUKIO YA BUNGENI JANA  MJINI DODOMA APRIL 19


Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kuongoza kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge Aprili 19, 2016.

Ruth Owenya akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016.

Ritta Kabati akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016.

Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Ritta Kabati kuwa mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Spika wa Bunge, Job Ndugai akimwapisha Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 10, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2016.


LADY JAYDEE:Kiufupi ndoa yangu ilikuwa ni ya mateso tu

East Africa Television (EATV)
LadyJay Dee asema hatuja achana niliamua kumuacha
"Hatuja achana niliamua kumuacha.Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano,furaha,amani na upendo.ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo,sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.sioni kujishushia heshima,ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima,anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba.
Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini. Ukiachilia mbali vipigo.Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu.Ushahidi ninao. .....niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. bado kupigana na kuwatusi wateja pia.Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso.

SOURCE EATV

TUCTA Yapinga Mpango wa Rais Magufuli Kukata Mishahara ya Watumishi wa Umma Kutoka Milioni 40 hadi 15 Kwa Mwezi


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) limepinga mpango wa Rais John Magufuli wa kukata malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh40 milioni kwa mwezi hadi Sh15 milioni.

Bungeni: Serikali yaanza Kuzipanga Shule Katika Makundi ili Kuweka Viwango vya Ada Elekezi


Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imeanza zoezi la kupanga shule katika makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora wa huduma na kwamba haitaathiri ubora wa elimu.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). 

Mdee alitaka kufahamu iwapo Serikali imebaini kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na kutwa, iwapo hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu.

Manyanya alisema wizara hiyo imefanya utafiti kuhusu gharama za kila mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari. 

“Baada ya utafiti, wizara yangu ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia elimu kwa shule zisizokuwa za Serikali na kukubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi,” alisema.

Alisema wizara inatarajia ubora wa ada elekezi hautaathiri elimu kwa shule binafsi, kwa sababu itapangwa kulingana na ubora wa miundombinu ya shule.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema) alitaka kufahamu jinsi Serikali inavyotaka kupanga bei elekezi wakati imeifanya elimu kuwa biashara.

Manyanya alisema siyo mara ya kwanza kwa Serikali kupanga bei elekezi kwa faida ya wananchi na kwamba, imefanyika kwa upande wa huduma ya maji hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura) wamefanya.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 21 2016 kwenye,Habari zaUdaku, Kitaifa,kimataifa na michezo.

Bofya hapa Download app ya Tanzaniampyasasa 

 April 20 2016 naanza kwa kukuletea habari zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye ,habari za kitaifa,kimataifa Michezo na udaku na stori nyingine kali ili ujue kilichojiri duniani.. usiache kukaa karibu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamiiyaani facebook/tanzaniampyasasablog na twitter@tanzaniampyasasa.

WANAWAKE WAANDAMANA WAKIDAI KUKOSA WANAUME WA KUWAPA UJAUZITO



Wanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume.

Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Akhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi.
Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji

hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa.
Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao. =>

 

Gallery

Popular Posts

About Us