KINGAZI BLOG: 05/15/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, May 15, 2016

Vijana Wanaovaa Suruali Chini ya Kiuno Kuchapwa Viboko 70

Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

 

Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.
 

Vazi lingine lisilotakiwa kwa wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
 

Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria.
 

Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.
 

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.

Machangudoa waitaka serikali itambue biashara yao. Na walipe kodi pia.



Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.

Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.

" Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini" alisema Rosemary Kazeze.

Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya  hivyo kunaikosesha serikali mapato

Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.

“ Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein

Serikali Yanasa Kilo 34,000,000 za Sukari iliyofichwa.


Shehena ya sukari ya kilo milioni 34 zilizokuwa zimefichwa kwenye maghala ya wafanyabiashara watatu Kilimanjaro imekamatwa na vyombo vya usalama, na serikali mkoani humo imetangaza kuiuza kwa wananchi kuanzia jana kwa bei elekezi ya Sh. 1,800.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki alithibitisha jana kukamatwa kwa shehena hiyo, baada ya makachero wanaoongoza timu maalumu ya ukaguzi wa maghala ya wafanyabiashara na mawakala wa sukari kubaini kufichwa kwa bidhaa hiyo.

“Tumefanya ukaguzi katika maghala 45 na katika harakati hizo tumenasa kilo milioni 34 za sukari iliyokuwa imefichwa," alisema.

"Katika zoezi hilo kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa, yeye alikutwa na tani 31.33 lakini alikuwa akiiuza, isipokuwa bado tumewapa kazi Mamlaka ya Mapato (TRA) ichunguze kama imehodhiwa isivyo halali,” alisema Sadiki.

Kiasi cha sukari iliyobakia, alisema Mkuu wa M koa huyo, kilikamatwa kwa wafanyabiashara wengine wawili, ambao walikuwa na tani nne kasoro, Moshi mjini na Marangu.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, shehena hiyo ya sukari hadi jana mchana ilikuwa ikishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kiuchunguzi na kwamba ametoa amri igawiwe kwa wananchi kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali.

Kuhusu upungufu wa sukari Kilimanjaro, Sadiki alisema "Sisi kama mkoa tumefanya mawasiliano na mawakala walioko Dar es salaam, ambao sukari yao ilikuwa inashikiliwa na vyombo vya usalama na wametuahidi kuukabili uhaba wa sukari uliopo hapa kwetu.

“Jana (juzi) niliwasiliana na Mmiliki wa Kampuni ya Zakaria Enterprises na amekubali kuwapa bidhaa hiyo mawakala ambao ni wadau wa Kiwanda cha Sukari cha TPC," alisema Sadiki.

"Kwa hiyo tunakwenda vizuri na tumejipanga kuhakikisha kwamba uhaba huo tunaupatia ufumbuzi wa kudumu.Ila ninawaomba wananchi wangu wawe wavumilivu kwa sasa.

"Mawakala wakubwa wa sukari wa Kilimanjaro na mikoa ya Kanda ya Kaskazini ni mfanyabiashara Vicent Laswai ambaye atapatiwa tani 600 za sukari kutoka Kampuni ya Zakaria, alisema Mkuu wa Mkoa huyo.

Aidha, Laswai atapokea tani 640 toka katika Kampuni ya Mohamed Enterprises, alisema.

Kampuni ya Zakaria pia imekubali kutoa tani 640 kwa Kampuni ya Marenga Investment, alisema Sadiki na kubainisha kuwa Mohamed Enterprises imemuahidi kuziba pengo la upungufu utakaojitokeza.

Tangu Rais Magufuli apige marufuku uingizaji sukari kutoka nje ya nchi Februari 17 mwaka huu, baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakificha bidha hiyo kama njia ya kuihadaa serikali kwamba kuna uhaba mkubwa.

Wakati akipiga marufuku, Magufuli alisema kama kutakuwa na uhitaji wa sukari kuingia nchini, vibali atavitoa yeye si mtu mwingine yeyote ili kuviwezesha viwanda vya ndani viendelee kuzalisha bidhaa hiyo, kuendelea kutoa ajira na kuinua kipato cha wakulima wa miwa.

Alisema inasikitisha kuona sukari ikiingizwa nchini kutoka nje wakati nchi ina viwanda vingi vya bidhaa hiyo na kusababisha Watanzania wengi kupoteza ajira kutokana na sukari wanayozalisha kukosa soko.

"Nakuagiza Waziri Mkuu, kuanzia leo, marufuku mtendaji yeyote wa Serikali kutoa kibali cha kuagiza na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi...vibali vyote nitatoa mimi," alisema Rais Magufuli.

"Katika kampeni zangu mwaka 2015, nilisema Serikali yangu itakuwa ya viwanda hivyo lazima tuvithamini viwanda vya ndani na kulinda bidhaa zinazozalishwa."

Rushwa inahitaji nguvu ya pamoja kuikomesha-Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani ni kiashiria kwamba tatizo la rushwa ni kubwa sana na linataka juhudi za pamoja kukabiliana nalo.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening walipokutana kwenye mkutano huo uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.
Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais John Magufuli, alimweleza Greening kwamba viongozi wa Serikali wa Awamu ya Tano wameamua kupambana na kila ovu linalotokana na janga la rushwa na pia wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongozi mwa watu wetu,” alisema.
Alipoulizwa ni kitu kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hii, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe au kupokewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.
“Serikali inachukua hatua za kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi mwezi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.
Greening alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalumu wa kushiriki mkutano huo kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali.

WHO yaeleza kuwa hewa chafu yazidi kuathiri dunia



Utafiti huo umegundua kwamba hali chafu ya hewa imeongezeka mara mbili zaidi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita katika miji elfu 3 kwenye nchi 103.

DC Kinondoni akemea vigogo wa sukari wanaompigia simu


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amefichua kuwa amekuwa akipigiwa simu na baadhi ya wafanyabiashara vigogo wenye nia ya kutaka kupunguza makali ya operesheni inayofanywa na wilaya yake dhidi ya waficha sukari.

Kwamba simu hizo amekuwa akipigiwa hadi usiku wa manane na huku wengine wakimtumia ujumbe mfupi wa simu wa maandishi (SMS). Amekemea wafanyabiashara hao na kutaka waache mara moja mchezo huo, kwani vyombo vya dola vinaendelea kuwafuatilia.

Hapi alisema hayo jana wakati akizungumzia suala la Uadilifu kwenye Mkutano wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wanaotokana na shirikisho hilo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba amekuwa hapokei simu hizo na SMS hizo za wafanyabiashara wakubwa kutokana na sababu mbalimbali. “Sababu ya kwanza sina sababu ya kuzipokea, lakini pili nahofia nikizipokea nitarekodiwa na wafanyabiashara hao na sauti yangu itasambazwa kwenye mitandao, kuonesha nipo pamoja nao.

“Wakati mwingine mpaka usiku wa manane wanapiga simu na kutuma meseji na wengine wanajitambulisha. Lakini huwa namuonyesha mke wangu na kumwambia sina sababu ya kuzipokea, kwani naweza nikapokea lakini katika mazungumzo yetu nikasema neno ‘sawa’, kisha neno hilo linaweza kusambazwa katika mitandao kuonyesha kwamba nia yetu ni moja ya kuficha sukari”, alisema Hapi.

Alisema hao wafanyabiashara wanaoficha sukari, wanaleta madhara makubwa kwa jamii na uchumi wa nchi, kama vile kuua viwanda vya sukari nchini. Alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiweka ‘oda’ katika viwanda vya sukari kuchukua bidhaa hiyo, lakini hawaendi kuichukua kwa madai ya kwenda kuichukua siku za baadaye, lengo likiwa kuificha. Hapi aliwaomba wakazi wa wilaya ya Kinondoni, kuendelea kuisaidia serikali kufichua watu wote walioficha sukari.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo jumapili Mei 15 kwenye habari za kitaifa,kimataifa na michezo.

Mei 15naanza kwa kukuletea habari zilizoandikwa kwenye magazeti ya Leo kwenye habari za kitaifa kimataifa na michezo ili ujue kilichojiri duniani.Pia usiache kukaa karibu nasi kwenye mitandao ya kijamii yaani Facebook@tanzaniampyasasa blog ma Twitter @Tanzaniampyasasa.karibu.


Mashine "iliyotumbuliwa" na JPM Uwanja wa Ndege Imepona na Inafanya kazi Kwa Ufasaha

Hatimaye mashine iliyotembelewa na Rais JPM jana na kukutwa ikiwa mbovu au haifanyi kazi kwa ufanisi sasa inapiga mzigo kama kawaida na ikiwa chini ya uangalizi wa Maafisa Usalama wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege,Polisi na Afisa wa TRA.

Mashine hiyo aina ya Rapscan inayotumika kukaguwa mizigo ya abiria wanaoingia Dsm kutoka Znz,na mikoa mingine ya Tanzania,mapori ya Utalii kama Selous,Mikumi,Sadani na Ruaha pamoja na wasafiri wa nje ya nchi.Ikumbukwe kuwa palikuwa na "uzembe" wa abiria wanaoingia nchini kupitia eneo la TB One,uwanja wa Terminal One una "Status" ya "General Aviation" kwa maana huruhusu kutua ndege za abiria,mizigo na kukodishwa,ambazo zinaweza kuwa za kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi

Kwa maana hiyo,Arrival ya Terminal One ni tofauti na ile ya Terminal Two,sababu ya Teeminal Two imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni "Domestic Arrival" na "International Arrival",hivyo ndege nyingi za domestic katika Terminal Two mizigo ya abiria haina haja kukaguliwa sababu watu wanatoka mkoa mmoja ndani ya nchi kwenda mkoa mwingine,na wale wanaotoka nje ya nchi hawachanganyikani na wa ndani ya nchi

Uwanja wa Terminal One "Arrival" hiyo hiyo moja hutumika na abiria wa kutoka Zanzibar,Mikoani,Mbuga za Wanyama(Porini) na nje ya nchi.Hivyo kuwa na Mashine mbovu eneo la Arrival ambayo inahudumia watu wanaopita toka Zanzibar(Wakiwa na mizigo ya kibiashara kwa nia ya kukwepa ushuru) na nje ya nchi ni "kosa" kiutendaji.Wapo watu kama Pasco wa JF wanaodhani JPM kakurupuka,wasijuwe kuwa "status" ya Terminal One Arrival sio kama ile ya "Domestic Terminal Two"

Vijana wa JPM,hatumpi vitu vya kukurupuka,anapewa data zilizoshiba,ndio maana akifika anaenda moja kwa moja.Jana baada ya kuongea tu kufika saa kumi mashine zikawa zimetengenezwa na mizigo inakaguliwa kwa ufanisi mkubwa.Simu nyingi zilizokuwa zinapitishwa kinyemela toka Dubai via Zanzibar kuja Dsm zimeanza kunaswa,mali pori zisizo na vibari zinaonekana na hivyo kuwa na uhakika wa kutambua nini na nini kinaingia nchini.

Kwa taarifa tu ni kuwa Wamiliki wengi wa ndege Terminal One ni wafanyabiashara wa uwindaji na utalii,matengenezo ya ndege zao hufanyika nje ya nchi,hivyo hufanya udanganyifu wa kwenda porini na kubeba mali pori,kurudi Dsm bila kuushusha mzigo,na baadae kusafiri kwenda nje ya nchi na mzigo "kimyakimya",na wakati ndege zikirudi toka nje huja na bidhaa ambazo ni "dutable",na baadae kuingia nchini bila kutozwa kodi

Ujanja mwingine uliokuwa unatumika na wafanyabiashara wengi ni kushusha mzigo Zanzibar na baadae kuuleta Dsm na ndege za Charter na hivyo kukwepa kosi,Ndege ya Qatar na Oman Air hutua Zanzibar,hivyo wafanyabiashara wengi huja na bidhaa na kuzishusha Znz na baadae wanakuja kama abiria kupitia Terminal One na hivyo kuingiza nchini bidhaa nyingi bila kulipa kodi,kwa mashine ile kutokutumika vizuri basi Taifa limepoteza mapato mengi kwa muda mrefu

JPM kwenda pale jana hajakurupuka,ni matokeo ya jitihada za kumuonyesha sehemu ambapo kuna mianya ya ukwepaji kodi.., Twende JPM ipo siku watakuelewa,hasa utakapoanza kuiachia hela unayoikusanya sasa,wacha tule ugali dagaa kwa muda..Msosi wa uhakika mezani unakuja

UN: Uhusiano wa Boko Haram na IS ni tishio


BOKO HARAM Uhusiano wa Boko Haram na Islamic State

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu kasi ya kuimarika kwa ushirikiano kati ya kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria na lile la Islamic State, wakati Nigeria inaandaa kongamano la kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza hilo la wanachama 15 limesema kuwa Boko Haram linaendelea kuwa tishio kwa amani na usalama wa mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika ya kati.

Wapiganaji wa Boko Haram

Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa Islamic State mwaka jana, na inaripoitiwa kuwa liliwatuma wapiganaji wake kuungana na Islamic State nchini Libya.

Baraza hilo pia limekaribisha kongamano lililoandaliwa na rais wa Nigeria Mohamadu Buhari siku ya Jumamosi, kuangazia upya jitihada za kupambana na wapiganaji hao.

Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Kongamano hilo litahudhuriwa na viongozi wa kikanda pamoja na rais wa ufaransa Francois Hollande

JINSI TABIA INAVYOWEZA KUKUFANIKISHA AU KUKUFELISHA MAISHANI

Michael Jackson.

Kama vile mmea unavyoweza kupandwa kwenye mbolea ukaota, kukua na baadaye kuzongwa na magugu ambayo huudumaza na hatimaye kama hayatang’olewa kuua, ndivyo ndoto za mwanadamu na mafanikio yanayoweza kujengewa tabia njema ya kukua lakini baadaye tabia mbaya ambazo huja na mafanikio zikaua kila kitu.

Withney Houston.

Ili mwanadamu afanikiwe maishani mwake ni lazima awe na tabia pamoja na mwenendo unaovuta au kuchochea mafanikio, zipo tabia za namna hiyo maishani ambazo mwanadamu akizifanya na kuzifanya ziwe sehemu ya maisha yake, mafanikio humfuata hata kama hayataki! Lakini ziko tabia ambazo mwanadamu anaweza kuzianzisha maishani mwake, zikaota mizizi na kuwa sehemu yake, ambazo hukwamisha kabisa mafanikio na hata kama kuna kipaji zinaweza kukiua kisimletee manufaa yoyote maishani.

Wapo watu wengi waliozaliwa na vipaji vya kuimba, kuandika, kucheza mpira na kadhalika lakini kwa sababu ya tabia fulani walizozianzisha maishani mwao, vipaji hivyo vilikufa kama ambavyo mmea hufa ukizongwa na magugu.

Tabia mbaya zinatesa watu, zimerudisha watu nyuma, zimefanya watu waliotakiwa kuwa mabilionea wafe wakiwa maskini, waliotakiwa kuandika vitabu au kugundua dawa za kutibu magonjwa, walikufa bila kufahamu kwamba hiyo ndiyo ilitakiwa kuwa hatima yao kwa sababu ya tabia mbaya ya hofu.

Tabia zote mbaya na nzuri hujengwa, hakuna mwanadamu aliyezaliwa na tabia mbaya au nzuri, zote tumezitengeneza sisi wenyewe wakati tunakua, nazo baadaye hugeuka kuwa vichocheo au vigingi vya sisi kuelekea kwenye mafanikio! Kila mwanamke anapozaa mtoto, watu husema tu “mama fulani amezaa mtoto wa kike au wa kiume!” Hakuna mwanamke hata mmoja ambaye huzaa halafu watu wakasema “leo mama fulani amezaa jambazi” au “mama fulani amezaa mteja wa unga!” au “mama fulani amezaa mzinzi!” wanawake wote huzaa watoto wazuri wanaovutia, lakini watoto hawa ukiwafuatilia baadaye maishani mwao huishia kuwa na tabia fulani ambazo hawakuzaliwa nazo, bali walijifunza wakati wanakua.

Ziko tabia zinazochochea maendeleo au kuvuta mafanikio kumfuata mtu, ukiwaangalia watu wengi waliofanikiwa maishani huwa na tabia za kufanana na miongoni mwa tabia hizo ni; UADILIFU, UAMINIFU, USEMA KWELI, DHAMIRA NA UCHAPAKAZI NA HOFU YA MUNGU.Mtu mwadilifu na mwaminifu huwavuta watu wengi sana kufanya naye kazi, watu wengi wanataka kuhusiana na watu waaminifu na waadilifu badala ya matapeli na watu waongo wasiosema ukweli! Vilevile watu wavivu wasio na dhamira ya kufanikiwa na hata wasio na hofu ya Mungu, huvuta watu wachache sana kushirikiana nao.

Watu wengi wenye tabia mbaya hujitenga wao wenyewe au kutengwa na jamii bila kufahamu, kwa sababu hiyo bahati ambazo siku zote maishani mwetu huletwa na watu huwa haziwafikii kirahisi kwa sababu sifa zao mbaya huwa zimesambaa! Hivyo basi mwanadamu anaweza kuwa hana fedha, lakini sifa yake ya uadilifu na uaminifu ikamfanya aungane na mtu mwenye fedha anayetafuta watu wa kushirikiana nao, ndiyo maana kuna msemo usemao uaminifu ni mtaji.

Kama tunataka kufanikiwa maishani ni vizuri sana kujiepusha na tabia mbaya ambazo tumezitengeneza wenyewe maishani mwetu na zimegeuka kuwa vikwazo au vigingi kwenye maendeleo, tabia hizi zipo, lazima ziondolewe kama kweli mtu amedhamiria kubadilisha maisha yake.

Hakuna mwanadamu aliyekamilika kila mmoja wetu analo eneo fulani maishani mwake ambalo anapambana ili awe bora, hivyo basi kama unafahamu tatizo lako ni matumizi mabaya ya fedha au ulevi au uzinzi au matumizi ya dawa za kulevya, tabia ambazo zimekukwamisha kusonga mbele ni lazima uziue tabia hizo mara moja ili upate kufanikiwa.

Ni kweli ni kazi ngumu sana kuua tabia ambayo umeijenga kwa muda mrefu, lakini inawezekana kabisa kufanya hivyo, utaumia lakini baadaye utasikia furaha! Si lazima uikate tabia hiyo mara moja, unaweza kupunguza kila siku hatimaye ukakata mizizi yake kabisa.

Mfano kama unakunywa bia ishirini kila siku na hizo ndizo zinazomaliza fedha zako ambazo ungezitumia kujenga nyumba au kuwekeza, unaweza kupunguza bia mbilimbili kila siku hatimaye siku moja utajikuta hujanywa bia kabisa na kuendelea na maisha hayo.

Wakati unapunguza bia unakuwa na jambo jema unalolianzisha kwa ajili ya kuchukua nafasi ya bia huku ukiwaepuka marafiki ambao siku zote walikuchochea kuendelea na tabia hiyo. Haya yakifanyika unaweza kung’oa tabia zote mbaya katika maisha yako na kuanzisha tabia njema zitakazokuwezesha kusonga mbele.

Waziri Mkuu: Tanzania Kushirikiana Na Jumuiya Ya Madola


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Jumuiya ya Madola inaweza kuiga mbinu ambazo Tanzania imetumia katika kupambana na rushwa zikiwemo za kujumuisha wadau tofauti kwenye vita hiyo.

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bibi Patricia Scotland walipokutana kwenye mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na ninyi katika kujenga timu hii na ili uweze kupata picha halisi, nakukaribisha Tanzania uje ujionee hatua ambazo tumechukua hadi kufikia hapa tulipo kwenye vita hii dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Alimweleza Katibu Mkuu huyo kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kupambana na rushwa kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa wananchi.

“Wananchi wanafurahia juhudi za Serikali, vyama vya kiraia pia vinaunga mkono jitihada zetu na vyombo vya habari vinashirikiana nasi katika vita hii,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa wito huo baada ya kuelezwa na Bibi Scotland kwamba anataka kuanzisha idara malum kwenye Jumuiya hiyo ambayo itasimamia mapambano dhidi ya rushwa na makosa ya jinai.

“Nataka tuwe na idara yenye watu mahiri wa idara za uhasibu, mahakama yenyewe ikiwemo waendesha mashtaka na wanasheria kutoka kwenye nchi kadhaa ili washirikishane uzoefu kutoka kwenye nchi zao. Ninaamini katika nchi 53 ambazo ni wanachama wetu, sitakosa watu wa aina hii,” alisema.

Alisema ameamua kufanya hivyo ili aweze kuendanana na malengo makuu matatu ya jumuiya hiyo ambayo ni kupiga vita rushwa, kuhimiza utawala bora na usimamizi wa demokrasia.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

Chelsea yawapa tuzo wachezaji wake, Terry abaki


Matajiri wa London timu ya soka ya Chelsea jana usiku ilifanya hafla fupi yakuwatuza wachezaji wake waliofanya vema katika michuano mbalimbali kwa msimu huu wa 2015/2016.

Katika tuzo hizo nyota wa Brazil, Willian amefanikiwa kufunika usiku huo baada ya kutwaa tuzo mbili kubwa moja ya kuwa mchezaji bora wa mwaka wa labu hiyo na nyingine ya kuwa mchezaji Bora Chaguo la Wachezaji wa Mwaka wa klabu hiyo baada ya kushinda usiku wa jana katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge, London.

Mbali na Willian kushinda tuzo hizo, Eden Hazard ameshinda tuzo ya kufunga Goli Bora la Mwaka, huku kinda mwenye uwezo mkubwa Ruben Loftus-Cheek naye akishinda tuzo ya Mchezaji Bora chipukizi wa Mwaka.

Kinda mwingine mwenye ufundi mwingi kiwanjani Fikayo Tomori ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Akademi na mwanadada Katie Chapman yeye akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka.

Wakati huo huo Chelsea imempa ofa ya Mkataba mpya wa mwaka mmoja, Nahodha wake, John Terry na sasa ni juu yake kubaki au kuondoka Stamford Bridge msimu ujao.

Terry na wakala wake, Paul Nicholls, wamekutana na Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia na Mwenyekiti, Bruce Buck kwa mazungumzo katika viwanja vyao vya mazoezi vya Cobham wiki hii.

Klabu hiyo imethibitisha leo kwamba Terry anaweza kubakia baada ya Juni 30, wakati Mkataba wake utakapomalizika, ingawa Chelsea imemuachia mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 kuamua kama atabakia ndani ya kikosi hicho kinachotumia dimba la Stanford Bridge jijini London au ataamua kusaka maisha mahali pengine au hata kutundika daluga zake.

Msemaji wa klabu amesema; "Marina Granovskaia na Bruce Buck wamekutana na John na wakala wake na kumpa ya Mkataba wa mwaka mmoja abaki,".

"Na wakati msimu unaelekea ukingoni, haya ni maamuzi mazito kwa John na familia yake na kitu ambacho wanakifikiria kwa sasa,".

Mashabiki wa Chelsea walikuwa wakimpigia debe Nahodha huyo usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield wakitaka Terry aongezewe Mkataba mpya huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonyesha mataji mengi ambayo klabu ilishinda chini ya uongozi wake.

Pamoja na kwamba umri umeenda na kiwango kimeshuka, lakini Terry bado ni kipenzi cha mashabiki wa Stamford Bridge haswa wanapokumbuka mchango wake enzi zake akicheza kwa jihadi na kuwa kizingiti kwa washambuliaji hatari langoni.


 

Gallery

Popular Posts

About Us