Mbwana Ally Samata amezaliwaTarehe 7 mwenzi wa 1 mwaka 1992 katika mkoa wa Dar es salam. Katika maisha yake ya soka alianza kucheza mpira katika klabu ya African Lyon kwa muda wa miaka miwili kutoka 2008 hadi 2010 alipohamia katika klabu ya Simba na kucheza mwaka mmja tu.
Mwaka 2011 alihamia katika klabu ya Congo ambayo ni TP Mazembe aliweza kufunga magoli 60 pia katika timu ya taifa ya Taifa stars amefunga magoli 9. Samatta anajulikana sana katika mji wa Lubumbashi kwa kuwa alifunga magoli sita katika mashindano ya ligi ya mabingwa Africa na kuiwezesha Mazembe kutwaa kombe hilo.
Samata amekuwa mfungaji bora katika ligi ya mabingwa Africa pia Tarehe 7 mwenzi wa 1 mwaka 2016 Samata ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa Africa kwa wachezaji wa ndani pia ni mtanzania wa kwanza kutwaa taji hilo la ligi ya mabingwa Africa pamoja na Thomas Ulimwengu.
Baada ya kuwasili Tanzania Samata alipokelewa vizuri sana na watanzania akiwemo waziri wa habari na micheza Nape Nnauye pia Mh Zitto Kabwa na kufanyiwa Sherehe za kumpongeza katika sehemu mbalimbali Dar es salam. Kikwete alimpongeza na kumpa jezi ya TP M azembe pia mh. John Pombe Magufuli alimpongeza pia